Rais Kikwete: ampa buriani Nyaulawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete: ampa buriani Nyaulawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwalimu Jr., Nov 12, 2008.

 1. m

  mwalimu Jr. Member

  #1
  Nov 12, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  BILA kutegemewa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye majira ya kama saa tisa hivi aliingia katika Kanisa Katoliki Msasani kuja muaga aliyekuwa mbunge wa Mbeya vijijini, Marehemu Richard Nyaulawa.

  Kanisa hapo palifurika mawaziri, wabunge, wanasiasa wa vyama vyote, wahariri wa habari, wastaafu wa serikali kadhaa na kizazi cha waandishi wa habari na wafanyakazi katika vyombo vya habari wanawake kwa wanaume, Wakiristo kwa Waislamu bega kwa bega wakitoa heshima zao za mwisho.

  Fundisho nililoona kwa upande wangu kanisani hapo-nje nda ndani ni kwamba hatuna sababu ya kuzusha vigomvi vya kijinga kati ya waumini wetu mbalimbali maana hawa wanaishi pamoja, wanafanya kazi pamoja, wanahudhuria harusi za kila mmoja wao na mwisho wa yote wanazikana.

  Marehemu Nyaulawa anasafirishwa kesho Alhamisi kwenda kuzikwa kijijini na nyumbani kwake pale Inyala kando ya jiji la Mbeya.

  Richard Nyaulawa na mwenzake Rashidi Mbuguni watakumbukwa kama ndio wazazi wa kizazi cha waandishi wa habari na wafanyakazi katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. wao ndio waliokuwa wa kwanza kuanzisha gazeti binafsi la Business Times ambalo liliendeshwa kama kampuni na sio shughuli au biashara ya nyumbani.

  Mungu amlaze mahala pema peponi!
   
 2. I

  Iga Senior Member

  #2
  Nov 12, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naam, kweli na mimi nilimuona rais akiingia akatoa heshima zake za mwisho lakini nilishangaa kwa muda alioutumia kusubiri pale maana baadaye sikuona alikuwa akifanya nini. Nadhani alikuwa akiwa ndugu na washirika pole na maneno ya kuliwaza lakini pia nadhani alitumia fursa hiyo kusalimiana na watu ambao alikuwa hajaonana nao muda mrefu kama vile watumishi wa umma wastaafu, wabunge wa chama chake na upinzani na mawaziri kadhaa waliokuwepo pale...

  Kifo hiki tofauti na cha Wangwe kilikuwa kitu kizuri maana kilituunganisha badala ya kutugawa kwa siasa za bei rahisi. Tuendelee na tabia kama hii na tusiwe watu wa fikira fupi na uono usio wa mbali!

  Kesho kwa taarifa ya juujuu kutakuwa na zaidi ya ndege tatu kuwapeleka waombolezaji kwenda kwenye mazishi kule Inyala.
   
Loading...