Rais Kikwete atengua uteuzi wa DC wa Kishapu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete atengua uteuzi wa DC wa Kishapu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, Apr 26, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Rais Kikwete atengua uteuzi wa DC wa Kishapu

  Na Julius Sazia, Shinyanga
  Source: Mwananchi


  RAIS Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu, Anatory Choya muda mfupi baada ya kumtangaza na badala yake akamteua mwingine, Abdul Suleiman Lutavi.

  Habari zilizopatikana zinaeleza kutenguliwa kwa uteuzi wa Choya ambaye ni mbunge wa zamani wa Biharamulo Magharibi mkoani Kagera, kutokana na kukamatwa na Takukuru na kufunguliwa kesi ya kutoa rushwa wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Biharamulo mwaka jana, nafasi ambayo alishinda.
  Kesi yake namba 270 ya mwaka 2008 inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo na wiki iliyopita, Aprili 17 mwaka huu ilitajwa na inatarajiwa kutajwa tena Mei 11 mwaka huu.

  Jumatatu wiki hii wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Shinyanga, pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwake walipigwa na butwaa baada ya kushuhudia akiapishwa Lutavi badala ya Choya.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Dk Yohana Balele alimwapisha Lutavi na kuwafanya watu kuhoji kimya kimya nini kilichofanya Choya kushindwa kuapishwa na hakuna maelezo yaliyotolewa.

  Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zinaeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete, alitengua uteuzi wa Choya kutokana na taarifa zilizoifikia ikulu kuwa Choya, anakabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani.

  Afisa Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Jonathan Simkoko alipohojiwa na Mwananchi Jumapili alidai mara baada ya uteuzi huo, ofisi yake ilifanya maandalizi yote ya kumpokea mkuu mpya wa wilaya kwa kumtuma dereva wa halmashauri hiyo kumfuata Choya na familia yake wilayani Biharamulo kwa ajili ya kuapishwa.

  Alisema wakati Choya na familia yake wakiwa njiani kuelekea Shinyanga walipofika katika Kijiji cha Tinde mkoani Shinyanga, mkuu huyo alipokea simu kutoka ikulu ikimuarifu asiripoti kwanza kwenye kituo chake kipya na badala yake aende mara moja jijini Dar es salaam ikulu kwa maelekezo zaidi. Simkoko alisema walichokifanya ni kumpeleka moja kwa moja uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya safari ya ghafla ya kuelekea Dar es Salaam.
  Alisema waliamua kuitafutia hoteli familia akiwamo mkewe, kaka yake na mtoto wao mmoja mjini Shinyanga kumsubiri hadi atakaporejea kutoka jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Simkoko, Choya aliporejea kutoka Dar es Salaam, alifuatwa na gari la wilaya Uwanja wa Ndege Mwanza na kuwaeleza walioompokea kuwa, 'mambo yameshaharibika'.
  Baada ya hapo wakamsafirisha hadi Shinyanga kuungana na familia yake ambayo ilikuwa imeshakaa hotelini kwa siku tatu.

  Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya ya Biharamulo na familia yake walisafirishwa kwa njia ya barabara kupitia Kahama kurejea wilayani kwake. Mwananchi Jumapili lilipowasiliana na Choya, alikiri kuwa ni kweli alisimamishwa kuripoti kwenye kituo kipya cha kazi lakini akabainisha kuwa hadi jana, alikuwa hajui sababu zilizosababisha mabadiliko hayo ya ghafla.
  "Kwa sasa (jana jioni) niko njiani naenda Dar es Salaam ili kujua sababu zilizosababisha hali hiyo," alisema Choya alipokuwa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

  Alisema kuwa alipata taarifa hizo akiwa safarini pamoja na familia yake kwenda Kishapu lakini baada ya kueleza, ilibidi airejeshe familia yake nyumbani. Kuhusu kukabiliwa na kesi ya rushwa, Choya alikiri lakini akasema ni vigumu kutoa maelezo juu ya kesi hiyo kwa njia ya simu na isitoshe alikuwa kwenye basi. Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili, wamesema kuwa wateule wa rais ngazi za wilaya na mkoa wawe wanaziacha familia zao nyumbani hadi pale wanapoapishwa ndipo wanasherehekea kwa vile wakati wowote rais anaweza kutengua uteuzi huo na kuleta tafrani katika familia.

  Wakati wa kuapishwa kwa Lutavi, Dk Balele aliahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa mkuu huyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo mkoani Shinyanga hasa katika sekta ya elimu, afya, kilimo na mifugo ambazo alidai bado ziko nyuma. Kwa upande wake, DC Lutavi, aliomba ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi katika kufanikisha shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Kishapu ambayo inakabiliwa na umaskini licha ya kuwepo mgodi pekee nchini wa almasi wa Mwadui.

  Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani aliithibitisha jana kutokea kwa mabadiliko hayo ya uteuzi na kwamba hilo limefanyika kutokana na mamlaka ya Rais ya kuteua na kubatilisha wakati wowote. Hata hivyo, alisema ofisi yake haina taarifa za sababu zilizomfanya rais kutegeua uteuzi wa Choya. Juhudi za kuwasiliana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, hazikuzaa matunda jana kuzungumzia suala hilo.

  Machi 27 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya nchini na kuwastaafisha saba, akiwamo Choya, kuwateua wapya 15 na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.

  Aliyekuwa DC wa Kishapu kabla ya mabadiliko hayo, Khadija Nyembo, alihamishiwa wilaya ya Chato mkoani Kagera.

  Choya aliyekuwa mbunge kwa kipindi kimoja (2000-2005) shindwa ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2005 na kufungua kesi mahakamani kupinga ushindi wa hayati Phares Kabuye (TLP) na matokeo yake kutenguliwa miezi 20 baada ya uchaguzi huo baada ya mahakama kuridhika kuwa mdaiwa alitumia lugha ya matusi wakati wa kampeni.

  Hata hivyo, Kabuye hakuridhika na hukumu hiyo alikata rufaa ambayo hadi juzi alipofariki dunia katika ajali ya Basi mkoani Morogoro, ilikuwa haijasikilizwa.
   
 2. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Hii nchi kweli usanii umezidi ,ina maana wakati anamteua alikuwa hana taarifa/rekodi zake
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Uwizi mtupu!

  Kama kweli hivi vyeo ni vya kuwatumikia wananchi kwa nini mtu akiteuliwa afanye sherehe?

  Ndo maana nchi hii inazidi kutia nanga ktk umaskini..
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  nilisha sema siku moja kuwa Usalama wetu wa taifa ni ziro!!
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hawa usalama wa Taifa wako wapi ??hadi mtu anapita kwenye vetting kweli ??inatia shaka hii hali ipo siku watateua mu marehemu stay tuned utajasikia tu....
   
 6. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna shida gani kufurahi ukipata nafasi kubwa zaidi ya kuwatumikia wenzio/watu? kwanini uchukie?
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  kweli sasa hakuna kabisa usalama wa taifa na pia rais sasa hana msaada wowote kutoka kwa watu wa usalama, na ndio maana last time alipigwa mawe saa za usiku, rais unaenda wapi usiku
  huyu jamaa kapewa majina tu na watu wake wasioaminika, kumbe jamaa ni kimeo na jamaa alishaanza na vijisherehe na kutumia gharama za serikali kuamishia familia hotelini hata kabla ya kuapisha WIZI MTUPU
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wewe ni mgeni ktk nchi hii?
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duuu?? ama kweli nchi inatawaliwa kwa mwendo mdundo..

  Mimi nilidhani teuzi kama hizi raisi huwa haamki kitandani na kupachika yeyote cheo, nilidhani huwa usalama wa taifa wanapitia majina hayo na raisi hujiridhirisha na hapo ndipo teuzi hutangazwa!

  Sijui kwakweli kwa mendo huu kama tutafika. Ndo maana hata mzee wa vijisenti hakumkopesha kumpiga kijembe walipo muuliza kwanini aliteuliwa uwaziri wakati anashutuma kibao, akawambia kamuulizeni aliye niteua!

  JK please!
   
 10. T

  Tom JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wote hao wanateuliwa kumtumikia RAISI na kuilinda CCM, ukweli hakuna ambaye yupo kwa ajili ya watu.
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  shida hipo, sasa hata madarakani hujaingia unahamishia na familia hotelini na kwa mlolongo wa kitanzania hapo hotelini palikuwa hapatoshi Mke, Watoto, Hawara, Mganga wa kumuweka sawa, na mpambe wa karibu (mleta majungu)
  tatizo lingine hata hiyo sherehe ilikuwa inaingia kwenye mahesabu ya serikali
   
 12. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hata Wema Sepetu au Stephen Kanumba they could run this country better. Seriously, this guy is terrible. Be sure to get a NO vote from me next yr.
   
 13. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwa ubavu huo huo alikuwa nao Raisi wetu pia angeliutumia kumnyang'anya madaraka yote mwizi na fisadi Chenge ingekuwa poa ile mbaya. Maana Chenge na huyo jamaa aliyepigwa chini U-DC wote ni watuhumiwa tu.
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hii inadhihilisha kuwa watu wanamchomekea Jk uteuzi wa watu na yeye anaanguka tu!! Huyu jamaa mchovu kweli hata hajui kuwa anaemteua ana kesi mahakamani?? It means katika appointments zao hawafanyi background check kujua tabia za hao wanaowapendekeza!! Ndio maana hata maharamia wanapata vyeo nchi hii!!
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  cheap publicity ya takuru eti wanafanya kazi, wakamkamate kwanza RA, EL na manji
   
 16. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  a one day wonder!! duh kweli kama walivyosema wakuu kabla yangu.... WE ARE NOT SERIOUS!!!!!! nafahamu tunapotoka lakini for sho sidhani kama tuna "any clue" of where we are heading to!!

  hii ni uzembe wa hali ya juu sana.... inadhibitisha sasa kwa nini makampuni, mawizara na pote ambapo viongozi wake ni appointees wa "bwana mkubwa" ni bure kabisa na wizi, uchafu na uzembe unaopelekea vifo vya taasisi, kampuni zetu!!!
   
 17. m

  mnozya JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hapo ni dalili kuwa vyombo vinavyomsaidia rais kama vile usalama wa Taifa havikufanya kazi yake ama Rais hakutaka kuvitumia.
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaelekea tuna viongozi wengi wasiofaa kuwepo kwenye nafasi walizopo. Lakini shida ninayoiona hapa ni kuwa hakuna mtu atakayejihangaisha kutafuta ilikuwaje mpaka jina la mtuhumiwa wa rushwa linafika kwa rais kwa ajili ya uteuzi wa nafasi kubwa kama hii
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Rais wa sasa huwa ana mazuri na mapungufu yake, na hili ni moja ya mapungufu yake ya kuweka uswahiba mbele na taifa nyuma,

  - Reading between the lines hapa ni kwamba huyu DC atakuwa ni either swahiba wake au rafiki wa swahiba wake Muungwana aliyemuahidi kumpa mlo kwa hiyo time ilipofika akampa tu, bila kujali venting process, that is Muungwana na tunaye for the next Six years.

  - Kwenye hili usalama hawana kosa lolote!

  FMES!
   
 20. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kumbukeni imani ya serikali kwa wananchi wa wilaya hiyo imeshapotea. Wanafanya kile tunachokiita systematic error na kuchezea hisia za wananchi. Sio kwamba usalama hawafanyi kazi bali wanafanya kwa kutengeneza hizo systematic errors. Ni sehemu ya kazi ingawa kwa sehemu kubwa ni kwa ajili ya kuulinda utawala uliopo ingawa umeshindwa kudeliver. Kumbuka huyo -DC mtenguliwa alikuwa na tuhuma kwenye jimbo ambalo lina upinzani sana. Alikuwa ndiye mbunge wa zamani (2000-2005) katika wilaya hiyo kabla ya kuangukia mikononi mwa TLP na alikuwa na mpango wa kugombea tena. Wananchi wengi walikuwa na hasira nae. Na selikari kwa kumteua kuwa DC basi ndipo walipochochea hasira za wananchi. Na serikari ili kupata popularity kwa wananchi walichofanya ni kumteua huyo mtuhumiwa katika nafasi ya u DC. Walipopata hisia za wananchi ndipo wakatengua uteuzi. Hivi sasa usishangae biharamuro watu wanamsifia rais kwa kutengua huo uteuzi na kuonyesha ufanisi wa kazi kwa kusikia kilio chao.
   
Loading...