Rais Kikwete amteua Zitto kamati ya Madini

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
JK amteua Zitto kamati ya madini

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Mark Bomani na kuongoza Kamati ya Kuangalia upya Mikataba ya Madini, ikijumuisha wabunge wawili wa upinzani na wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, imewataja wabunge wa upinzani waliomo katika kamati hiyo kuwa ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kupitia Chadema, Zitto Kabwe na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Chadema, John Cheyo.

Kwa upande wa CCM wabunge walioteuliwa yumo Dk. Harrison Mwakyembe wa Kyela na Ezekiel Maige wa Msalala. Wajumbe wengine wametajwa kuwa ni pamoja na Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Wengine ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
 
Nakupa shavu JK.... kumbe mzee ukiamua kufatilia unaweza ....tuondolee Karamagi, kwenye hiyo wizara....Big up thou
 
Hongera sana, tunataka kiongozi anayesikiliza maoni na kero mbali mbali za Watanzania. Hapa umecheza kama Pele, sasa hii kamati ipe meno na isiingiliwe na mtu yeyote katika maamuzi yake. Wawekezaji ni lazima wapate faida, lakini wakati huo huo Watanzania ni lazima tuone manufaa ya madini yetu.
 
Mbona kamuacha Tundu Lissu , na prof.Shivji?
Naamini kama alitaka kupata more inputs angewaongeza hawa ingekuwa na ufanisi mkubwa zaidi .
 
Muh.Zitto angalia hapo ndipo watakapo kupia Sumu ya panya inaitwa ''die slowly' ushauri tu.
 
Hapo anajaribu kuwa smart.Kama kweli JK ana nia ya dhati mi nampa tano.Kumbe Jk alimuona Zitto alikua na point ila sasa mheshimiwa rais uwaambie hao manazi waliomshupalia Zitto bungeni next time wajaribu kuweka maslahi ya taifa mbele.

Lakini kama anaweka usanii itamcost kuliko anavyotegemea.
Hapo nakufagilia mzee,

Hili la kumuweka Cheyo lina utata sana.Kwanini iwe Cheyo kwani hapo mimi naona kama mbunge wa upinzani yupo mmoja tu.Nadhani pia Jk kumweka cheyo hiyo ni strategy fulani fishy anataka kuachieve.

Hebu ngoja tumpe cheyo muda tutamsikia
 
Mnyonge Mnyongeni...........hapa Jk Anahitaji Pongezi.. Wise And Brave Decision. Isije Ikawa Tu Ndio Chanzo Cha Kumfunga Mdomo 'dogo',si Mnakumbumbuka Marmo?mzindakaya? Time Will Tell.
 
hapo ndio tutajua kama kweli Zitto ni chapa kazi au ni chapati tuu
 
Ndo maana nasema hapo kumweka Cheyo mmhhh! ila ndipo ninaposita kumpa pongezi zote JK
 
Poa sana.Nahisi narudia kusema nahisi wanataka kumnyamazisha Zito.Sasa kama kweli wana nia hiyo na Zito hapo ndio tutajua kuwa ni mpinzani kweli na sio mpinzani wa jukwaani
 
Richmond sio?

OMBI: Members, mnapomtamka Karamagi naomba awe Karamagi na msimbatize matusi pls. Tulinde heshima yake hata akiwa mkosaji vipi. Thanks

Ndio mkuu tumekusikia..unaangalia live hapo?kama uko live tupe dondoo maana jamaa kasema El kanyanyuka
 
Karamagi anasema

"Sheria ya madini ndiyo yetu iliyopo unless tunaibadili vinginevyo tutaendelea kuitumia…. Hata

WIzara yangu ina ushirikiano wa karibu sana na kamati ya uwekezaji na biashara na huu uhusiano umedumu nikiwa mwanachama na sasa naendelea kuwa katika sekta yangu, si busara wala si busara kubishana na mjumbe anayesimamia katika kamati, natofautianan sana na Sendeka kwama wizara yangu haijawahi kuacha kutoa ushirikiano… Sijawahi kupokea ombi la kamati kutoa mkataba na wala kuhojiwa… Serikali imepokea na wala hina pingamizi lolote juu ya mapendekezo ya kamati… Kama inavyofahamika serikali ilifanya uamuzi katika mazingora magumu, kwa uwazi na kufuata taratibu kwa mujibu wa mazingira ya wakati huo,, na haina cha kuficha … Serikali haina pingamkizi kwa pendekezo hilo na itatoa ushirikiano na kihakikisha kamati inapata nyaraka na taarifa zote na lengo likiwa ukweli unafahamika. Nitapitia tu baadhi ya hoja za wachangiaji kwa ruhusa ya mwenyekiti…."
 
Sendeka anasimama na kutaka mwongozo wa Spika kwa kusema: "Wakati waziri anachangia, anasema nilisema … Tulimuomba atupe na mpaka leo hajaleta mkataba wa Richmond na Dowans… Naomba mwongozo wa Spika"

Spika akasema: Nadhani Waziri atajibu haihitaji mwongozo

Karamagi: Akiwa katika hali ya kigugumizi, anasema…Si kawaida waziri kujibishana, lakini inawezekana sijapata, lakini nitaomba Mwenyekiti anisaidie….Lakini….
 
Huyo Karamagi ni muoga sana wa maswali.Huwa ni mtu wa kupaniki sana.Debate mashuleni zinasaidia sana
 
Mnyonge Mnyongeni...........hapa Jk Anahitaji Pongezi.. Wise And Brave Decision. Isije Ikawa Tu Ndio Chanzo Cha Kumfunga Mdomo 'dogo',si Mnakumbumbuka Marmo?mzindakaya? Time Will Tell.

-Pongezi za nini? wakati kachelewa sana kutimiza huo ulio wajibu wake?

-Si hilo tu, kashindwa kumuwajibisha kiranja mkuu EL kwa kuzuia/kuzima kamati ya bunge isiundwe yenye jukumu hasaaaa la kutunga hizo sheria!!

-Hii kamati ina tofauti gani na ambayo ingeundwa na bunge waliyo izuia?

Tatizo letu watanzania ni kitu kidogo tu eti pongeziii!! Tunaridhika na kusahau ufisadi wooote anao endelea kuukumbatia!
 
Ndo maana nasema hapo kumweka Cheyo mmhhh! ila ndipo ninaposita kumpa pongezi zote JK

Ben, Cheyo ni kiongozi wa UDP chama ambacho mbali ya kuwa na nguvu kubwa kanda ya ziwa waliko wasukuma wengi, waliunda tume kuchunguza matukio ya maafa katika mgodi wa Bulyanhulu, tume iliyoongozwa na Steven Mhuli. Cheyo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kamati ambayo imekua ikifuatilia kwa kina mapato katika sekta ya madini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom