Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
Rais Kikwete ateua Katibu wa Ikulu
Na Mwandishi Wetu
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, uteuzi huo unafuatia nafasi iliyoachwa wazi Rose Lugembe ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
"Rais Jakaya Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilieleza kwamba kabla ya uteuzi huo, Mwanda alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu na uteuzi huo unaanza rasmi leo.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi