Rais Kikwete aongea na Wazee wa Dar: Adai pesa za Escrow ni za IPTL. Uteuzi wa Tibaijuka watenguliwa

Amekwisha sema siyo Fedha za Umma ni mali ya IPTL..Tukutane 2015 tutaheshimiane watanzania wameona, wamesikia, wamejua sasa Wataamua

Amesema ki-kwao tunazoza..... Tutazoza vizuri 2015.... Kama anafikiria wote tulibeba LUMBESA, kura yangu ni zaidi ya LUMBUSA
 
Hao wazee wa mkoa wa Dsm hawaelewi kitu wanangaaa sharubu wala hawapigi makofi...daah Nam miss sana Mzee Mkapa na Uongozi wake daah
Kama wazee wa Mkoa wa Dar unawaona hawaelewi kitu, je wazee wa mkoani kwako?
 
Ndugu wana jf mmeamini nilichosema mwanzo kabisa? Kuwa hapa hakuna maamuzi magumu zaidi ya kutetea walio CCM (Chukua Chao Mapema)
 
Sasa kwa nini Mwanasheria Mkuu wa serikali aliamua kuachia ngazi?

Kumbe alitoa ushauri mzuri tuu? Why resign then?

Hakujiuzulu alishastaafu rasmi baada ya kufikia miaka 60 Tarehe 16 decemba 2014 aliyekwambia kajiuzulu kamwuulize kustaafu ndio kujiuzulu?
 
kahotuba kenyewe ndo haka, ngoja niendelee kujipigilia viroba nchi ishapigwa hela siku nyingi
 
Amekubali kuwa Tanesco ilishinda ICSID. Kwa nini Tanesco waliacha maamuzi ya ICSID ambayo yaliwapo ushindi 2001? Badala yake wakaenda kufungua ESCROW mwaka 2007? Hapa ndo rais amekosa flow na corelation ya anachokiongea.
na kwa nini tanesco wafungue account ya Escrow bila kupeleka kesi mahakamani? Hapa tatizo ni nini wakati kwa kufanya hivo Tanesco lazima walipe riba ya 2% ambayo ni hasara ya zaidi ya 30m$... kwa nini watu wa tanesco wasichukuliwe hatua....
 
Hivi wazungu wametunyima misaada kwa bahati mbaya hawakuchunguza kwa umakini ufisadi huu?je hawa wabunge wote hawana uwezo wakufikiri kama yeye anavyotuaminisha?kwamba alichoambiwa yeye ndio sahihi?
 
Anawakanusha PCCB kwa kudai pesa zilichukuliwa kwe visandarusi. Nategemea Hosea kutemeshwa kazi kwa kulidanfanya Bunge na kusababisha mgogoro baina ya Bunge na Serikali.

Vv
 
Kwa Tafsiri nyingine Jakaya kikwete anatuambia ni kuwa huu mchakato ulikuwa halali, fedha ni za iptl na hakuna cha kuchunguza wala maazimio ya bunge hakuna litakalotekelezwa.
 
Chezea Kikwete..huyu ndo Kungwi wa siasa za bongo, anajua kuzipika na kuzipakuaa....
Hapa Kina Zitto wanasutwajee sasa...Wezi wanasafishwa kwa nguvu...

Nchi ngumu sana hii...
 
Back
Top Bottom