Rais Kikwete asema siasa basi, sasa tuendeshe nchi kisayansi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete asema siasa basi, sasa tuendeshe nchi kisayansi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 6, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Date::9/5/2008
  Rais Kikwete asema siasa basi, sasa tuendeshe nchi kisayansi

  Rais Jakaya Kikwete, ametoa tahadhari kuwa kuendesha mambo kisiasa hakuna tija ya kutosha isipokuwa kisayansi.
  Na Peter Edson

  RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba kama nchi ikiendelea kuzalisha wanasiasa kwa wingi itaishia kwenye malumbano na migogoro isiyo na tija, badala yake amewataka Watanzania kuijenga katika misingi ya sayansi na teknolojia.

  Akizungumza kwenye mkutano wa sita wa Siku ya Wahandisi nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema njia pekee ya kuiletea nchi maandeleo ni kuzingatia sayansi na teknoliji badala ya siasa ambayo huishia kwenye porojo na malumbano.

  Alisema umefika wakati kwa kutumia wataalam hasa wanasayansi kufanisha utendaji badala ya wanasiasa katika mambo yanatakiwa watu waliobobea kwenye fani hizo.

  Rais alisema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina wahandisi 8,000 ikimanisha kuwa kila mhandisi mmoja anashughulika na Watanzania 5000, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya taifa.

  "Wasomi wanaeleza kuwa kama mtu anataka kujua maendeleo ya nchi, anaangalia idadi ya wahandisi na ubora wao, kama sisi tuna wahandisi wasiozidi 8,000 na nchi ina watu karibu milioni 39 hapo mambo yanakuwaje?’’alihoji Rais Kikwete.

  Alisema nchi ya Japan kila mhandisi mmoja anawahudumia wananchi 54, wakati hapa Tanzania mambo uwiano unaonyesha kwamba mhandisi mmoja huwahudumia watu zaidi ya 8,000.

  Kiwete alifahamisha kwamba katika kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kisayansi yanatokea nchi, serikali imeandaa mpango wa elimu ya sekondari wenye nia ya kuingiza wanafunzi kwa wingi katika masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi.

  "Tukijaza wataalamu wa siasa tutaendele kubishana tu na tukiwajaza wanasheria tutaishia kufungana, kinachotakiwa sasa ni wataalamu wa sayansi na teknolojia, ili nchi yetu iweze kusonga mbele kimaendeleo," alisisitiza Rais.

  Alisema wahandisi 500 wanaozalishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka haiwezi kukidhi mahitaji, hivyo kinachotakiwa kufanyika ni ongezeko la idadi, hadi kufikia wahitimu 1,000.

  Rais alisema pamoja na kazi nzuri ya kufundisha wahandisi inayofanywa na UDSM, bado kuna changamoto nyingi za kuboresha fani hiyo, kama vile ubora wa ufundishaji unaoweza kukidhi mahitaji ya sokoni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vyote muhimu.

  Alisema kazi ya uhandisi inahitaji kujiendeleza kimasomo, hivyo aliwataka wahandisi na makandarasi nchini kutotosheka na kiwango cha elimu walicho nacho badala yake watafute nafasi za kujiendeleza kimasomo.

  "Heshima ya uhandisi inategemea ubora wa kazi mnayofanya, acheni mambo ya ujanja ujanja," alisonya Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alitoa wito kwa bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa umoja ili kuondoa tofauti dhana iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kwamba wazawa hawawezi kufanya vizuri isipokuwa wanaotoka nje ya nchi.

  Alisema kama wahandisi na makandarasi wakifuata maadili ya kazi, shughuli nyingi zinazohusiana na fani hiyo zitafanyika kwa ubora unaotakiwa na kuipunguzia hasara taifa kutokana majengo kuporomoka.

  Wakati akiyasema hayo, hivi karibuni Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, waliunda tume kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la ghorofa 10, jijini Dar es Salaam Juni 21, mwaka huu ambayo ripoti yake haijatangazwa hadi leo

  Si hivyo tu pia kuna tume iliundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuchunguza chanzo cha kuporomoka jengo la ghorofa tatu, eneo la Chang'ombe Village na nyingine zilizoundwa kuhakiki uhalali wa majengo ya ghorofa katika eneo la Kariakoo na kwingineko nchini, ambazo hazijatolewa ripoti.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewashutumu makandarasi wenye tabia ya kuwapa kazi wahandisi ambao hawajasajiliwa na Bodi ya Wakandarasi (ERB), kuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya kuporomoka kwa majengo.

  Alisema kuna haja ya ERB kuhakikisha kuwa inawapa usajili wahandisi wote nchini, ili kuhakikisha wanafuata misingi, kanuni na sheria katika kutekeleza majukumu yao ya kihandishi.

  "Nawaagiza ninyi ERB kuhakikisha kuwa mnawasajili wahandisi wenye sifa zinazotakiwa kimataifa, ili wimbi hili la kuanguka kwa majengo liishe kabisa nchini,"alisisitiza Rais Kikwete.

  Naye Mwenyekiti wa ERB, Profesa Ninatubu Lema, alisema ili sekta hiyo iweze kukua inahitaji kuwezeshwa na kupewa fursa mbalimbali zitakazoonyesha ubora wa kazi zao tofauti na sasa ambapo kazi nyingi za uhandisi zimekuwa zikifanywa na wakandarasi kutoka nje ya nchi.

  "Ili tuweze kufanyakazi kwa ufanisi tunahitaji kuaminiwa na serikali yetu pamoja na wananchi kwa ujumla, kwa njia hii tutafanya kazi kwa uhuru," alisema Profesa Lema.

  Profesa Lema alifahamisha kuwa madoa ndani ya fani hiyo inayosababisha na watu wasio waaminifu na kuahidi kuwa wataedelea kuboresha shughuli zao ili ziwe na viwango vinavyokubalika kimataifa.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Huyu wakati anawaambia wahandisi waache ujanja ujanja yeye mwenye usanii kila kukicha.
  1.Ameshindwa hata kutaja majina ya waliorudisha pesa za EPA
  2.Ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya mafisadi mbali mbali, akiwemo
  mzee wa vijisenti, fisadi Mkapa na wengineo
  3.Ameshindwa kuchukua hatua zozote za kuhakikisha mikataba ya madini ambayo haina maslahi na
  Tanzania inapitiwa upya.
  4. Kila kukicha hubeba kikopo chake cha kuombaomba na kupita nacho US kuendelea na kazi yake ya kuombaomba
  5. Ameendelea kukumbatia watendaji mbali mbali ndani ya serikali ambao wana vyeti bandia.

  Usanii kama kazi!!!!
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Sep 6, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kikwete anatufundisha jambo ambalo wengine tumekuwa tunaliongea kila asubuhi: kwamba, kati ya sayansi na siasa, ujuzi utakaotulekea maendeleo ni wa sayansi - correct and full stop!!!

  Lakini sasa Kikwete ni mwasiasa, sasa sijui anataka tumrudishe darasani kwanza akapige shule ya sayansi? kwa vile kutokana na ukweli kuwa yeye ni mwanasiasa mtandao, na kulingana na maneno yake mwenyewe, hatatutapata maendeleo yoyote kama tutafuata uongozi wake wa kisasa. Tunataka uongozi wa kisayansi.
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Noamba nimuige Nyani Ngabu Palin McCain na YNIM na kusema Bwana Raisi, bwa ha ha ha haha
   
 5. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo sasa tuanze kulalamikia wanasayansi au unajua tena lazima kosa liwe la fulani na sio la mimi mkuu wa Nchi kushindwa kuiongoza nchi. Anaanza kujifananisha na japan sasa hivi Hahahah! Jamani mnaomuandikia raisi hizo hotuba zake huwa mnakuwa mnawaza nini? au ku-Google sanaa?
   
 6. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,593
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Kwa hili namuunga mkono Kikwete, blah blah za kisiasa haziwezi kuisaidia nchi, wataalamu wa fani za Sayansi wanahitajika sana. ni matumaini yangu kwamba raisi kwa kuling'amua hili ataweka juhudi ili hatimaye liweze kufanikiwa huko mbeleni
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Sep 6, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Wanasayansi ndio wanaoturidisha nyuma; hawatuletei mkakati wowote wa maendeleo. Sisi wanasiasa kazi yetu ni kupiga kelele tu ili kuhamasisha mawazo ya wanasayansi yasikilizwe.
  Teh !!!!!!!!!! Teh !!!!!!!!!! Teh !!!!!!!!!!
   
 8. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama wangekuwa na uhuru wa kutokuingiliwa na wanasiasa sawaa, ila Bongo kila kitu lazima wanasiasa wawepo hata kama ni cha ki-sayansi.
   
 9. RR

  RR JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Natamini huyu mwandishi aweze kutofautisha uhandisi na ukandarasi.
  Kuna tofauti kati ya bodi ya usajili wa wakandarasi (Contractors Registration Board - CRB) na bodi ya usajili wa wa wahandisi (Engineers Registration Board - ERB).
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani mmefikiria hili?.... tokeni ndani ya kabati na sayansi na Teknologia kwanza...

  1. Ni jambo la aibu kubwa Tanzania nzima kuwa na Wahandisi 8,000 tu...
  sababu ya umaskini wetu sio kuendesha nchi kisiasa isipokuwa kutokuwa na wahandisi wa kutosha, kutowekea mkazo ELIMU kama ndio chimbuko la hao wahandisi na hizo Technologia..Tuna wahandisi wachache nchini kuliko idadi ya Wanasiasa si aibu hii!..

  2. Huwezi kubadilisha mfumo wa nchi kiungozi kwa raia wako kwa sababu ya Technologia..yaani unaendesha nchi kisayansi ikiwa na maana tuko mwezini au?..Siasa ina nafasi yake, huwezi kuendesha nchi kwa teknologia isipokuwa unaihititaji Teknologia pale inapotakiwa ktk utendaji... Policy ambazo ndizo zinaongoza nchi hazitokani na teknologia hata kidogo.
  Hakuna solution ya kitoknologia inayoweza kusolve issue za Haki na hasa hawa Mafisadi ambao sasa hivi wameturudisha nyuma..Hiyo Teknologia itawazuia nini kina Mkapa, Lowassa na Rostam kuendelea Ufisadi!... au mkuu JK alikuwa akiepusha kujibu maswali (hotuba yake) ambayo yangeandamana na issue za kisiasa. kawahi kuzizima!

  Teknologia haiwezi kupima haki na Usawa wa binadamu, mdumo bora wa kiutawala, sera, ilani na kadhalika kisha kutoa hitimisho kiufundi isipokuwa Teknologia na Sayansi inakuwepo pale inapostahili baada ya siasa kufanya maamuzi. JK hakutumia Teknologia kumsafisha Lowassa ama Mkapa ila katumia siasa za kutupaka mafuta na hivyo tutaendelea kutafuta ufumbuzi kisiasa.

  3. Leo hii tunaona Kikwete akiwapeleka wanajeshi na makachero kuwa mabalozi nchi za nje hali hawa watu hawana elimu kabisa ya fani hiyo!. Tumewahi shuhudia Mawaziri wakiongoza wizara bila elimu na uzoefu wakutosha, hao kina Meghji ambao wamefikia kuitumia vibaya wizara kubwa ya FEDHA kisha Waziri mzima anaweka madai kuwa nilidanganywa!.

  Jamani, tusiwe wepesi sana kuamini vitu kama hivi maanake kama kweli Kikwete angekuwa anataka kuzungumza haya kwa nia safi ingekuwa wakati akifungua vyuo na vitengo zaidi vya Uhandisi, kuonyesha umuhimu wa sera hiyo ya kuongeza wataaalam toka kutegemea Wahandisi 8,000 kwa wananchi zaidi ya millioni 40..
   
 11. africa6666

  africa6666 JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 281
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni kweli kabisa mzee.
   
 12. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwanini JK asitume wawakilishi wanaojua cha kuongea kwenye hadhira za wasomi kuliko kuongea as if yuko kijiweni?Tunahitaji as many lawyres,doctors,journalist,etc as possible just like tunavyohitaji wanataaluma ktk teknolojia.Wanaobishana kila kukicha ni wanasiasa na si wataalam wa siasa in the sense of political analysts,researchers,scientists,etc.This presidaa cant be serious kudai tukijaza wanasheria wataishia kutufunga tu....by the way watamfunga nani kama state inalinda mafisadi kwa kutowapeleka mahakamani?
   
 13. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Heeeh, jamani. Ni huyu huyu Kikwete aliyewabeza waataalamu wa ndani kwa uzezeta wao na kwenda kuomba wengine nje?

  Sasa hapa si amesema kabisa kuwa miaka yote miwili utawala wake ulikuwa unapiga soga tu la kisiasa bila kazi yoyote ya kisanyansi?

  Haya tuwe basi na wanasayansi wazuri chini ya sera mbovu kabisa za wanasiasa wa CCM!

  Asha
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Hata ajaze wanasayansi milioni ndani ya serikali yake yeye kama kiongozi na hana utashi wa kushughulikia matatizo ambayo ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu kama ufisadi, matumizi makubwa ya serikali yasiyo na msingi, mikataba ya madini isiyo na maslahi kwa Tanzania na upindwaji wa sheria kila kukicha ili kuwakingia kifua mafisadi ambao wako karibu na 'vingunge' kamwe Tanzania hatutaona maendeleo yoyote.

  Kumbuka miradi ya IPTL na Richmond yote ilipingwa na wataalamu wana sayansi katika nyanja za umeme, lakini wanasiasa mafisadi wakailazimisha kwa nguvu na ikafanyika. Matokeo ya mikataba hiyo wote tunayajua.
   
 15. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  afrika inaelekea pabaya, wale wahandisi waliojenga kaburi la the late mwananwasa juzi kule zambia walitoka china

  tatizo letu ni kubwa kuliko anavyosema kikwete, na si katika uhandisi tu katika taaluma zote, wahandisi bila quantity surveyors, architects, surveyors hakuna lolote
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtaalamu yeyote atakayekubali kufanya kazi Tanzania kwa kulipwa ujira ambao hauendani na gharama halisi za maisha, kutokuwa na vitendea kazi na utaalamu wake kutupiliwa mbali na wasiochujua chochote kila anapotoa ushauri wake wa kitaalamu. Kama mtaalamu huyo atapata kazi ambayo watamlipa ujira mzuri, kupewa vitendea kazi na pia kuuthamini ushauri wake kamwe hatafanya kazi bongo
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Na hapo ndio maana tumerudi kwenye point A....Kuwa ni wanasiasa wametufikisha hapo na ni wao wako responsible kutuondoa hapo.

  Kwa hiyo hadi hapo serikali za hao wanasiasa zitakapotambuwa umuhimu wa wataalam hao...Tena utambuzi wa vitendo na si porojo zao za kisiasa ambazo zimetufikisha hapa tulipo.

  Pesa walizofuja...Kweli kama isingekuwa wao wanasiasa wasiokuwa na logic...Then tungekuwa mbali sana...Its time for change.
   
 18. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sayansi inakataliana na siasa kwa mbaaali. Sasa mwanasiasa akikubali kuwa sayansi ni mkombozi wakati kisiasa bado hajiwezi huo ni usani. Ufisadi tena ukifanyika kisayansi nim mbaya zaidi kwani sasa utahusu damu za watu. Au mnasemaje?
   
 19. A

  August JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  sio siasa tu na udini tuache ndio tutaendelea
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Katika kusema kwamba tuache siasa na kufuata sayansi kisanii bila kumaanisha hivyo kweli, rais anaendeleza ulaghai na siasa, wala siyo sayansi.
   
Loading...