Rais Kikwete anahusika Richmond?Mungu azidi kutubariki, atufunulie akili zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete anahusika Richmond?Mungu azidi kutubariki, atufunulie akili zetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,603
  Likes Received: 5,780
  Trophy Points: 280
  Rais Kikwete anahusika Richmond?
  [​IMG]


  PDIDY

  [​IMG]
  KWA wanafalsafa, nilishasema hakuna neno la bahati mbaya. Kila neno hutolewa kwa kukusudia jambo fulani, huwezi kutamka kitu fulani ukasema kuwa ni bahati mbaya, mfano umetukana mtu, ukiulizwa unasema ni bahati mbaya, mbona hakuna bahati mbaya katika kutukana mawe? Au miti? Kwanini ukaja kwa huyu na ukasema hivi wakati huu?
  Katika moja ya mambo yanayoonekana kukosa majibu mwaka huu, ni sakata zima la Kampuni ya Kimareani ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond. Kampuni hii inaonekana kuwaumiza vichwa watawala wetu kwa kukosa majibu ya msingi.
  Watanzania wengi wameumiza vichwa kufikiri sana na kila kukicha wanalalamika, suala la Richmond limekuwa moja ya mambo mazito sana nchini kujadiliwa. Limejadiliwa likaonekana kuwa halina rushwa, hii ni kutokana na ripoti ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah, baadaye iliundwa Kamati ya Bunge kuchunguza sakata hili na kukaonekana kuwa kuna ufisadi mkubwa usiomithilika, tena uliofanywa na viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Baada ya kamati kufanya kazi yake, kulitolewa mapendekezo mbalimbali ambayo serikali ilipaswa kuyafanyia kazi, mojawapo ilikuwa ni kuwawajibisha wote waliohusika na kashfa hiyo.
  Taarifa nyepesi isiyokidhi hata kuwajibu watoto wadogo, ilitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuwahadaa Watanzania. Akasema kuwa wahusika wamepewa onyo na kuwahakikishia Watanzania kuwa hakukuwa na dalili zozote za rushwa katika sakata hili na Rais Jakaya Kikwete hahusiki na Richmond.
  Luhanjo anasema: “Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maneno na vijembe ati kuwa kuna mkono wa Rais Jakaya Kikwete katika kutoa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopata Kampuni ya Richmond. Kiini cha maneno hayo ni kauli za baadhi ya wanasiasa zilizopazwa sauti na baadhi ya vyombo vya habari.
  “Tunapenda kusema, tena kwa msisitizo kuwa, maneno hayo si ya kweli na hayana msingi wowote. Rais hajahusika na uamuzi wa tenda hiyo kupewa kampuni ya Richmond.”
  Kauli hiyo ilipokelewa na Watanzania, lakini kama ambavyo nimekwishasema huko nyuma, kauli za viongozi wetu kwa sasa kila zinapotolewa tuzipokee kwa umakini mkubwa kama ambavyo kauli nyingi zinazopingana ambazo amekuwa akizitoa rais mwenyewe wala si kupitia kwa watendaji wake.
  Ni kutokana na kashfa ya Richmond, IPTL, taifa letu limekuwa likipata mgawo wa umeme kwa sababu tu Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) limekuwa likizilipa kampuni hizo pesa nyingi kiasi cha kushindwa hata siku moja kujitegemea.
  Baada ya sakata la Richmond kuhamia bungeni na pia suala la ununuzi mitambo ya Dowans ambayo ni kampuni ambayo iliuziwa tenda ya kuzalisha umeme na Richmond, kumetokea mambo kadhaa yanayotufanya tujiulize kuwa, rais wetu anahusika na Richmond?
  Kwanza ilitolewa tahadhari kuwa mitambo ile isingenunuliwa taifa lingeingia gizani, hivyo ili kukwepa giza afadhali mitambo ya kifisadi inunuliwe. Hiyo ilikuwa hoja ya Dk. Idris Rashidi.
  Hatujui mtendaji huyu wa serikali aliwasiliana vipi na mkuu wake wa nchi au alimshauri vipi, mpaka akawa na ujasiri wa kupendekeza mitambo hiyo haramu inunuliwe hata kama katika kuinunua tulikuwa tunapingana na sheria ya nchi kuhusu manunuzi ya umma.
  Nchi yetu kweli imeingia gizani, chanzo cha tatizo kinafahamika, mkuu wa nchi akatoa “amri” kuwa sasa mitambo ya IPTL iwashwe.
  Sentensi kama hiyo ilionekana kuwa ni nafuu ya Watanzania, kuwa wataepushwa na giza hili. Wizara husika zikaamriwa huenda kwa amri ile ile kama iliyotumika wakati wa kuingiza Richmond, na mawaziri husika wakaingia mkenge kudanganya Watanzania.
  Oktoba 21, 2009 Rais Kikwete alitoa agizo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe. Oktoba 25, 2009 tayari meli yenye shehena ya mafuta iliwasili Dar es Salaam kwa ajili ya kutumika kwenye mitambo ya IPTL. Tufikiri kwa makini na kwa kina bila woga, tena kwa ujasiri wa uzalendo, kweli hakuna mkono wa rais katika giza linaloendelea nchini, au katika hili suala la kukatika umeme?
  Tafakari kuwa Rais Kikwete alitoa tangazo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe, Oktoba 21, 2009, kisha tukaambiwa na kina William Ngeleja kuwa serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL Arabuni. Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo na yamefika bandari ya Dar es Salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe. Tena meli zingine inabidi zisogezwe haraka ili kupisha upakuaji wa shehena ya mafuta ya IPTL.
  Tujiulize tena, meli toka Arabuni huchukua siku ngapi? Au mafuta yaliagizwa kabla ya Ikulu kuzungumza? Na ilikuwaje mafuta yakaagizwa kabla ya Ikulu kutoa tamko? Ikulu ilipataje kujua kuwa giza litaingia na nchi itatumia mitambo ya IPTL?
  Ni wachache sana watakaokubali kuwa giza hili limepangwa, tena kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa kisiasa ambao hauna uzalendo hata kidogo, bali ni udhaifu mbaya sana wa uongozi, unaoashiria rushwa mpaka uongozi wa juu wa nchi.
  Meli hii ilikimbia kiasi cha kuvunja rekodi ya safari za meli toka Arabuni kuja Tanzania chini ya muda wa siku sita tu! Imewezekanaje? Kama kweli mafuta yalishaagizwa toka Arabuni kabla, kwanini yaliagizwa? Nani aliagiza? Alikuwa anatekeleza agizo lipi? Alijuaje amri ya rais kabla haijatamkwa? Alijuaje kuwa IPTL wangekubali kuwasha mitambo? Alijuaje kuwa IPTL hawana mafuta ya kuwasha mitambo?
  Kufuatia ushahidi huu, nimeweza kuona kuwa majibu ya maswali yafuatayo yanaweza kusababisha rais wetu kuhusishwa na kashfa ya giza la nchi yetu.
  Je, rais alipanga na wahusika wa TANESCO ili giza liwepo aweze kutoa tamko?
  Pili, aliwasiliana na watu wa IPTL kwa ajili ya ‘biashara’ ya kuleta mafuta kwa spidi kubwa ya ajabu hususani kwa meli kubwa ambazo zimewahi kusafiri toka Mashariki ya Kati hadi Afrika Mashariki?
  Kama hayo mawili si ya msingi, tunaomba kujulishwa mafuta hayo yaliagizwa na nani? Lini? Kwa njia gani ya haraka iliyosababisha yakafika hata muda wa wiki haujafika?
  Lakini yakiendelea madudu hayo yote, tujue kuwa ni rais wetu aliyewahi kusema kuwa nchi yetu kwa sasa mgawo wa umeme utakuwa historia, baada ya kutoka Marekeni na kuongea na wawekezaji wa Richmond.
  Tunaogopa nini kumuwajibisha Rais Kikwete na serikali yake kwa kushindwa kuwaletea wananchi umeme wa uhakika, badala yake wamekuwa wakitufanyia biashara sisi masikini? Si Rais Kikwete ndiye aliyewaahidi Watanzania kuwa sasa mgawo wa umeme utakuwa historia nchini baada ya kuwapo kwa kampuni za kuzalisha umeme wa dharura kupitia kampuni hii ya Richmond?
  Tamko nyonge la Ikulu lililotolewa na Luhanjo liliwahi kusema kuwa: “Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya USD 10 million na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane. Rais alikataa maombi yaliyopelekwa kwake na Wizara ya Nishati na Madini ya kumuomba aagize Wizara ya Fedha, iilipe kampuni hiyo fedha hizo.
  “Rais aliagiza Wizara ya Fedha ibaki na msimamo wake na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wafanye mambo mawili. Kwanza, wafanye utafiti zaidi kujua undani wa Kampuni ya Richmond, isije kuwa ni kampuni bandia wakapewa fedha wakatokomea nazo na mitambo isipatikane na hukuna namna ya kuipata kampuni wala wahusika wake.
  “Pili aliagiza wawatake viongozi wa Kampuni ya Richmond kwanza walete mitambo, ikishafika, ndipo walipwe. Maagizo hayo ya rais yalizingatiwa na Kampuni ya Richmond ikapewa sharti hilo. Lakini, ikashindwa kulitekeleza na kuishia kuingia mkataba na Kampuni ya Dowans iliyokuja kuleta hiyo mitambo badala yake.”
  Hivi baada ya hapo Rais Kikwete alimchukulia nani hatua kwa kuona kuwa aliyoagiza hayakutekelezwa? Baada ya kujua kuwa Richmond haikuweza kazi na kabla haijaingia mkataba na Dowans, yeye kama Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri alipokeaje hilo, huku akijua kuwa Richmond imelipwa pesa huku ikiwa haijafanya kazi? Kwanini alikaa kimya muda wote mpaka sasa? Kama hahusiki awawajibishe waliohusika. Mungu azidi kutubariki, atufunulie akili zetu tuweze kujua tunayofanyiwa.


  [​IMG]


   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hii habari ni nzito sana, wahusika msg kama hizi zinawafikiaga kweli??????????
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwanza aliwasiliana au kushauliana na idrisa rashid jinsi wanavyoweza kupenyeza hii deal.
  Pili wakawasiliana na iptl kuona uwezekano wa kutumia mitambo yao, baada ya kukubaliana wakapewa masharti ikiwa ni pamoja na kuwaagizia mafuta, wakaagiza hayo mafuta
  Tatu baada ya kila kitu kukamilika umeme ukaanza kuleta shida
  Nne ndipo rais alipo jitokeza na kutoa tamko,
  Kilichofata ni mawazili wake wasio na akili hata kidogo wakaanza kutoa habari ambazo ndo kimekuwa chanzo kuumbuka
   
 4. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Habari ni hizohizo....watu walewale..in short hamna jipya.ashiriki asishiriki poteleambali maana hamna chochote kitakaco endelea wala kupelekwa mahakamani.
  haohao watapigiwa kura na watanzania wengi, ukidhania labda wapinzani nao wataamka, ndo kwanza wanaanza kutimuana, mwisho wasiku mtu unaamua kujenga familia yako, life goes on.
   
 5. s

  siyajui Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 4, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  we need to make something happen next year! Let us make it happen by bringing major change in Tanzania like in Kenya. We are fed up with corrupt leaders in Tanzania. Together we can!
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,603
  Likes Received: 5,780
  Trophy Points: 280
  oooohhh yeah its true lets make some changes
   
 7. j

  jonbalele Member

  #7
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mungu ibariki tanzania
   
 8. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  with the current opposition, it is a day dream to make that change!! It is a bitter pill for you but JK will continue to be the president until 2015.
   
 9. Jerome

  Jerome Senior Member

  #9
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du! Kasheshe wadanganyika tutaliwa mpaka lini? Tuombe Mungu mabadiliko yetu yawe ya amani siyo kama kenya ,rwanda na burundi
   
 10. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Unajua kuna kitu wazungu huwa wanapenda sana kukitumia hasa kwa maslahi ya taifa ... kufanya mammbo OFFBOOK" yaani kuna wakati mnatakiwa mpindishe sheria huku serikali ikihakikisha ina cover mianya yoyote yakuonekana kama sheria imepindishwa ili mradi taifa lisiingie pabaya na hiyo ndio patriotism.. sasa Mtu unajiuliza katika maswala haya nyeti haaingii akilini Raisi mwenye dhamana ya nchi.. eti anawapa watu siku 30 warudishe hizo pesa.. tena akiwaahidi kuwa hatawataja na hawatashtakiwa.. kama hiyo haitoshi zilipokwisha hizo siku akaongeza nyingine...na baada ya hapo akawasamehe... then kwa kuona hataeleweka wakaanza kutafuta njia mbadala wa nani wa kumtoa kafara...

  WEWE KAMA HAUHUSIKI INAKUWAJE USHIKWE NA KIGUGUMIZI CHA KUWAWAJIBISHA HAO. anaweza akawa hausiki kwa richmond ila anajua ana madhambi yake ambayo anajua akiwatibulia wenzie na wao watamfunulia ya kwake... ndio maana anabaki kijichekesha na kuongea sana..pasipo maana.. matokeo yake wenzie wanamfanya mjinga kwa kumuingiz a kwenye mtego wa kutoa ahadi zisizotekelezeka.. na kubaki akaonekana mpiga domo....
  rais wenu hana maana....
  HII NDIO TZ ZAIDI YA UIJUAVYO
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa mkuu. Tanzania pia kuna kundi la watu wanao-operate ki-MAFIA. Kundi hili lina watu kama Rostam ambao wamejilimbikizia utajiri kwa njia haramu kiasi cha kuweza hata kuamua nani ashike madaraka gani serikalini (ikiwemo URAIS) na sehemu nyingine. Hii ni hatari sana! Watu wa aina hii wakishajichimbia kwenye nchi serikali inaacha kuangalia maslahi ya wananchi wake na kujikita zaidi kwa hawa MAFIA. Hapa nchini sasa hivi wanajulikana kama mafisadi lakini ndio hao hao MAFIA... Lazima tuchukue tahadhari.
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  dua la kuku halimpati mwewe......mimi kikwete niacheni nitese na hapa nilicheleweshwa tu na yule mwasisi vinginevyo mngekuwa mmefikia hatua ya kusaga meno kwa hiyo nawaambieni bado na acheni nifaidi kile nilicho kipigania kwa muda mrefu halafu nikakipata.....ccm yangu na sera yetu ni chukua chako mapema,,,,,,,,,nyie mara kibao nimewaambia kuhusu uswahiba wangu na akina lowasa,rostam nk sasa nyie mnafikiri hawa wanaweza kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu kiasi hiki alafu mimi nisijue? na baada ya kubainika si ningalikuwa nimesha wachukulia hatua kali? nawaambia mnapoteza muda wenu na hayo maisha bora kwa kila mtanzania sikumaanisha ndani ya miaka kumi ya utawala wangu nilimaanisha kutakuwepo na maisha bora kwa kila mtanzania huko mbeleni hivyo subirini huu ni wakati wetu sisi wanamtandao kufaidi matunda haya kidogo ya nchi yetu hivi nyie watz mnaakili kweli lazima muangalie na aina ya ahadi maana kuna ahadi zingine ni mungu tu ndiyo anaweza kuzitoa mfano hii ya maisha bora kwa kila mtanzania ni kitu ambacho hakiwezekani jamani kumbe nimegundua ''mnadanganyika kirahisi''.....kuna baadhi wanaccm wenzetu wanatuonea gele sana tunawatahadharisha watuache na wao wasubiri zamu yao....hivi jamani kwa nini msikae kimya kipindi hiki tufanye tunavyo taka na nyie mkija tuwaone.......tunasemwa sana....tunaonewa sana.....tunatukanwa sana....tunanyanyaswa sana....hii yote eti kwa sababu mimi ndiyo rais wa nchi,wivu tu unawasumbua.ngoja niagize wadogo zangu waandae fulana na kofia zenye nembo ya ccm kwa wingi wa ajabu kwa ajili ya ''COME PAIN'' za mwakani.nikimaliza muda wangu mniache nipuimzike kama nilivyoagiza aachwe mkapa apumzike.......mimacho tu!!!!!!!!
   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  so more sufferings to come? are we ready to wait for it?.......where is the active new generation to help here?
  things are so worse....why jk again? because of his smile? his face? his leadership ability? what is behind? why are we so blind to this extent?
  aren't we fade up? what are we waiting for?
  my God....................!!!!!!!!????????????????this is enough jamani.

   
 15. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nimekupata mkuu; yaani inawezekana:
  Kwenye mafuta hayo kuna deal ya watu maana haiwezekani kuagiza mafuta yakafika kabla ya hata wiki moja. Kumbuka kuna utaratibu wa kupata meli (inawezekana ilikuwepo meli tupu tayari) kuna kujaza mafuta (inawezekana kulikuwa na meli imepakia mafuta hayo tayari) kuna muda wa kusafiri (inawezekana hii ni meli maalum). Concidencies zote hizo haziwezi kutokea, lazima kulikuwapo na mpango kabla.

  Kuhusu IPTL: Watu mnasahau kuwa kampuni hii kuingia nchini JK kuna mkono wake kabla hajawa rais? Wadanganyika acheni kudanganywa - amkeni!
   
 16. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa hilo kundi la MAFIA lipo na kazi zake ni dhahiri. Pia linajulikana kama FREEMASON, ILLUMINATE, BABILONIAN nk. Wanyonge kuepoka maangamizi ya kundi hili ni kwa neema ya Mungu tu sii vinginevyo!!
   
 17. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Habari hii kwa nchi na uongozi unaojali waajiri wao (wananchi) isingeishia kwenye gazeti au kwenye forum kama hapa JF. Tatizo ni kwamba viongozi wetu wanajua kwamba wananchi hatuna meno wala hatuzijui haki zetu, ingawa tunaoujasiri na nafasi ya kusema maovu tunayoyaona.

  Kuhusu kwamba kikwete ataendelea kupeta mpaka 2015 hii hatuna option nayo, na hii inaumiza suala ni je sisi kama wana jamii hivi tufanye nini ili kujinusuru na majanga haya kama jamii ya watanzania?

  Utaona kwamba jinsi maisha ya mwananchi mtanzania wa kawaida jinsi anavyobanwa na maisha inafika wakati kwamba hawa walioko madarakani sasa hivi wanaandaa kizazi cha watawala (watoto) wao kwani pesa wanazotuibia sasa hivi mbali na kutumika kwenye kampeni za ushindi wa kishindo na kuhujumu mipango na vyama vya upinzani wanahakikisha pia kwamba mtu wa kawaida ambaye hayupo kwenye system hata kusomesha watoto kwenye shule za maana inakuwa kama anasa vile.

  Matokeo ya hili watoto wetu ndio wateja wa shule za kata wakati wenyewe hata shule ya msingi watoto wanasoma nje ya nchi kwa kutumia kodi zetu. Unategemea nini kama waziri wa elimi mwanae anasoma nje ya nchi, nani ataboresha hiyo elimu yenu wakati yeye hai feel?

  Wana JF mie sina muarobaini kwa matatizo tuliyonayo lakini naomba tujadiliane kwa kina hata kama ni kwa miaka hamsini ijayo tupate suluhu ya hili. Sote tunafahamu kugombania haki na mtu mwenye ukwasi ni shughuli lakini wanamapinduzi hawalali wala kukatishwa tamaa na wakandamizaji.

  TANZANIA BILA VIONGOZI WEZI INAWEZEKANA. Take your part as a citizen with concern.
   
Loading...