Rais Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Rais Kikwete ateua Katibu wa Ikulu

Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, uteuzi huo unafuatia nafasi iliyoachwa wazi Rose Lugembe ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

"Rais Jakaya Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba kabla ya uteuzi huo, Mwanda alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu na uteuzi huo unaanza rasmi leo.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
mie nnaomba CV yake, ili tujue uteuzi wa JK uko makini au longo longo. ila kwa vile watu wamekaa kimya inaonyesha yuko makini
 
invisible

nnavyowajua wajumbe wenzangu hapa, wangekuja mbio, au sijui kwa kuwa si mtu wa pwani?
 
bado kuna uteuzi mmoja haujatajwa,changa la macho hilo.hata yule aliyesaini mkataba wa RDC kwa niaba ya serikali kapewa shavu serikalini,uteuzi wote now unafanywa na EL,so anawatanguliza watu wake IKulu ili wawe wanampa habari za ndani
 
hee hee mmmh sio JK eeh? haya ndio tuseme EL ndio akiachiwa ikulu huteuwa bila ya kupewa idhini na muungwana?


mmmh hatukosi la kusema, sasa tunataka kujua jee uteuzi vipi ? alieteuliwa na nafasi aliyoteuliwa inamfaa?
 
bado kuna uteuzi mmoja haujatajwa,changa la macho hilo.hata yule aliyesaini mkataba wa RDC kwa niaba ya serikali kapewa shavu serikalini,uteuzi wote now unafanywa na EL,so anawatanguliza watu wake IKulu ili wawe wanampa habari za ndani
Kwa hiyo hawajaanza leo kuteua kwa niaba
 
Back
Top Bottom