Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
Rais Kikwete amwagiwa sifa toka Cameroon
Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari
RAIS Jakaya Kikwete amemwagiwa sifa na kutajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa daraja la kwanza duniani, ambaye ni mfano wa pekee katika Afrika, kutokana na utendaji wake unaoonyesha kujali watu wa tabaka zote bila ubaguzi.
Katika waraka wake uliochapishwa kwenye gazeti la The Post la Cameroon hivi karibuni, Mwanasheria wa kimataifa, Mwandishi na mwana-umajumui wa Afrika, (Pan-Africanist) Chief Charle Taku alisema Rais Kikwete alianza kuonyesha kitu cha pekee tangu alipoingia madarakani, kwa kuleta sura mpya baada ya kuamua kuteua wanawake kushika nafasi nyeti za uongozi ukiwemo uwaziri.
Alisema hatua hiyo iliyotoa nafasi kwa Tanzania kupata Naibu Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kwenye Umoja wa Mataifa.
Taku ambaye pia ni Kiongozi wa Baraza la mashauri la Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR) na Mahakama maalum ya Sierra Leone, pia kwenye Baraza la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) alisema Rais Kikwete ameonyesha njia na kuwafanya wanawake kupata upenyo kwenye siasa za kimataifa.
"Kikwete aneonekana kuwa hana mchezo katika kupambana na rushwa, umaskini na maradhi, tofauti na viongozi wengine wengi wa Afrika ambao wameshindwa kabisa kuyapa kipaumbele. Lakini pia ziara yake kwenye magereza, hospitali, kwenye masoko na maeneo mengine inaonyesha nia yake ya dhati katika kuwajenga wananchi wake kuwa watu wanaojitambua na kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao," alisema.
Aliongeza kuwa umaarufu wa Rais Kikwete unaonekana kukua kwa kasi duniani, hasa kutokana na namna alivyotumia nafasi yake kupitia hotuba yake ya Umoja wa Mataifa, akiyataka mataifa duniani kuhakikisha yanapambana na kumaliza vita, umaskini na maradhi, kwa kutoa wito wa kuanzishwa kwa mtizamo wa Jamiii mpya yenye amani ya kutosha duniani, ili kuchochea maendeleo na kudumisha heshima miongoni mwa wanajamii.
Taku alisema wa mara ya kwanza kiongozi huyo wa Afrika aliweza kuzungumza na kuleta mwamko mpya wa kifikra kwa Afrika na dunia akiwa na mtizamo mpya, huku matumaini mapya ya kujali utu, pia kuwasilisha ujumbe maalum wenye maana kubwa kusisitiza amani, matumaini na heshima kwa kila binadamu bila kujali rangi, dini wala asili ya watu.
"Huyu ni miongoni mwa viongozi wa awali katika Afrika, ambaye kwa asil yake, anaonekana kutokuwa na makuu na kuleta mtizamo mpya unaobadilisha mtizamo na kuleta tumaini jipya la viongozi wanaotakuwa kuwepo Afrika, baada ya kizazi cha viongozi wazee waliopo kumalizika, sula ambali ninaamini halina muda mrefu," alisema Chief Taku katika makala hiyo.
Alisistiza kuwa kutokana na mtizamo huo, Rais Kikwete anaonekana kufuata nyayo za baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa ni kipenzi cha watu na mpenda amani, kiasi cha kuufanya hata mji wa Arusha kuwa kituo cha kimataifa, kwa kutoa nafasi kwa masuala mengi yahusuyo mikakati ya kidunia kufanyika hapo.
source mwananchi