Rais Kikwete amefungua rasmi Jengo la Shughuli Nyingi (Multipurpose Hall) la Ikulu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,498
3,465
Jakaya-Kikwete_0.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefungua rasmi Jengo la Shughuli Nyingi (Multipurpose Hall) la Ikulu katika moja ya shughuli zake za kwanza baada ya kuanza rasmi kazi kufuatia upasuaji mwezi uliopita.Sherehe hiyo ya ufunguzi wa Jengo hilo lililoko upande wa kushoto wa Bustani za Ikulu upande wa Lango Kuu la Ikulu, zimehudhuriwa na Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Anne Makinda.

Mara baada ya kufungua rasmi Jengo hilo lenye vyumba 53, Rais Kikwete ametembezwa kuona shughuli zitakazofanyika kwenye Jengo hilo ambalo ukumbi wake mkubwa una uwezo wa kubeba watu kati ya 500 na 1,000 kwa wakati mmoja.

Akimkaribisha Rais Kikwete kufungua Jengo hilo, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa Mradi wa Ujenzi huo, alisema kuwa ukumbi huo mkubwa unaweza pia kugawanyika na kuwa na kumbi tatu kubwa na kutumika kwa wakati mmoja.

Balozi Sefue amesema kuwa Jengo hilo pia lina vyumba viwili vya mikutano vya kuweza kubeba watu 30 na 60, chumba cha Wageni Mashuhuri na jiko lake dogo, chumba cha utawala, chumba cha habari na mikutano ya waandishi wa habari, chumba cha usalama, mgahawa, jiko kubwa lenye chumba cha kuokea na chumba cha kuwashia mitambo itakayotumika katika Jengo hilo.

Kufunguliwa kwa Jengo hilo ni matokeo ya maelekezo ambayo Rais Kikwete aliyatoa mjini Dodoma Agosti 21, 2009, wakati alipoelekeza kujengwa kwa Jengo hilo kwa nia ya kuongeza nafasi ya kufanyia shughuli mbali mbali Ikulu kwa kutilia maanani kuwa nafasi imekuwa finyu kwenye Jengo la sasa la Ikulu lililojengwa mwaka 1902. Aidha, alitaka uwepo ukumbi mkubwa wa mikutano ili kuondokana na gharama za kukodi kumbi wakati wa mikutano ya Ikulu ikiwemo mikutano ya viongozi wa nchi za nje.

Maandalizi ya ujenzi yalianza mwaka wa fedha wa 2010/2011 na kazi ya maandalizi ya kumpata mkandarasi ilichukua miaka miwili na hatimaye ujenzi wenyewe ulianza Agosti 22, mwaka 2012.

Chanzo: Nipashe
 
yaani kujenga kote huko ni kwa ajili ya kufanyia state banquate , huyu jamaa anapenda sherehe
natusingepiga kelele angeleta mdundiko na mnanda ukeshe pale ikulu
 
Hivi pale ikulu kwetu kuna "situation room" walau kiduchu level za ile ya White house? .........Situation room White house ipo chini ya Baraza la usalama la taifa ........hapo Rais anakutana na washauri wake wakuu ..........pia wanaweza kuunganishwa live na mtu yeyote muhimu kwa kutumia mawasiliano salama (ambayo ni ngumu kudukua) ............

Tutafika tu ..............sio vyumba vya kunywea chai ......

Situation room.... Kuna kile chumba chengine huwa wanaita banker(naweza sahihishwa) enewei mwanzo mzuri pengine sisi pia tutafika huko siku moja
 
Situation room.... Kuna kile chumba chengine huwa wanaita banker(naweza sahihishwa) enewei mwanzo mzuri pengine sisi pia tutafika huko siku moja

Nakusahihisha basi ni Bunker ambalo ni Handaki tu maana yake, hivyo ungeweza kuandika/kusema pia handaki ni rahisi kihivyo tu!
 
..hamna kitu wanacho fanya pale ktk ofisi kuu maana wote naona ni maescrow tu....hamna kitu.
 
Huo ukumbi niulizie kukodi kwa ajili ya harusi yangu ni Tshs ngapi? Including mapambo na vitu vingine mhimu
 
Kwa mpango huu Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ni tantalila tu.Hakuna raisi atakaye hamia Dodoma, wote wana penda upepo wa bahari ya Hindi.
 
Nakusahihisha basi ni Bunker ambalo ni Handaki tu maana yake, hivyo ungeweza kuandika/kusema pia handaki ni rahisi kihivyo tu!

Hiki chumba lazima Kiwepo kwenye sehem muhimu Kama Ikulu ...na pia kuna vyumba Kama hivi kwa uhakika kabisa kwenye secret locations or safe houses hapa DAR au mikoani... Ambapo huwezesha Rais na kamati yake ya ulinzi na Usalama ...kuweza ku command Tukio ...na kwa Teknelojia ya Sasa angalau wanauwezo wa kupata live coverage ...
 
Kuwepo kwa vitu vya kiusalama kama hivyo ni muhimu sana ILA SIO KWA UTAWALA WA WAKATI HUU. Kwa nini ninasema hivyo, hakuna utawala wowote unaowedha kuwa thabiti kiulinzi kama Mafisadi na wafanya biashara haramu wameuweka mfukoni. Unaweza kukuta miniti za vikao vikubwa kama vya ulinzi na usalama kabla hazijafika kwa kwa watendaji wahusika watu kama Singasinga wa PAP kesha soma tayari.
Taifa linakuwa kwenye matatizo makubwa sana kama linachekea chekea "mafisadi" ambao kimsingi ni maadui wa taifa.
 
Back
Top Bottom