Rais Kikwete aota kujenga safu ya vijana katika uongozi wa kitaifa

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwa kama akijaliwa kupata kipindi cha pili cha kuliongoza taifa la Tanzania, atafanya jitihada kubwa kuubadilisha uongozi wa Tanzania kuwa uongozi wa vijana.

Rais Kikwete akizungumza juzi, mjini Dar es Salaam na vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika wanaoshiriki katika Mpango wa Kulea Uongozi wa Afrika wa African Leadership Initiative, Rais Kikwete alisema kuwa anauthamini Mpango huo.

Alisema kuwa vijana ndiyo Tanzania ya kesho, na kama Tanzania haikuwekeza vya kutosha katika vijana na maendeleo yao, basi itakuwa haiwekezi katika hali yake ya baadaye.

Aliwaambia vijana hao ambao wanashiriki katika Mpango huo unaodhaminiwa na Askofu Mkuu (mstaafu) wa Kanisa la Anglikan Desmond Tutu wa Afrika Kusini kuwa kwa kadri miaka inavyokwenda ni lazima rika la wazee lipishe lile la vijana.

Rais aliwaambia vijana hao kwenye mkutano wao katika Hoteli ya Southern Sun mjini Dar es Salaam: "Kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, kama nitajaliwa na nikapata bahati ya kuchaguliwa tena, nitahakikisha kuwa naubadilisha uongozi wa Tanzania kwa kuufanya uongozi wa vijana zaidi."

Aliongeza: "Wale viongozi wa rika langu lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi, na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.

Amesisitiza: "Vijana ndiyo matumaini ya nchi hii katika miaka inayokuja, na kama hatukuwekeza katika vijana wetu, basi ni dhahiri kuwa hatuwekezi ipasavyo katika miaka ijayo ya taifa letu."

Akijibu maswali ya vijana hao kutoka nchi mbali mbali za Afrika zikiwamo Tanzania, Nigeria, Kenya, Afrika Kusini na Uganda, Rais Kikwete amewaeleza vijana hao jinsi gani alivyojikuta anaingia katika siasa.

Akijibu swali kuhusu maendeleo ya karibuni katika siasa za Zanzibar, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba vyama vya siasa katika Zanzibar vimeamua kuachana na siasa na mazoezi ya zamani na kuanza ukurasa mpya.

"Nawatakia heri sana katika mwelekeo mpya na sahihi kabisa katika uendeshaji wa siasa. Ni mwelekeo ambao sote tumekuwa tunautafuta kwa muda mrefu." Katika siku za karibuni, Chama cha CUF ambacho ni chama cha upinzani kimeamua kumtabua Rais Amani Abeid Karume kama Rais wa halali wa Zanzibar, hatua ambayo imefungua kila aina ya uwezekano wa kupatikana maelewano na mwafaka katika Tanzania Visiwani.

Source: Mwananchi
 
Bado kalala kwenye 'vijana ndiyo taifa la kesho" wakati watu hawana kazi leo!
 
Du hivi huyu jamaa bado anataka kuendelea beyond 2010?????? Du kweli kazi tunayo na vijana wenyewe ni kina nani? Msauni? Jerry Slaa? Ridhwani? Maina? au Nchimbi?

Kama vetting ya wazee ambao amekuwa nao siku zote serikalini imemshinda wht about the so called vijana??????
 
Halafu kwa mantiki hii ni vijana wa aina gani atakaotuandalia? Akina Masha,Ngeleja, na Ridhwani? Kama wewe mwenyewe uongozi wako ni mbovu si utatuachia vijana wabovu tu katika taifa hili? Tanzania deserves better!
 
Kuchagua vijana ni safi, kwa sababu wengi watahofia ajira zao, hasa ikiwa ni vijana waelewa!
Cha muhimu ni kuachana na wapiga debe, kama akina Masha na Nchimbi!!
Yaani sifa ya kupayukapayuka aiweke pembeni!!
 
Back
Top Bottom