Rais Kikwete amefanya kila mtu adhani anaweza kuwa rais Tanzania

valour

Senior Member
Aug 3, 2010
168
71
Kazi ya urais sio taasisi ya kuchezea ni taasisi ngumu ambayo inakufanya ufikiri na kutafakari kwa kina kabla hujaamua. Uwe na utashi wa kutatua matatizo na kujua unalisukuma vipi gurudumu la maendeleo. Kwa kipindi utakachokuwa madarakani utatutoa wapi na kutupeleka wapi. Kwa jinsi hiyo mtu inabidi ujipime na ujijue mwenyewe kwamba hapa hata kama nitasukumwa na kundi gani kugombea sitaiweza kazi hii.

Lakini sasa hivi umeibuka mtindo wa kuona kuwa hata mimi naweza kuwa rais. Hii ni kwasababu tumeacha kwenda kutatua kero za nchi lakini tunachofuata ni power, authority and wealth regardless who is hurt in the process.

Rais wetu ametufikisha hapa tulipo maana upole wake umemfanya ashindwe kukemea hata wale wanao onekana kuharibu utawala wake. Kila mtu anaibuka na lake na hakuna collective responsibility. Kuna watu wanajitokeza kugombea urais wakati hata ku 'manage' taasisi hawawezi kutokana na background zao huko nyuma hata matamshi wanayotoa. Kweli nchi yetu inapomoromoka vibaya sana na hadhi yake inashuka kwa speed kali.

Tufanye nini jamani ili tupate kiongozi kama Nyerere, hata Mkapa licha ya madudu yake ya hapa na pale alikuwa ana thubutu.
 
Sheria zetu(katiba) iseme wazi na kuifanyia kazi miiko ya viongozi, na rais aweze kushitakiwa hata katikati ya term yake ya kuongoza!
 
ni kwa kuwa hakuna mtu aliyedhani a cheat person like him can be a president...
 
Sheria zetu(katiba) iseme wazi na kuifanyia kazi miiko ya viongozi, na rais aweze kushitakiwa hata katikati ya term yake ya kuongoza!

Kwahio jamani kila mtu aipe katiba yetu uzito wa juu ili tuhakikishe inambana Rais pamoja na mambo mengine kiasi cha kwamba ni wale tu ambao kweli wanasukumwa na maendeleo ya nchi na umaskini wa watu wake wajitokeze kututoa hapa tulipo. Maana kama kweli Nyalandu kasema USA wanataka awe Rais, ni dhihaka kwetu. Ina maana sisi hatujui ni mtu gani anatufaa. Kweli sasa watanzania tumeoneka majuha. Indeed sad but that is the reality and something needs to be done. Kila mtu kwa nafasi yake ajaribu kufanya atakachoweza kama kushauri, kumwomba Mungu, kuchangia mawazo, fedha etc ili kuhakikisha katiba yetu inamilikiwa kweli na raia wake
 
Tatizo sio Kikwete, tatizo ni katiba yetu, ( mfumo)

bunge linatakiwa kuwa na uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais kisha uchaguzi umpya kuitishwa, mfumo wetu rais hata kama kafanya madudu gani hawezi kuwajibishwa na mtu yeyote.
 
What we need now is a strong person who will revive the institutions which are almost collapsing.

It is easy to be a presdent in the USA, than in Tanzania.
Hapa kwetu kila kitu ni wewe, watu wanakuangalia wewe, wewe ndio wa kutoa direction, bila wewe hakuna kinachofanyika. Nyerere aliyaweza haya.
 
Kikwete siyo kwamba ni mpole ndivyo alivyo hapa hakuna upole ila hana uwezo wa kuongoza nchi .

Kumbuka kauli ya Nyerere 1995 alisema umri bado,yule mzee alikuwa ana saikolojia kali watu walizani ni umri bali alizungumzia kuwa uwezo wake wa kutatua matatizo ya wananchi hana
 
Kuna tofauti kati ya upole na uwezo mdogo.
Kuna tofauti kati ya upole na wizi.
Kuna tofauti ya upole na ujinha.

Napita njaa inaniuma.
 
huyu ndugu yetu uwezo wa kuongoza nchi hana hata kwenye kampeni alikua anauza sura tu na kucheka akinamama wanashangilia hakua na point hata kidogo, na ccm kuona hivyo wakatumia udhaifu huohuo wa kumuuzisha sura hata kwenye mkutano wa kampeni jangwani rais mstaafu akimpiga kijembe Prof.Lipumba na wana cuf kua eti mgombea wenu hakubaliki kwani nani aliyewatuma mlete mgombea mwenye sura ya kijambazi, kwa iyo sera ilikua sura nzuri sio uwezo, we are getting the taste of our own medicine!
 
What we need now is a strong person who will revive the institutions which are almost collapsing.

It is easy to be a presdent in the USA, than in Tanzania.
Hapa kwetu kila kitu ni wewe, watu wanakuangalia wewe, wewe ndio wa kutoa direction, bila wewe hakuna kinachofanyika. Nyerere aliyaweza haya.

CHADEMA wakija na sera za majimbo wanaambiwa wanaleta ukabila. Tatizo la centralisation ndiyo hilo, kila kitu ni rais au waziri. We huoni ajabu waziri kwenda kupandisha nauli za vivuko na vituo vya mabasi??
 
Tutengeneze Katiba,tuunde mfumo mpya wa kuongoza nchi. Tujenge Taasisi za kidemokrasia,tuache kumtegemea mtu mmoja kama kwamba wengine wote hii nchi haituhusu. Pili tuwaondoe kabisa CCM. Wamekuwa kikwazo kikubwa ktk kukuza demokrasia nchini
 
Rais wetu ametufikisha hapa tulipo maana upole wake umemfanya ashindwe kukemea hata wale wanao onekana kuharibu utawala wake. Kila mtu anaibuka na lake na hakuna collective responsibility. Kuna watu wanajitokeza kugombea urais wakati hata ku 'manage' taasisi hawawezi kutokana na background zao huko nyuma hata matamshi wanayotoa. Kweli nchi yetu inapomoromoka vibaya sana na hadhi yake inashuka kwa speed kali.

Tufanye nini jamani ili tupate kiongozi kama Nyerere, hata Mkapa licha ya madudu yake ya hapa na pale alikuwa ana thubutu.

Rais wetu siyo mpole bali ni kuwa hana uwezo, nia na dhamira ya kuifanya kazi ya urais, kihere here chake ilikuwa awe rais bila kujua majukumu ya urais.Mwisho ni kuwa hana sababu ya kuwatumikia watz kwa kuwa katiba iliyopo inampa uwezo wa Mungu mtu kiasi hakuna anayeweza kumuwajibisha hata asipotimiza wajibu wake, na pia kwa vile hahitaji tena kura za watz hivyo anaona bora liende.
 
Kazi ya urais sio taasisi ya kuchezea ni taasisi ngumu ambayo inakufanya ufikiri na kutafakari kwa kina kabla hujaamua. Uwe na utashi wa kutatua matatizo na kujua unalisukuma vipi gurudumu la maendeleo. Kwa kipindi utakachokuwa madarakani utatutoa wapi na kutupeleka wapi. Kwa jinsi hiyo mtu inabidi ujipime na ujijue mwenyewe kwamba hapa hata kama nitasukumwa na kundi gani kugombea sitaiweza kazi hii.

Lakini sasa hivi umeibuka mtindo wa kuona kuwa hata mimi naweza kuwa rais. Hii ni kwasababu tumeacha kwenda kutatua kero za nchi lakini tunachofuata ni power, authority and wealth regardless who is hurt in the process.

Rais wetu ametufikisha hapa tulipo maana upole wake umemfanya ashindwe kukemea hata wale wanao onekana kuharibu utawala wake. Kila mtu anaibuka na lake na hakuna collective responsibility. Kuna watu wanajitokeza kugombea urais wakati hata ku 'manage' taasisi hawawezi kutokana na background zao huko nyuma hata matamshi wanayotoa. Kweli nchi yetu inapomoromoka vibaya sana na hadhi yake inashuka kwa speed kali.

Tufanye nini jamani ili tupate kiongozi kama Nyerere, hata Mkapa licha ya madudu yake ya hapa na pale alikuwa ana thubutu.

Kwenye bold red nivizuri kutumia neno sahihii SIYO upole

Tupendekezeeya kufanya
 
Kwani hawezi kuwa rais. Vipi ujenzi wa daraja la kigamboni? wenzake walishindwa yeye ameweza.

Hongera JK
 
Sio kazi ya RAISI kuziba midomo watu wasiongee?..Hata ww sema unataka uwe raisi,,acheni ufala
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom