Rais Kikwete apewe tuzo ya rais bora katika ukanda wa maziwa makuu

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
28
Hakuna asiyeona kazi nzuri na utumishi uliotukuka wa rais wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete. Kwa muda aliokaa madarakani ameleta maendeleo makubwa katika nchi yetu.

Elimu, afya, kilimo na ujenzi wa miundombinu ni baadhi ya maendeleo katika kipindi cha uongozi wake.

Kuna haja ya Watanzania kuandaa hafla kubwa ya kumpongeza na kumpa tuzo ya kuwa rais bora kanda ya maziwa makuu kwani mchango wake unatambulika mpaka nje ya mipaka yetu katika kusimamia ustawi wa nchi nyingine za maziwa makuu.Kama katiba inaruhusu JK anasifa ya kuendelea kuliongoza Taifa la Tanzania.
 
Kwa sababu anaruhusu umafia wa kukandamiza wananchi wa nchi za pembe ya Afrika sijui yeye kama watanzania watamkubalia na ubwanyenye anaoendekeza nchi za watu
 
Sio rais bora apewe bora rais kwa sababu ana PHD (Pure Head Damage)
 
Mzimu wa Escrow utamfuata hadi kaburini, subirini muone. Mmeshiba maharage ya ikulu, karibu hata mtamwabudu. Poleni.
 
Ningeona ubora wake iwapo angewatafutia ajira vijana wa Lumumba kwenye mabenki ili kupunguza jam humu JF maana kule watu wapo busy hakuna muda wa kuja jf kutema pumbapumba ..7,000 x 28days = 196,000/= wangelipwa hata 250,000 kwa mwezi wawe serious kidogo
 
Ni kweli ni Rais peke yake ambaye
1) Amebadili baraza la mawaziri mara 3
2) Amejenga barabara za lami fupi kuliko mtangulizi wake Rais Mkapa-Rejea hotuba ya Magufuli
3) Haki za Binadamu zimefinywa sana kipindi chake. Rejea Mwangosi, Said Kubenea, Ulimboka
4) Alikuta serikali ina pesa anaiacha mufisili. Juzi msajili wa Bodi ya makandarasi alisema kuna baadhi ya wakandarasi wamejiua kwa kutolipwa.
5) Tulihaidiwa katiba mpya na sasa mwelekeo ni kwamba hakuna kitu!
Ni kweli kafanya mengi ambayo wengine tunaona kama ni bure.
 
Hakuna asiyeona kazi nzuri na utumishi uliotukuka wa rais wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete. Kwa muda aliokaa madarakani ameleta maendeleo makubwa katika nchi yetu.

Elimu, afya, kilimo na ujenzi wa miundombinu ni baadhi ya maendeleo katika kipindi cha uongozi wake.

Kuna haja ya Watanzania kuandaa hafla kubwa ya kumpongeza na kumpa tuzo ya kuwa rais bora kanda ya maziwa makuu kwani mchango wake unatambulika mpaka nje ya mipaka yetu katika kusimamia ustawi wa nchi nyingine za maziwa makuu.Kama katiba inaruhusu JK anasifa ya kuendelea kuliongoza Taifa la Tanzania.

mpuuzi wewe
 
Yaani watanzania tuwaamulie wengine ukanda wa Afrika Mashariki kwamba Kikwete ndio kiongozi bora? Kwa nini asiwe Mwai Kibaki kwa mfano?

Kumbuka kuna tuzo ya Mo Ibrahim. Ndiyo mbivu na mbichi zitajulikana. Mwaka huu kachukua Pohamba wa Namibia. Kule hakuna ESCROW, EPA wala RICHMOND.
 
Back
Top Bottom