Rais Kikwete akutana na viongozi wa wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete akutana na viongozi wa wafanyakazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Apr 20, 2011.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Aprili 20, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini.

  Mkutano huo wa kawaida kati ya Rais Kikwete na vikundi mbalimbali vya jamii kikiwemo kile cha viongozi wa wafanyakazi umefanyika Ikulu, Dar es Salaam katika mazingira ya kuelewana.


  Mkutano huo umechukua kiasi cha saa tano na kuhudhuriwa na viongozi 20 wa wafanyakazi, mawaziri wanaohusika na masuala na haki za wafanyakazi na watumishi wengine waandamizi wa Serikali.


  Viongozi wao wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bwana Ayoub Omar Jumaa umeshirikisha viongozi kutoka TUCTA yenyewe, Chama cha Walimu Tanzania (CWT), TPWU, TEWUTA, DOWUTA, TRAWU, CHODAWU, TUICO, TASU, TAMICO TUGHE na COTWU.


  Mawaziri waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Gaudencia M. Kabaka, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Umma, Mheshimiwa Hawa A. Ghasia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mheshimiwa George Huruma Mkuchika.


  Katika kikao hicho, pande hizo mbili zimejadili masuala mengi yanayohusu haki na maslahi ya wafanyakazi na masuala mengine muhimu ya taifa yakiwamo madai ya malimbikizo ya malipo ya wafanyakazi ikiwamo mishahara.


  Rais Kikwete na viongozi hao pia wamejadili kuhusu uwezekano wa Serikali kuongeza mishahara ya watumishi kwa kuzingatia upandaji wa gharama za maisha, uwakilishi wa wafanyakazi katika mchakato wa kuandaa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na uwezekano wa Serikali kupunguza kodi kwa wananchi ili kutoa ahueni zaidi ya maisha kwa wananchi.


  Kuhusu sera ya Serikali ya kupunguza kodi ili kutoa ahueni ya maisha kwa wananchi, Rais Kikwete amewaambia viongozi hao wafanyakazi: "Hili tulikwishakubaliana kuwa lazima tuchukue hatua za mara kwa mara kuongeza unafuu wa maisha kwa wananchi wetu. Tutaendelea nalo hili kwa sababu ni muhimu sana. Suala kubwa hapa ni kutekeleza sera ya kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi. Lazima tufanye kila liwezekanalo kufanikisha hili."


  Kuhusu ombi la viongozi hao kuwa Serikali itoe dhamana kwa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) ili kuliwezesha shirika kuwa na uwezo wa kukopa fedha katika mabenki kusaidia kuliimarisha, Rais Kikwete ameigiza Wizara ya Fedha kuchukua hatua za haraka kuhakikisha hili linafanikiwa. "Tulifanye hili haraka sana, halina sababu ya kucheleweshwa kwa sababu TTCL ni shirika muhimu sana."


  Mwisho.


  Imetolewa na:


  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais
  ,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM
  .

  20 Aprili, 2011


  MY TAKE; Ni kikao kilichokuja siku 11 kabla ya sherehe za mei mosi. Hii inaashiria nini??
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameenda kuelezwa namna na protokali za kufuata watakapomkaribisha Mwaka huu. Ni ule mtindo maarufu ' You screach my back and I screach yours' wizi mtupu.
   
 3. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ni mwanzo wa mahusiano mazuri baina ya serikali na vyama vya wafannyakazi, bravo JK
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...........Wazo linaonekana kama zuri,my be tutafakari kwanini imekuwa siku 11 before mei mosi..
   
 5. B

  Blessing JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamaa amekosa kazi ... Anaongea na wafanyakazi nini wakati wote ni mafisadi tupu.

  Let him not wash his dirty linen in public -- it is too dirty to see.
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hana lolote huyu m k w e r e hajui kazi aliyoiba.
   
Loading...