Rais Kikwete atapeliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete atapeliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fidel80, Jul 24, 2008.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na Saed Kubenea
  Mwanahalisi.
  BARAZA la Wadhamini la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), limemtapeli Rais Jakaya Kikwete katika mradi wa mabilioni ya shilingi, MwanaHALISI limeelezwa.

  Baraza la Wadhamini, chini ya mwenyekiti wake Edward Lowassa, limeingia ubia na mfanyabiashara Shubhash Patel kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa mabilioni ya shilingi kinyume cha taratibu, na rais hakupewa taarifa sahihi.

  Mradi huo ni ule unaohusisha Jengo la Umoja wa Vijana uliopo Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam, kiwanja Na. 108/2.

  Mgogoro uliopo ni kwamba wakati Baraza Kuu la UV-CCM limekataa mradi huo unaokadiriwa kuwa wa zaidi ya Sh. 12 bilioni, Baraza la Wadhamini, chini ya Lowassa, limeruhusu mradi kuendelea.

  Tayari ujenzi wa kitegauchumi umeanza nyuma ya jego la sasa la makao makuu ya UV-CCM bila kuwepo hati maalum kuidhinisha ujenzi wa mradi.

  Kwanza, hakuna mkataba kati ya UV-CCM na mwekezaji. Pili, Baraza Kuu la Vijana limekataa mradi huo. Tatu, Baraza la Wadhamini lililopitisha mradi huo halina mamlaka ya kufanya hivyo.

  Jambo la nne, Kamati Kuu ya CCM haijajadili mradi huu na kuupitisha, na kwa vyovyote vile haiwezi kuepukwa.

  Tano, kwa mujibu wa mkataba ambao haujasainiwa, na ambao ni msingi wa Baraza Kuu la UV-CCM kuukataa, ni kwamba inapendekezwa mwekezaji amiliki kitegauchumi bila ukomo.

  Sita, na muhimu zaidi ni kwamba kauli za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba na zile za Rais Kikwete zinasigana kiasi kwamba inaonekana moja kwa moja kwamba Makamba anapinga mapendekezo ya rais ambayo kawaida huwa ni amri.

  Saba, wawekezaji wanadai wamilikishwe ardhi ili waitumie hati kukopa fedha benki, jambo ambalo inadaiwa kuwa baadhi ya viongozi wa UV-CCM wanakubaliana nalo.

  Hii ina maana kwamba “mwekezaji” hakuwa na fedha za kuwekeza isipokuwa alitaka kutumia hati kukopea fedha benki.

  Imefahamika kwamba mwekezaji tayari ametumia Sh. 6 bilioni katika mradi wa ujenzi wa majengo mawili ya ghrorofa 25 kila moja.

  Mradi mwingine unahohusiana na huo ni kukarabati jengo la sasa la UV-CCM ambamo “mwekezaji” – kwa mwaka wa pili sasa amefukuza wapangaji wote na kukosesha UV-CCM mapato yapatayo Sh. 7 milioni kila mwezi.

  MwanaHALISI limeelezwa kuwa ni vurugu hizo zilizofanya Rais Kikwete kuagiza chama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.

  Imeelezwa kuwa Kikwete alimwandikia Katibu Mkuu Makamba akimtaka kusimamia uchunguzi huo.

  Kwa upande mwingine, Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM, ilimwandikia Makamba ikimtaka kufuatilia suala hilo, lakini katika hali ambayo haijaeleweka, Makamba hakuchukua hatua.

  Kamati ya Maadili haikukata tamaa bali ilimwandikia Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mipango na Oganaizesheni, Kidawa Hamid Salehe wakati Makamba alipokuwa safari ya matibabu nchini India.

  Taarifa zinasema Kidawa hakulikawiza suala hili. Alimwandikia Rais Kikwete na ilikuwa katika hatua hii, taarifa zikaanza kuvuja ndani na nje ya chama.

  Baada ya Kikwete kupata taarifa ya Kidawa, alimwandikia Makamba akitaka wote waliohusika katika sakata hilo wahojiwe.

  MwanaHALISI lina taarifa za uhakika kwamba tayari Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Lowassa amehojiwa juu ya kuhusika kwake.

  Taarifa zinasema Lowassa amekubali kuwa baraza lake lilibariki mradi huo, lakini akasema lilishauri mkataba usisainiwe hadi Kamati Kuu (CC) ikubaliane nao.

  Hata hivyo, wakati Lowassa anasema mradi usisainiwe mpaka kupatikana kwa kibali cha CC, tayari ujenzi wa mradi huo umeshaanza, jambo linalotafsriwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni utepeli kwa Kikwete.

  “Hapa hakuna mradi. Kuna ufisadi. Mwekezaji atachukua asilimia 75 ya hisa, huku UV-CCM wakiambulia asilimia 25. Lakini kibaya zaidi, mwekezaji anaruhusiwa kuhamisha mpaka senti ya mwisho ya hisa zake,” anasema mtoa taarifa.

  Kwa mujibu wa mtoa taarifa, mwekezaji amemilikishwa kwa muda wote wa maisha yake, na kwamba anaruhusiwa kuhamishia hisa zake kwa mrithi wake kwa jinsi anavyoona inafaa.

  Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia ujenzi ukiendelea kwenye sehemu ya mradi. Alipomuuliza Kaimu Katibu Mkuu wa UV-CCM, Francis Isack, iwapo mkataba tayari umesainiwa, alithibitisha ujenzi unaendelea lakini akamtaka mwandishi aende kukutana naye ofisini kwake.

  Isack alisema mwandishi anaweza pia kumwona Katibu Mkuu Makamba kwa ufafanuzi zaidi.

  Juhudi za akumpata Makamba hazikuweza kufanikiwa. Simu yake Na. 0784 483878 ilikuwa ikijibu kuwa haipatikani.

  MwanaHALISI lilifanya juhudi pia kuwasiliana na Lowassa lakini simu yake Na. 0754 800000 iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

  Wachunguzi wa mambo wanasema mradi wa UV-CCM unaweza kuwagawa vijana na hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu katika umoja huo.

  source;http://www.halihalisi.co.tz/08/07/16/1.php
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Lowassa nenda mahakamani baba, kubenea anawaanika sana mafisadi. nenda kaombe punguzo la dozi.
   
 3. i

  issa ramadhani JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2015
  Joined: Nov 11, 2014
  Messages: 1,321
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  dah kila kitu lowassa
   
 4. rallphryder

  rallphryder JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2015
  Joined: Jan 24, 2015
  Messages: 3,137
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 180
  Hii makitu ni ya mwaka 2008 leo unaileta tena jf kwa ishu gani kama sio kutumwa huko!
   
 5. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2015
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  naona mmeishiwa hoja, ishu ya 2008, inakuja sasa? kweli naona mzee EL, anawashinda wapinzani wake.
   
 6. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2015
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 12,576
  Likes Received: 15,002
  Trophy Points: 280
  Ndio hata ESCROW ilikuwa ilianza mika hiyo lakini bomu limelipuka baada ya miaka 7 .boya wewe au wewe ni walewale

  swissme
   
 7. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2015
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  kwa hoja hii uwezo wako wa kufikiri umeshaliwa na homa ya lowasa, sasa unabaki kutegemea fuvu kufikiri, we unaona mada hii uliyoleta ni mpya? wakati tulishaisoma tangia zamani, fikiri kwa ubongo hata kama umebakiza akili chache na fupi zitakusaidia. mnatafuta mbinu za kumfaua EL, ni zilezile, ushauri jaribuni kuja na mpya lakini kila siku wimbo ni huu umechuja. wasubiri wenzenu sasa wanaojipanga na makombora yao mtakimbiana.
   
 8. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2015
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,518
  Trophy Points: 280
  hii wikendi inaboa sana,hamna nyuzi za kuchangamsha kidogo,ishmael yukwapi leo?
   
 9. n

  nakoz Member

  #9
  Feb 24, 2015
  Joined: Dec 27, 2014
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mambo ya 2008 mnaileta ya nini kama sio mmpewa hela kumchafua MTU na habari yenyewe ilikuwa ya kizushi kubenea unataka hii nchi iweje?
   
 10. Y

  Yakobi Member

  #10
  Feb 25, 2015
  Joined: Feb 24, 2015
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Doooooooooooooo
   
 11. tamimusalim

  tamimusalim JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2015
  Joined: Jun 17, 2014
  Messages: 1,829
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Safiiii
   
Loading...