Rais kikwete amtolea uvivu david jairo ...apigwa stop tena..

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
1,878
Points
1,500

jamii01

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
1,878 1,500
Rais Jakaya Kikwete

Katibu mkuu kiongozi Philemon Luhanjo ambaye alitangaza kumrudisha kazini Jairo

David Jairo akipongezwa jana

David Jairo akiwa kazini jana​

Rais DKt Jakaya Kikwete ameamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw David Jairo asiendelee na kazi hadi hapo baada ya uchunguzi dhidi yake wa kuchangisha pesa ili Bajeti ya wizara yake ipite ukamilike.

Taarifa hii kutoka bungeni mjini Dodoma imetolewa na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda wakati akijibu swali la papo kwa hapo toka kwa Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe, ambaye alitaka kujua kama Bw. Jairo ataendelea kuwa likizo ili kupisha mchakato wa uchunguzi huo utaofanywa na kamati teule ya Bunge.
"Jambo hilo limekwisha fanya Mheshimiwa Rais", alijibu Mh Pinda kwa utulivu na kwa kifupi baada ya swali hilo, huku wabunge wakishangilia kwa kugonga meza.
Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Bw. Jairo kuripoti ofisini kwa shangwe, ambapo wafanyakazi wa wizara walimpokea kwa vifijo, na wengine hata kusukuma gari lake hadi ofisini, aliporipoti mapema asubuhi.
Uamuzi wa kumrejesha kazini Bw Jairo ulipokewa kwa mtazamo tofauti kwa kila kada nchini, wengi wakihoji sababu ya mhimili mmoja kati ya mitatu iliyopo (Serikali, Bunge na Mahakama) kuingilia mwingine, ikizingatiwa kamba sakata hilo liilianzia bungeni na wengi walihisi ingekuwa vyema Bunge lingelishughulikia hadi mwisho.
Bunge lililidhia kuundwa kwa kamati maalumu kuchunguza tuhuma hizo na inategemewa wajumbe wake watatangazwa kesho wakati wa kufunga kikao cha Bunge kinachoendelea sasa. Ripoti yake inategemewa kutolewa Bunge lijalo
 

Mess

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2009
Messages
667
Points
195

Mess

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2009
667 195
sasa wewe si umeona toka asubuhi watu wanajadili kitu hicho na wewe unaanzisha thread nyingine sasa
 

ByaseL

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
2,225
Points
1,225

ByaseL

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
2,225 1,225
Mie nadhani issue hapa sio Jairo kuchangisha pesa kwa ajili ya Budget. Issue hasa ni pesa hizo zilitumika vipi. Tayari kuna ripoti kwamba wajumbe wa kamati ya Nishati akiwemo Mhe. John Mnyika walipewa bahasha wakazikataa. Uchunuzi wa Ludovick Utoah hakuwenda uko uliishia kwenye pesa ngapi zilikusanywa.
 

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
16,391
Points
2,000

Rweye

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
16,391 2,000
Wengine jamani tulikuwa busy kukata majani ya ng'ombe toka asubuhi hvyo tuacheni nasi tuchangie chidogochidogo
 

Forum statistics

Threads 1,352,850
Members 518,197
Posts 33,067,937
Top