Rais Kikwete ampongeza CAG Utouh kwa kazi nzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete ampongeza CAG Utouh kwa kazi nzuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Aug 23, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ameipongeza Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, NAO, kwa kazi nzuri inayofanya ya kutoa ripoti ya ukaguzi kwa wakati, hivyo kusisitiza ripoti hizo lazima zifanyiwe kazi kwa makini.
  Pia Rais Kikwete amesisitiza imani yake kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, CAG bwana Ludovick Utouh, na kusisitiza kutokana na umuhimu wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, hata yeye kama rais wanchi, anayo mamlaka ya kumteua tuu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu lakini hana mamlaka ya kumfuta kazi.
  Rais Kikwete alitoa hakikisho hilo, katika hafla fupi ya kupokea taarifa ya Mipango Mkakati ya Mika 3 ya Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, iliyosomwa kwake na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, kwenye jingo jipya la Ofisi ya Ukaguzi wa Taifa mjini Singida, hivi karibuni.
  Rais Kikwete amesema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyotajwa kwenye ibara ya 144 ya katiba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hivyo mamlaka yake kama rais ni kumteua tuu mdhibiti
  Nae Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, akieleza kuhusu mpango mkakati wa miaka mitatu 2008/2011, amesema ofisi yake itaboresha zaidi huduma zake ikiwa ni pamoja na kujidhatiti zaidi katika ukaguzi wa value for money.
  Baadhi ya vipengele vya Mpango Mkakati wa Miaka 3 wa Ofisi ya Ukaguzi wa Taifa pamoja na umuhimu wa ofisi hiyo kutakiwa iwe na uhuru zaidi ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Bwano Utouh ametolea mfano wakaguzi kufadhiliwa ofisi na vitendea kazi na mkaguliwa unategemea nini zaidi ya kujisikia kuwajibika kulipa fadhila.
  Kauli ya rais kuwaweza kuwateu baadhi ya watendani lakini hana mamlaka, inajibu baadhi ya dukuduku za mgawanyo wa madaraka kati ya vyombo vikuu vitatu vya dola, Bunge, Serikali na Mahakama ambapo kila kimoja kinatakiwa kutimiza majukumu yake kwa uhuru bila kuingiliwa na kingine.
  Hivi karibuni, kumeibuka mvutano wa maingiliano kati ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania likiishinikiza serikali kuwachukulia hatua baadhi ya maofisa wake, na serikali kushikilia msimamo wa kiserikali ambapo Bunge halikuridhika.
  Ofisi nyingine zinazotajwa na Katiba ambazo rais anayo mamlaka ya kuteua tuu na sio kufukuza kazi ni pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu.
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JK ni bora tuu akae kimya...huwa anatoa pongezi halafu kwenye vikao vya CCM anawageuka.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mimi nilisha kata tamaa miaka kibao na huyu JK tangia siku ile alipo pitishwa kugombea.Hajui kwa nini ni Rais yeye anadhani watu wote ni CCM tu na kwamba ni Rais wa CCM si Tanzania.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mbona taasisi kadhaa zimeshawahi kutoa malalamiko kwamba huyu CAG anafanya kazi bila kufuata kanuni?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuna maeneo vijana wa Utouh wanapokwenda kufanya ukaguzi, tayari wanakuwa na mind set ya lazima wakute madudu, pia kuna maeneo hawafanyi exit conference, wakishapata walichopata, hawasubiri tena majibu ya audit queries bali wanakwenda kuwatundika wenzao msalabani.
  Pongezi za JK ni kwa Utouh mwenyewe na ripoti promtly.
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Strong point, ni kweli kabisa wanachama millioni tano wa CCM, pole pole wanaanza ku-behave kama vile wananchi wote Millioni 40 wa Tanzania ni wanachama wa CCM,

  - Ndio maana huwa tunasema mara nyingi sana kwamba katiba yetu ya Jamhuri ni mbovu mno kwa sababu ilikuwa intended kwa ajili ya utawala wa Chama kimoja na sio siasa za vyama vingi kama tulivyo sasa Tanzania na mpaka hilo litakapo badilishwa tutaendelea kuhangiak tu na hawa mafisadi.

  Respect.

  Field Marshall Es!
   
 7. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160

  Kusema kweli tatizo letu kubwa ni Katiba!
   
Loading...