Rais Kikwete asema amepona Saratani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,477
33,440
10502407_892063144145685_727512664383415972_n.jpg

Rais kikwete akitoa hotuba yake kwa taifa .Amesema kuwa amepona saratai ya kibofu.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.

Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..

"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya

kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.

Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."

Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.

Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.chanzo.
Rais Kikwete asema amepona Saratani - BBC Swahili
 
raisi kikwete amesema muhimbili inafanya upasuaji huo wa saratani ya kibofu lakini je yeye alifata nini marekani kama huduma zinapatikana hapahapa?????:sad:

Prostate sio kibofu (Bladder) angalia picha, hapa inafanywa prostate examination lakini utafiti mpya siku hizi unasema njia hii ya kupima haina accuracy.

Muhimbili inaweza ikawa inafanywa hiyo treatment lakini sio kwa kutumia hivo vifaa vya roboto kama Raisi alivyofanyiwa, hivi vinaongeza precission ya ule upasuaji na hivyo kupunguza chance za matatizo ya kufanya upasuaji eneo hilo nyeti ambayo ni pamoja na kukosa nguvu za kiume na kushindwa kuzia mkojo kutoka.
CDR457840-750.jpg
 
Kumbe saratani...watu si walisema busha...Tanzania kwa radio mbao nimewaaminia...
Anyway watu punguzeni kuwa cynical...hivi nani hapa apate opportunity ya kupata matibabu nje ya nchi aseme sitaki nipelekeni Mhimbili????? Tena saratani...Mhimbili...lazima ukamsalimie Israel mtoa roho...
 
nyumba kubwa,

..kwasababu ameamua kutafuta matibabu nje, basi angetumia fedha zake mwenyewe.

..sheria ielekeze kwamba matibabu bure kwa viongozi, yawe ni ndani ya nchi kwenye hospitali za serikali.

..pia kitendo cha Raisi kwenda kutibiwa Marekani kwa gharama za serikali/umma, huku hospitali hospitali za serikali zikiwa ktk crisis ya kinyimwa madawa na MSD kutokana na deni la serikali, nadhani kimeleta picha mbaya.

Janjaweed, Kiranga
 
Alikuwa na Ca prostate au BPH?
Alijuwa na uvimbe wa tezi dume au saratani ya tezi dume?
 
Kwa hiyo wewe ungekuwa rais ungeenda mhimbili???

ha ha ha...

Hata wangeweka sheria hiyo bado kama rais asingekosa ela ya kujipeleka nje...

Tusiwe tunalalamika katika kila kitu..
Mwisho tutasema rais akaishi Manzese ili nae aonje umasikini...nae akatikiwe umeme...
Hatuwezi kulingana wote kimaisha...
yeye ni rais hawezi ishi kama mimi na wewe...

Tunaweza kukosoa ukosekanaji wa huduma hospitalini bila kusema rais naye atibiwe mhimbili...
Hayo ndio malupulupu yenyewe bana...tuache hizo...Nyerere mwenyewe mjamaa lakini alifia UK...

Hapa hapa bongo penyewe mabosi mhimbili wanaenda kwa emergency ...wengi ni Regency sijui wapi...nao waambieni waende Mwananyamala

nyumba kubwa,

..kwasababu ameamua kutafuta matibabu nje, basi angetumia fedha zake mwenyewe.

..sheria ielekeze kwamba matibabu bure kwa viongozi, yawe ni ndani ya nchi kwenye hospitali za serikali.

..pia kitendo cha Raisi kwenda kutibiwa Marekani kwa gharama za serikali/umma, huku hospitali hospitali za serikali zikiwa ktk crisis ya kinyimwa madawa na MSD kutokana na deni la serikali, nadhani kimeleta picha mbaya.

Janjaweed, Kiranga
 
nyumba kubwa,

..kwasababu ameamua kutafuta matibabu nje, basi angetumia fedha zake mwenyewe.

..sheria ielekeze kwamba matibabu bure kwa viongozi, yawe ni ndani ya nchi kwenye hospitali za serikali.

..pia kitendo cha Raisi kwenda kutibiwa Marekani kwa gharama za serikali/umma, huku hospitali hospitali za serikali zikiwa ktk crisis ya kinyimwa madawa na MSD kutokana na deni la serikali, nadhani kimeleta picha mbaya.

Janjaweed, Kiranga

Kwani hakutumia pesa yake?!, kwa pesa gani tulonayo watanganyika kumpeleka Rais akatibiwe mwezini?!, halafu sasa he travels with a hundred people!, this's Ludicrous!
Mpaka unaona uchungu kuitwa mbongo!
He's freaking Filthy Rich!, why spend walalahoi money?!!!!!!
Ama some of matibabu money came from the Escrow A/C
 
Mkuu, ukiwa na uvimbe si ndo saratani yenyewe hiyo?!

Uvimbe si sawa sawa na saratani.uvimbe waweza kuwa saratani au uvimbe usio saratani.kuna terminologies mbili muhimu unapoongelea 'uvimbe'

Kuna benign tumor na malignant tumor.

BPH ni benign prostatic hypetrophy ni tofauti na CA Prostate.
 
  • Thanks
Reactions: kui
vipi ameandaa mazingira kwa ajili ya hao wananchi kupata huduma hapa nchini au watasafirishwa mpaka marekani kwa ajili ya hizo checkup na matibabu,
zero brain

Same thoughts here....well, good for him!, sasa amekuwa buheri wa afya afanye kazi kwa bidii kusaidia wananchi wake wasoweza kuvuka mipaka kwa ajili ya matibabu.
I hope SASA, ataelewa kuwa kuumwa nchini kwake ni kama kuwa ktk Mahakama ya kifo!
 
Uvimbe si sawa sawa na saratani.uvimbe waweza kuwa saratani au uvimbe usio saratani.kuna terminologies mbili muhimu unapoongelea 'uvimbe'

Kuna benign tumor na malignant tumor.

BPH ni benign prostatic hypetrophy ni tofauti na CA Prostate.

......kuumbe!
 
Jamani tujaribu kuwa realistic...siwezi endelea ku argue...
Maana naona tunaacha kuwa objective na kutumia emotions zaidi...
Rais ku behave kama yule wa Latin America anayetumia bito ni uamuzi...
Otherwise yuko entitled kutibiwa nchi yoyote...
Unless mkumbuke kuandika kwenye katiba mpya kuwa hilo ni marufuku...

Mwisho mtasema na holiday aende Arusha...kha...

Hakuna uhusiano kati ya rais anatibiwa wapi na utendaji wake wa kazi...
Tunachanganya habari hapa...

Kama hata Chavez kipenzi cha wananchi wake alitibiwa Cuba iwe Kikwete???? Nani anataka kufa huku anajua kuna option...
 
Back
Top Bottom