Rais Kikwete alimpongeza Filikunjombe, leo amwona adui NEC? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete alimpongeza Filikunjombe, leo amwona adui NEC?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete akimpongeza mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kwa kutekeleza ilani ya CCM mara alipotembelea jimbo hilo mwaka jana

  Utendaji kazi wa Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, umemfurahisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisema kuwa utendaji kazi wa Filikunjombe ni utendaji wenye kasi ya kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wa Ludewa, katika Mkoa mpya wa Njombe.

  Akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Kata ya Mawengi, hivi karibuni, Rais Kikwete alisema kuwa utendaji kazi wa Mbunge Filikunjombe ni ishara tosha kuwa wana CCM hawakukosea kumchagua mbunge huyo katika kura za maoni, "jambo lililopelekea wapinzani kumheshimu ambapo hawakujitokeza kumpinga Filikunjombe katika Uchaguzi Mkuu na hivyo kumfanya apite bila kupingwa".

  Aidha, Rais Kikwete alionyesha kufurahishwa zaidi na mikakati mizuri ya Mbunge Filikunjombe baada ya Filikunjombe kumweleza wazi vipaumbele vyake vikubwa viwili atakavyoanza navyo katika Wilaya ya Ludewa.

  Filikunjombe alivitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na "kuhakikisha bara bara ya lami inaanza kujengwa Ludewa [ambapo toka Tanzania ipate uhuru wananchi wa jimbo la Ludewa hawajawahi kuiona lami] na pia kuhakikisha kuwa Uchimbaji wa Liganga na Mchuchuma unaanza mara moja".
  "Hamkukosea," alisema Rais Kikwete huku akiwashukuru wananchi kwa kumchagua Deo Filikunjombe kuwa Mbunge wa Ludewa.

  Pamoja na kupigania usafiri bora Ziwa Nyasa, Filikunjombe pia, amekuwa akipigania uwepo wa soko la uhakika kwa zao la mahindi kwa wakulima wa Ludewa, jambo lililopelekea serikali, mwaka huu, kununua mahindi katika vituo vya Mawengi, Ludewa Kijijini, Shaurimoyo na Mlangali.

  Rais Kikwete aliviunga mkono vipaumbele hivyo akisema kuwa ni vipaumbele vyenye tija katika maendeleo ya Wilaya ya Ludewa na kwamba ni azma yake yeye Rais Kikwete kuona kuwa juhudi zaidi zinaelekezwa katika wilaya hiyo.

  Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa, amewataka wananchi wa Ludewa waendelee kushirikiana na Mbunge Filikunjombe kwani anaitekeleza vema ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

  "Sasa ni zamu ya Ludewa kubadilika ki-maendeleo," alisema Rais Kikwete akisisitiza kuwa serikali yake itaelekeza nguvu zaidi jimboni humo akiongeza kuwa, Ludewa imechelewa mno kupata maendeleo.

  "Nitakuja tena Ludewa," alisema Rais Kikwete ambaye pia aliwashukuru wananchi kwa kuwachagua madiwani wengi toka CCM. "Ludewa kuna madiwani 32 na kati ya hao ni Diwani mmoja pekee ametoka upinzani, huu ni ushindi mnono," alisema Kikwete.


  Filikunjombe, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, alimweleza Rais Kikwete kuwa pamoja na kwamba Taifa linasherekea miaka 50 ya Uhuru, wakazi wa Ludewa walikuwa bado hawajapata uhuru na kwamba, mwaka huu chini ya utawala wa Rais Kikweye, Ludewa ndo wanapata uhuru wao baada ya kuwa na uhakika wa barabara ya lami na kuanza kutekelezwa kwa miradi wa Liganga na Mchuchuma.

  Rais Kikwete alikuwa wilayani Ludewa kufungua mradi wa umeme wa KW 150 uliotekelezwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ACRA, Ubalozi wa Italia, pamoja na Jumuiya ya Ulaya.

  [​IMG] [​IMG]

  Nimelazimika kiurudia habari hii hapa leo ili kuona ni jinsi gani CCM inavyojitafuna yenyewe rafiki wa leo ni adui wa kesho ndani ya CCM.

  Ni nani alitegemea leo kama CCM chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete ingemuengua mbunge Filikunjombe na Mkono katika orodha wa wagombea wa wajumbe wa NEC wilaya katika uchaguzi ndani ya chama kwa utendaji wao wabunge hao?

  Ila pia naweza kujifunza jambo ndani ya CCM hawapendi kabisa uwe msemakweli ama mpambanaji wa ufisadi wanapenda zaidi kulindana na ndio sababu ya akina Filikunjombe ambao walionekana wazuri kwa kuungana na wapinzani kuorodhesha majina yao kwa kutaka waziri Mkuu ajiuzulu kwa kufumbia macho mafisadi leo wamegeuka ni wapinzani ndani ya CCM.

  Hivyo kwa mwendo huu ni vigumu kwa hata hao ambao wamepitishwa kuja kufanya vizuri kwa maana ya kuwatumikia wananchi kwa kupinga ufisadi zaidi ya kuendelea kunyamaza kimya huko mafisadi wakiendelea kupongezwa na kubembelezwa ndani ya CCM.

  Hapa ndipo napo sema ni heri CCM kutokana na mwendo huu ikaa pumzika ili kujipanga upya badala ya kuondolewa kwa aibu mwaka 2015 na upepo huu wa M4C kiukweli CCM inajichimbia kaburi lake na kujiandalia mazishi kabla ya kifo chake .

  Binafsi napingana hata mfumo uliopo ndani ya CCM kwani leo tunashuhudia mwenyekiti ni Rais wa nchi hivyo hata kama atakosea ni vigumu kumkemea kiongozi wa nchi .

  Ila pia siungi mkono kabisa watoto wa wenyeviti wa CCM Taifa na Rais kupewa nafasi ndani ya CCM kwani leo tunashuhudia CCM kuna makundi mbali mbali lipo kundi la Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa , lipo kundi la mtoto wa Rais ambaye ni mjumbe wa baraza kuu la UVCCM sasa badala ya kuvunja makundi hayo tunakazana kuwaziba midomo akiwa Nimrod Mkono na Deo Filikunjuombe .

  Hata salama nzuri ya chama iliyoasisiwa na baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere ile ya kidumu chama cha mapinduzi !!! inavurugwa sasa na kuwa Kigumu chama cha mapinduzi!!??

  Haya jamani wana CCM hiyo ndio CCM na akina Nape Nnauye na Dkt Jakaya Kikwete ipo siku litabaki jina huu ni mtazamo wangu


  Source:
  Habari: Mzee wa matukio daima,
  Picha: File

   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Deo Filikunjuombe alikosa sifa moja tu kupata nafasi ya kugombea huko NEC nayo ni ufisadi Angekuwa nayo muda huu ungekuta anajiandaa kwa uchaguzi
   
 3. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  CCM ni chama kisicho na dira, hivyo maamuzi yake yasikupe taabu sana kwani hayana dira.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Kikwete ndumilakuwili, hamna haja ya kujipendekeza kwake
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  its sound lyk true,,,,bt what iz abt MKONO???
  NADHAN NI KUKOSOA LIVE
   
 6. i

  iseesa JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hili la Filikunjombe kutokuingia NEC ya MAFISADI natumai limekaa sawa na siyo UADUI. Kwake natumai iwe FARAJA kwa kuwa si mmoja wao kwenye JOPO la MAFISADI. Cheers Filikunjombe
   
 7. C

  Concrete JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio tabia halisi ya JK kazi yake ni kuwatumia wanasiasa wampambe akishakuchoka anakutupa kama Condom!

  Nape wakati wake unakaribia, akae tayari tayari.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Vipi babu yako Mkono alikosa sifa gani.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Unafuki ni moja ya sera ya hiki chama
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Alisaini waraka wa kumpindua Pinda....katika duru za kisiasa that was a treason!
   
 11. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Swali la msingi la kujiuliza,
  NANI MWENYE AKILI TIMAMU NA UWEZO WA KUCHAMBUA HOJA ANAYEMWAMINI KKWETE?
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Sahihi za zito zilimpoza
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyo fisadi kilichomponza ni sahihi za zito za kumuondoa waziri mkuu
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Ritz namsikitikia sana Mzee Mkono licha ya ukongwe wake wote lakini ameshindwa kujuwa kwama Zitto Kabwe ni karani wa JK na kukubali kurubuniwa kumbe mwenzake baadaye anaripoti yote kwa Boss wake. nimeshangazwa sana Nimrod kuingizwa mgenge na Zitto.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  umegundua mkuu matola, zito alitumika na kikwete kugundua ni nani wanaompiga vita ndani ya chama wasiujua wakaingia kichwa kichwa na sasa yamewapata ila hii itatusaidia kujua mengi zaidi.ila tatizo kubwa la ccm kwa sasa ni unafiki na bahati mbaya mnafiki zaidi ndio kichwa cha chama kwa sasa.
   
 16. m

  malaka JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ogopa JK kwa visasi. refer: Babu Seya!!! Usiniulize.
   
 17. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Tukuulize wewe mwenye habari motomoto za CCM.
   
 18. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  "An empty stomach is not a good political leader"
   
 19. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Ahamie Chama Kubwa CDM.
   
 20. o

  obwato JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huu ni mkakati wa kumpunguza nguvu, si unafahamu kuna mwana dada mrembo mwenye vinafasinafasi vingi ndani ya chama ameshaandaliwa kuchukua lile jimbo? Ila Deo anauzika maana hana alufu za ukijani halisi, wakijichanganya yatawakuta ya Iringa mjini. Tusubiri.
   
Loading...