Rais Kikwete amteua Alan Kijazi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete amteua Alan Kijazi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Friday, May 27, 2011

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  TAARIFA KWA UMMA  UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TANAPA

  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Alan Kijazi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA).

  Bwana Kijazi anachukua nafasi ya Bwana Gerald Bigurube ambaye alistaafu kwa hiari.

  Kabla ya uteuzi huo Bw. Kijazi alikuwa mfanyakazi wa TANAPA kama Mkurugenzi wa Mipango, Miradi ya Maendeleo na Huduma za Utalii.

  Bwana Kijazi alisoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika fani ya Uendelezaji wa Maliasili (MSc. Management of Natural Resources). Awali Bwana Kijazi alipata elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alihitimu Shahada ya Mipango ya Mazingira (BA. Environmental Planning).

  Kabla ya kujiunga na TANAPA Bw. Kijazi alifanya kazi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mwaka 1998 hadi 1999. Pia alikuwa Meneja wa Mradi wa Kuendeleza Uhifadhi wa Wanyamapori (African Wildlife Foundation), mwaka 1999 hadi 2003.


  Uteuzi huo unaanza mara moja.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hongera xana kijazi lakn chunga sana
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hongera xana kijazi lakn chunga sana kama we ni fisadi
   
 4. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mkurugenzi mkuu mwenyewe ndio huyu kwenye picha, au?

  [​IMG]

  Hakuna hata ki profile cha uongo na kweli kueleza professional achievements zake zilizoshawishi watu wamteue, yani Juma na Roza yoyote anaweza kuteuliwa chochote Bongo
   
 5. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi yako ya kwanza tunataka ukweli wa utoroshaji wa wanyama hai kutoka hifadhini kwenda uarabuni kupitia KIA. Wewe huko sio mgeni, na kwa vyovyote unalijua hili vizuri, ukishindwa kushughulikia hili jitoe mapema aje anayeweza.

  Mwinjuma aliimba "mkulima kala mbegu" na " ukipanda bangi utavuna bangi sio mchicha" kwa hiyo hatuwezi hata kidogo kuwaacha hawa watu wachache wale mbegu zetu tukose mbegu za kupanda. Kuiba wanyama hai kuwapeleka nje maana yake ni kuzuia watalii wasije nchini, maana watakuwa wanawaonea wanyama hao hukohuko kwao, huo ni uhujumu mkubwa wa uchumi wa nchi kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Tunataka ukweli kuhusu hilo, ukishindwa achia ngazi, kwa maana inawezekana nawe umo kwenye mtandao huo wa wizi wa wanyama wetu hai, kwa kuwa ule wizi uliotokea ni mtandao, ambao ni mrefu na tanapa ni lazima wawe sehemu ya mtandao huo, kama wewe haumo wenzako wamo.

  Chukua hatua haraka.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Bwana Kijazi alisoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika fani ya Uendelezaji wa Maliasili (MSc. Management of Natural Resources).

  Hivi management = na uendeshaji au ni usimamizi???? hii kurugenzi ya habari ya rais ina matatizo sana ya uelewa wa mambo..
   
 7. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tena mbona huyu hamuulizi iwapo ana uwezo wa kufanya hili au lile kama mlivyouliza kwa yule Internal Auditor?

  Wengine udini mnauweka mbele sana Wakuu.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I am not impressed

  Hakuna jipya
   
 9. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Hongera Kijazi
   
 10. g

  gambatoto Senior Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuteua tu nampa "A". Utendaji "F".
   
 11. g

  gambatoto Senior Member

  #11
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said mkuu. Yote ni Makhirikhiri
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  the guy ni walewale wa siku ziende, safari za ulaya lukuki, maamuzi robo, bubu, nk

  ninamfahamu sioni change tanapa... watauza mpaka ardhi sasa

  sad
   
 13. g

  gambatoto Senior Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye Blue mkuu, hakuna kitu kama hicho chini ya Serikali ya CCM, lasivyo utang'olewa/shughulikiwa.
   
 14. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sasa naona bora kazi ya uteuzi ifanywe na JF, maana kila anaemteua Rais wanasema ni wale wale tu hakuna jipya.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,419
  Likes Received: 19,729
  Trophy Points: 280
  kaka majina yameisha nini hadi utumie hilo hapo
   
 16. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wewe kwanini usiulize unataka waulize wengine?! Muulize aliyemteua ndo anajua uwezo wake, halafu una akili finyu sana unawaza udini hata pasipostahili na ujifunze kuwa na subira maana watu wanaendelea kuchangia hoja labda anaweza kutokea mtu mwenye hoja unayotaka!
   
 17. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Maswala ya dini ni wewe na Mungu wako basi hapa tunajadili mambo kwa maslahi ya nchi yetu Tanzania.
  Elewa matatizo yanayolikabili taifa letu yanatuathili kwa ujumla wetu bila kujali dini kabila wala itikadi za kisiasa.
  Nawashangaa waTanzania wanaochukulia taifa letu kwa misingi ya dini mbili nakusahau kwamba kuna waTanzania wengi ambao hawafungamani na dini za kigeni inakera zaidi inapodhihirika kwamba hata hao mavuvúzela wa dini za kigeni wengi wao ni waumini majina tu au wachumia tumbo maana matendo yao ni kinyume kabisa na mahubili yao.
  Haohao wanaolialia oooh kateuliwa mkristo au mwislamu baadae wakienda pembeni wananongonezana sawa ni mkristo au ni mwislamu mwenzetu lakini sio wa dhehebu letu.
  Hiyo ni dhana potofu ya ubaguzi ambayo inaendelea kutafuna taifa hili hata baada ya miaka arobaini ya uhuru.
  Tanzania ni yetu sote wenye dini za kigeni na wale wasiokuwa na dini yeyote ile.
   
 18. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hongera kijazi angalau tanapa imepata kiongozi mahiri hana urasimu yuko karibu na watu kwa kweli uteuzi huu wa mkuu wa kaya umekaa vizuri , Kijazi kumuona haitaji kutumia mwezi au wiki km mtangulizi wake ila idara mbalimbali hasa prm amepata pigo
   
 19. A

  Ame JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hongera sana mate kwakuteuliwa, tafadhali usiiangushe taaluma yetu ya interdisciplinary; you were trained to solve problems comprehensively naona humu wameshaanza kukuchakachua kwakukosea hata jina la MSc yako!

  Må Gud lede og dirigere hvert skritt i denne nye stillingen, Fred være med dere!
   
 20. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Kama wewe maana inaonekana umeangalia dini yake kwanza kabla ya ku-comment
   
Loading...