Rais Kikwete akutana na Gordon Brown

610x.jpg

Kikwete ana marafiki wawili sasa - Bush na Brown.

Kazi nzuri sana baba Kikwete, tengeneza maisha ya watanzania na wapinzani wao walie tu na wivu wao uliokubuhu.
 
kwa taarifa yenu sasa hivi ni wakati muhimu sana wa kumsapoti JK pamoja na udhaifu wake. CCM ya mafisadi wanamkalia kooni vibaya mno. Na sisi JF tukimkalia kooni hatakuwa na sapoti popote bali ni kuanguka kisiasa na nchi kurudi kwenye kundi la majambazi (akina mkapa). Tutakuwa JF tumepata nini hapo? Tafakari

Na kwa kuongezea kidogo tu ningependa wana JF kufahamu kwamba Raisi wetu ana nia dhabiti ya kuisaidia Tanzania na watanzania.

Jakaya amekuwa ndani ya chama na serikali kwa muda mrefu sana hivyo anajua kila baya na zuri linaloendelea na nini kifanyike.
Lakini kama manavyojua si rahisi kupambana na maadui walio kamilika kama huna silaha na uwezo. Alichofanya Jakaya alitumia usemi wa Mao-Tsetung kwamba "Kama huwezi kupambana na adui ukiwa nje ya system basi jiunge nao then upambane nao ukiwa ndani ya system". Jakaya ni kweli amewatumia mafisadi kwenda ikulu lakini sasa ameanza kumtosa moja baada ya mwingine kwa staili ya kuwaachia wajikaange kwa mafuta yao wenyewe. Alijua wazi kwamba Chenge, karamagi na Lowasa ni mafisadi lakini ametumia ujanja wa kujiosha mikono na kuwaacha wajikaange na mafuta yao wenyewe na ndipo anapowatema moja baada ya mwingine.
Kwa mamlaka aliyokuwa nayo kama Raisi wa Jamhuri angeweza kabisa kuwaita wabunge wote wa CCM ambao wanafanya idadi kubwa ndani ya bunge na kuwakoromea kwaambia kwamba acheni mara moja kulivalia njuga suala la Richmond kama angetaka kumlinda Lowasa na wengineo, lakini amekaa pembeni ili akina lowasa wajikaange kwa mafuta yao wenyewe.
Angeliweza pia kama Raisi kutoa amri na kuwakamata mara moja na kuwaweka ndani, lakini katika siasa kuna namna na jinsi ya kumtema mtu huku wewe mikono yako inakuwa safi. Jakaya anajua wazi kwamba siasa ni mchezo mchafu, hivyo yeye pamoja na kwamba ni Raisi lakini pia ni mzazi na kama atakwenda kichwa kichwa ama fasta fasta hayo mafisadi ndani ya CCM yatamkolimba mara moja.

Hivyo wana JF tungempa support yetu Jakaya ili atusafishie upuuzi ndani ya nchi yetu. Ni kweli kwa sasa mafisadi mengi ndani ya CCM yanamchukia sana Kikwete kwani yalifikiri ni mwizi mwenzao kumbe si hivyo.
 
Back
Top Bottom