Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,

Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
 
Jamani nishasema humu jamvini msije shangaa J'tatu watu tunasubiri matokeo jamaa anateua watu.
 
Ebu Sasa Tuambieni Wana CCM; Tuseme Kwa Bahati Mbaya Magaufuli Akabahatika Kuupata Urais wa JMT, Je Walioteuliwa Jana na JK

Atarecall uteuzi Huo.Hii Sasa Ni Too Much, Nadhani JK Anajaribu Kucheza na Psychology/Bongo za Wapiga Kura. Wapiga Kura Ebu Jitokezeni

Tuwaonyeshe CCM ya Kwamba Rais Uchaguliwa na Wananchi na Sio Kuteuliwa na Viongozi wa CCM.Kesho Pigeni Kura za hasira

Tujinasue Na Minyororo Hii ya Kujiona Wanyonge kwenye Nchi yetu.


Ninawasiwasi Na Uchaguzi Huu..Tutaweza Kumaliza Vibaya Kwani Kuna Kila Dalili za Wagombea Kutofika salama.../ Uchaguzi Huu Ni

Mkali na Upepo Unavuma Kulekea Upande wa Lowassa/Ukawa. Je Itakuwaje Mh. Lowassa Akishinda, na je atakubali wateule wa jana Waendelee na Nafasi zao.

Kesho sio Mbali Tutajua Mbivu na mbichi...
 
huyu jamaa ahamini kama kesho anafungasha viragoo//////// hapa makomeo anaenda kuwa bawaba tu ila mlango ni jk
 
Yaani huwa nalaumu sana walompgia kura huyu jamaa,hii ni zaidi ya kero, cjui hata ni wa kuweka kundi gani
 
Maswi karudi tena? nimeamini huyu jamaa sio mzima kichwani na hakitakii mema chama chake!
 
Wakuu ikulu ni shangwe Jk anadhihirisha serikali yake ni ya kishikaji amemteua shemeji yake Omar chambo Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini
 
Ulaji wa mwisho mwisho kwa washikaji wapige nao pesa zao. Anapanga timu yake ya ulaji hata akiwa amestaafu simu itakuwa inafanyakazi kulipana fadhilla.
 
Omar chambo ni mpiga dili mkuu alikuwa wizara ya uchukuzi akashindwana na mwakyembe Leo kapelekwa kwenye gesi
 
Wanini hawa wakati tunategemea Rais mwingine kesho?

wataendelea kuwepo,,,unafikiri rais mpya anaanza kuondoa wafanyakazi kazini,,,itachukua kama miaka 2,kabla rais mpya hajaweka watu anaowataka yeye,,sio jambo la kuapishwa leo na kuanza kuondoa makatibu tawala,,etc
 
Mdeni Kipande,alikuwa bandarini. Hatari kama nungwi,nahodha sio kirikou
 
Back
Top Bottom