Rais Kikwete anamhujumu waziri Magufuli?

Ngoja nianze kulipuliza hilo kwenye profile picture yako bila shaka lilikupa hii akili

Ukilipuliza litazima, livute moshi mweupe utoke.
Ha hahahaha, duh miaka imekwenda kasi na leo jamaa anafukuzana na makontena na kuaibisha anaowategemea kumfanyia kazi. Tutafika na safari inaendelea:lock1:
 
Mkuu Obe heshima yako mkuu,wewe ni nabii wa kweli na Maneno daima huumba from there naanza kuamini Magufuli ni mpango wa Mungu na ntaenda kueneza neno hili kwa mataifa yote.
 
Magufuri anatisha na anaogopesha na kama itatokea akashika nchi mambo ya longolongo yatapotea

Magufuli ni mchapakazi, kichwani anapeta ile mbaya!! Sasa kwa hili kwa nini hao wanaopiga bla bla wasimchukie na kutaka kumwangusha!!!! Hon. Magufuli usikate tamaa, tulikuheshimu tangu ulipokuwa hasa Wizara ya ardhi, na ulipotoka tu, kumerudi kama zamani, rushwa kuanzia reception!!! Hupati file pale bila kutoa kitu kidogo.Viwanja ndiyo hivyo, tena. Maneo ya wazi yameisha kuuziwa wakubwa, hata wengine kule Mbezi Beach wanataka kufunga street road kwa kuwa eti kuna michoro mipya imetolewa!! Hivi michoro hiyo inafuta street roads?? Magufuli Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Jitose urais 2015 utapata!!! Nitapiga kura kwa mara ya kwanza tena tokea mwisho wa uchaguzi wa Baba yangu wa Taifa aliyehakikisha nimesoma na kutibiwa bure mpaka nikawa health mentally and physically capable. R.I.P!

Watu waliona mbali???
 
Lisemwalo lipo manake huyu mkulu Magufuli ni tishio sana kwa watendaji wababaishaji.Nyota yake inang'ara kwa merits na siyo ujanja ujanja wa kuwanunua wanahabari na kuwahadaa wananchi.
Siyo siri huyu mkuu siku anaukwaa Urais,basi within 5years tu tungeona mabadiliko makubwa sana Tanzania.Bahati mbaya watu kama Magufuli katika siasa zetu hawana nafasi.Ndiyo maana sometimes nakereka sana manake watendaji wazuri tunao lakini wanapigwa vita kwa maslahi binafsi.
Mkapa leo kesho haachi kumsifia na kumshukuru Magufuli kama waziri aliyeiletea sifa kubwa serikali yake.
Go Magufuli go,as long as umma upo upande wako basi ile siku ya vikwazo wako kuumbuka iko njiani inakuja.
JF inajua kutunza kumbukumbu
 
JK nimegundua ni mfuasi mkubwa wa 48 laws of power alizoandika Robert Greene.Na hasa law namba7,ya let people work for you,take credit always

Pia Magufuli ni mchapakazi sana.Nadhani pia ukaribu wake na Urafiki8 wake mkubwa na Raila Amolo Odinga wa kenya umechangia mfanano wao wa kiutendaji

Nakumbuka ile kashfa ya kumuuzia nyumba kimada,sijui ni kweli au ilitengenezwa na mtandao ktk harakati zao?

Huyu akiwa Rais Tanzania basi tutakua tumepiga hatua maanake ana kaudikteta flani hivi ambako watanzania wanakahitaji ili wafanye kazi
Ushampata sasa
 
Jamani hii nimeipata kwenye chanzo kimoja cha uhakika mno; kwamba wale samaki wa magufuli walikuwa wanakwama kuuzika kutokana na hujuma za Raisi wa Tanzania JM Kikwete dhidi ya Dk Magufuli.
Chanzo hicho kimesema kwanza alijaribu kufunika na kudakia kazi ile ya kukamata jodari ili ionekane ni yeye aliyefanya lakini ikashindikana kwani watu waliendelea kumpongeza Magufuli tu.
Ndipo alipokuja na mbinu mpya lengo likiwa ni kumpunguzia umaarufu Magufuli ili aonekane alifanya zoezi la kamatakamata samaki Jodari kwa kukurupuka na zoezi zima limeiletea hasara nchi..kama kwaida yake Kikwete alitumia vyombo vya habari na "UWT". Lakini kwa bahati mbaya kwake Raisi, Magufuli alifanikiwa kujua mapema hila hizo na akazisambaratisha kwa hoja zenye busara mno, kama vile Serikali inapofanya kazi yake kwa kufuata sheria hakuna hasara, akatoa mfano wa "mwizi wa vitumbua anavyohudumiwa na serikali kwa gharama kubwa kuliko alichoiba"
Inasemekana hujuma za Kikwete na wanamtandao kwa ujumla dhidi ya Magufuli hazikuanza hivi karibuni, hofu yao kubwa ni kukubalika kwa Magufuli miomngoni mwa watanzania kuona ni hatari kwa mbinu zao(wanamtandao) za kurithishana Uraisi wa TZ.

Alionekana kutoka mbaaali sana
 
"JK nimegundua ni mfuasi mkubwa wa 48 laws of power alizoandika Robert Greene.Na hasa law namba7,ya let people work for you,take credit always

Pia Magufuli ni mchapakazi sana.Nadhani pia ukaribu wake na Urafiki8 wake mkubwa na Raila Amolo Odinga wa kenya umechangia mfanano wao wa kiutendaji

Nakumbuka ile kashfa ya kumuuzia nyumba kimada,sijui ni kweli au ilitengenezwa na mtandao ktk harakati zao?

Huyu akiwa Rais Tanzania basi tutakua tumepiga hatua maanake ana kaudikteta flani hivi ambako watanzania wanakahitaji ili wafanye kazi"

Back
Top Bottom