Rais Kikwete akaribisha wawekezaji wa Malaysia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete akaribisha wawekezaji wa Malaysia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by sulphadoxine, Jun 23, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Rais jakaya kikwete ameiomba serikali ya Malaysia kuvishawishi vyuo vikuu vya nchi hiyo kuanzisha ama kuamishia shughuli zao hata ikiwezekana kujenga majengo ya vyuo hivyo,katika Tanzania.
   
 2. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kwanini aombe badala ya yeey kama Raisi kuweka mazingira mazuri ya watu wa nje kuwekeza kama vile uatikanaji wa umeme n.k. Anamalza fedha zetu buere kuzururua juzijuzi alikuwa Geneva katika mkutano wa ILO akiongea pumba tupu, mara Setchelles na sasa Malaysia.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kwa umeme gani?
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  umeme huu wa kimagumashi,hii ni nchi ya kisanii kwa hiyo kila kitu ni usanii tu.
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Red:jamani si mnamjua Rais wetu ni msanii,anaweza kuweka mazingira mazuri na watu wakaja kuwekeza///
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye red, mimi hakuna aliyenialika kutoka kijijini kwetu Kalangala kuja mjini pia, ni mazingira tu!
  Lakini pia tukumbuke kuwa ameshakaribisha utitiri wa mikutano na matokeo ya muda mfupi ni yafuatayo:

  • Umeme umekuwa shida zaidi
  • migogoro makazini, vijijini na vyuoni imeongezeka
  • shiringi yetu ilikuwa $1=Tsh. 1,150/- wakati anachukua nchi sasa ni $1=Tsh. 1,650/-
  • njaa imeongezeka vijijini
  • bei za vyakula zimepanda maradufu
  (ongeza vingine au punguza penye makosa) labda tusubiri matokeo ya muda mrefu kama kifaranga anayesubiri mama yake (kuku) ampe nyonyo!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Heko Kikwete, naunga mkono juhudi zako, na wasioziona wana yao.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania ilipata uhuru around the same time na Malaysia, leo hii bila aibu tunaenda kuomba huko! Jana bungeni Myinka, Lissu, Zitto wamepiga kelele kuhusu misaamaha ya kodi kwa SEZ & EPZ. Kwa taifa ombaomba inakuwaje tunatoa msamaha wa miaka 10 tena kwa makampuni ya mtaji mdogo? Huko Malaysia tunakopiga magoti wao wanatoa msamaha wa miaka 5.

  Rais Kikwete anatakia atambue kuwa 'solutions' za matatizo yetu zitatoka humu humu ndani na sio kwenye nchi nyingine. Watanzania ndio wenye ufungo wa ku-lock outside matatizo yatu na solution hiyo in my view iko kwenye LEADERSHIP. Maadam ungozi wa ccm wameonekana kutojuwa au kukataa kujuwa mara watanzania wanapotoa orodha ya mambo ya kufanya ili nchi iende, basi hatuna budi kuwaondoa wale woooote wanaziba masikio na kuendekeza hii theory ya ku-import solution. CCM must go kama kweli tunakata kuondoka na hii fedheha ya kuwapigia magoti wanaume wengine kila asubuhi tukiomba misaada.
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Wenzetu walipopata Uhuru waliweka misingi mizuri, sisi tuliwekewa misingi mibovu, waliopo sasa madarakani inabidi waibomoe hiyo misingi mibovu, kwani msingi wa nyumba ya vyumba sita uliowekwa baada ya uhuru, huwezi kuujengea "sky scrapper". Umeshabomolewa na sasa ndio tunaanza kuweka msingi wa "sky scrapper". Wakulaumiwa ni nani kwa kuwa tuko nyuma?

  Hiki cha sisi kuvutia wawekezaji kwa sasa wenzetu wa Malaysia walikifanya miaka hiyooo, soma habari za Mahathir Muhammad.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Maendeleo hayatokani na sky scrapers FaizaFaoxy, you need to learn a thing or two about foundamentals of sustainable national development. Malaysia wamewekeza kwenye rasiliamli watu - INVESTED IN HIS PEOPLE. Tanzania tunaonekana kufanya kinyume.Matokeo ya form IV mwaka 2010 yanaonesha nchi inayoelekea kuzimu. 80% ya wYanafunzi wamefli. Yaani zaidi ya 150,000 ya vijana walifanya mtihani sasa wako mtaani pengine wanauza viberiti na maji baridi. Mwaka huu wadogo zao kwa maelfu watajumuika nao mitaani. Wewe unaongelea physical building. Nikuulize hawa wanaouza viberiti wanafaidiake na sky scrapers? Only twisted mind ndio anaweza kupima maendeleo kwa majengo!
   
 11. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mkuu hujamuelewa vizuri FaizaFoxy. Hajakusudia skyscraper kwa maana ya nyumba, huo ni mfano tu.
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida yake kama alileta IPTL,Barrick Gold,Richimond,Symbion,atashindwaje kuwaleta wezi wengine waje kujichotea kwenye shamba la bibi tunajua huyo hawezi kuacha juzijuzi hapa kawaleta rafiki zake na dege la kivita qatar waje wajichotee wanyama
   
 13. m

  mjinga JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Salaam aleikhum
  wewe kweli ni Muislamu? Unajua dhambi ya unafiki? Umeajiliwa kwa kazi hiyo kwa bei gani? Unajua comments zako zita kukost? Kumbuka Allah yupo mpaka humu ktk komputa. Masalaam
   
Loading...