Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Afadhali huyu anagawa sasa aliyeingia mikanda ya kisultani mangungo tumweleje yeye na familia yake ndo wanafaidika
 
Lowasa alisema ''mamlaka za juu ziliagiza'' JK nae kasema ''huyo anayetembezwa na ukawa kumwombea kura''.

Bado unajiuliza nani mhusika wa richmond? Jiulize swali lingine.

Mnaona fahari gani kushusha uzi jukwaani kama huna la kutuambia? Ni busara kuchangia michango ya wengine kuliko nawe kuanza uzi na kutuagiza tufikirie swali lingine.
 
muhusika mkuu jamani asiruke ruke ni kikwete na riziwani wake,tutayajua yote baada ya October 25 ukawa wakiingia ikulu
 
Sijui hili ni taifa la aina gani? mtu anayetuhumiwa kwa wizi wa mabilioni ya umma yupo uraiani, tena anazunguka nchi nzima sio kama kajifungia chumbani, lakini wakati ndugu zetu vibaka wa kuku wakiozea segerea, lakini huyo wanayemtuhumu na richmond wamekuwa wakimsema kwa MAFUMBO kila kukicha, mpaka Amiri jeshi mkuu naye ameungana nao kumsema kwa mafumbo badala ya kuamuru achukuliwe hatua mara moja kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine. wanasiasa uchwara wa taifa hili tafadhali tunawaomba mkome kuendelea kuchezea akili za watanzani kwenye majukwaa ya siasa, siasa za vijembe hazina nafasi tena masikioni mwetu. Hatuwezi kufanya uchaguzi wa kitaifa kwa kufwata criteria ya RICHMOND, kamwe richmond haitaamua ni nani anayefaa au asiyefaa kuliongoza taifa hil, ila yule mwenye dhamira ya dhati ya kutuvusha hapa

Hapo mkuu wa nchi amediriki kuonyesha wazi kuwa mw/kiti wa ssem maana yake nn? lakn pia rais wa chama hicho anakuwa dhaifu ktk kufanya maamuz magumu. hata maguful hataweza kufanya lolo

Huu ndio utawala unaozingatia sheria mtu hafunguliwi mashtaka kutokana na majungu ya walevi wa komoni. Ukiondoa kero za wananchi rushwa inakufa natural death, ukibadili mfumo wa utawala ufisadi unakufa natural death, chama kikitawala muda mrefu kinaanza kuongoza kwa mazoea, piga chini, tupa kule!
 
Kamtaja Muhusika sasa tunataka amtaje na MMILIKI wake..... ukiishi nyumba ya kioo usianzishe ugomvi wa mawe.
 
Alishawahi kusema hajui owners wa Richmond na wahusika hawajui

As a commander in chief, aliaminika, sasa leo anakuja kisiasa zaidi

This kasshfa is not over

Na kama kipindi kile waliona kuwa kujiuzuru ni adhabu stahiki iweje leo waitengue na kuona kuwa haifai? Kwa nini hawakumpeleka mahakamani kipindi kile au kwa kuwa alikuwa mwanafamilia??
 
Itajulikana baada ya lowassa kuingia ikulu yote yatakuwa wazi " epa, mabilioni ya uswisi, escrow muamala wa stanbic, madawa ya kulevya, mabehewa na vichwa vibovu, majangili wa tembo, pamoja na wale twiga
 
Fisadi hatakwenda ikulu, endelea kujiandaa kisaikoloji.Huu ni wakati wa hapa ni kazi tu,watanzania wataongea kwa sauti kuu October 25.
Masonjo naona ccm imekutia upofu, hoja hapa ni kwamba wanasiasa wapite kunadi sera zao ili tuwapime katika hilo. endapo wataamua kueleza sera pamoja na ufisadi, basi wauzungumzie na kuuchambua ufisadi kwa UPANA wake kama wanavyotuchambulia sera na ahadi zao na sio nusu nusu, watueelze yoote ya kweli kuhusu RICHMOND, DOWANS, MEREMETA, ESCROW, NYUMBA ZA SERIKALI, KAGODA nk, wawataje wahusika waziwazi na watueleze hatua za kisheria zilizochukuliwa na serilikali iliypo madarakani zidi yao, na kama hawakuchukuliwa hatua wakaachwa wanatembea vifua mbele basi watuambie ni udhaifu na ni mapungufu ya nani kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria hao wezi wanaolihujumu taifa. kama wanaona hawawezi kuulezea ufisadi katika upana huo waache kututia hamu na kuondoka na utamu, badala yake watuambie wamepanga kutufanyia nini miaka 5 ijayo, na wale ambao tuliwapa miaka mitano iliyopita wasiishie kutuahidi bali waanze kutuambia walitufanyia nini na yaliyowashinda ni kwanini yaliwashinda na kwann wanafikiria tukiwapa miaka 5 mingine wataweza kuyafanya yaliyowashinda na mapya wanayotuahidi kwa wakati mmoja
 
muhusika mkuu jamani asiruke ruke ni kikwete na riziwani wake,tutayajua yote baada ya October 25 ukawa wakiingia ikulu

ukiona watoto wanatajana kuhusu aliyekula sukari, usimwadhibu mmoja. Chukua kiboko tandika wote umalize mchezo.
 
Kagoda mmiliki hajulikani hadi leo,Richmond mmiliki ni Mohamed Gire na wenzie-kuwajua anza kudadisi na jina la Mohamed Gire

Vipi na Escrow?! DeepGreen Finance je? Na Meremeta ya kina Warioba na mdogo wake Tangogold vp?!
 
Unanyakanganya udhaifu na ukimya unachanganya ukimya na weakness unachanganya nadharia na utawala wa sheria sijui hata kama unauwezo wa kutofautisha kati ya mahakama na serikali ni vitu viwili tofauti unaweza kumuhisi mtu anakula rushwa lakini ikawa ngumu kuthibitisha mbele ya mahakama na yule mtu akadai fidia zaidi ya ile baada ya kesi in short rais kama taasisi anajua mengi zaidi yetu ila mara nyingi hana uwezo wa kuthibitisha thus why wanaomba msaada kwa raia kutoa taarifa ili serikali ipate nguvu kufanya haki itendeke kupitia mahakama.
Hueleweki, kwa hayo uliyoandika, na majibu ya JK sijui ulitaka kusema nini?
 
Back
Top Bottom