Rais Kikwete Aenda Japan!!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Habari ifuatayo chini imenifanya nikumbuke video hii:

[media]http://www.youtube.com/watch?v=bNF_P281Uu4[/media]

Kipengele cha habari hii kinatoka: issamichuzi blog.....

JK aenda japani leo:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 0 kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe, Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman, Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami na Mbunge wa Muleba Kusini na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.



Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam
25.05.08
Source link: http://issamichuzi.blogspot.com/
 
Khe khe khe .... isije ikawa anapitia Malasyia kumuona Robert Mugabe kupanga mikakati ya kumuua Tsvangirai. Kwi kwi kwi....................

Nchi ameachiwa mzee wa mikasi na butcher za nyama.
 
kikwete anaenda japan, na akirudi tu anakwenda kufungua mkutano wa sulivan! i am not sure that this guy is thinking right!

akiwa Japani, JK hawezi hata kukutana na watanzania wa kule kwa sababu inabidi akimbilie mkutano wa Sulivan! for real i think he is over doing it. sio kama nchi kila kitu cha fame afanye yeye !!
 
Mimi kwenye hili la safari nilisha nawa mikono, pale Membe aliposema kuwa mkuu hasafiri kama mkuu wa SA, basi nikanawa mikono hasa kwa kuelewa kuwa Membe naye either anatayarishwa au anajitayarisha kwa urais!

Mungu Aibariki Tanzania!
 
Vipi mkuu ana mpango wa kutupitia na sisi huku MALTA siku za karibuni?!
 
Mimi kwenye hili la safari nilisha nawa mikono, pale Membe aliposema kuwa mkuu hasafiri kama mkuu wa SA, basi nikanawa mikono hasa kwa kuelewa kuwa Membe naye either anatayarishwa au anajitayarisha kwa urais!

Mungu Aibariki Tanzania!

Mkuu FMES;

Naomba msaada kidogo angalu mkuu wangu... mimi nakuaminia sana...

Je kwa safari hii on hand alitakiwa asafiri nani zaidi ya Rais mwenyewe?
 
hii sawa angeenda yeye, lakini safari hii aliijua mwaka mmoja nyuma, kwa hiyo angepanga kiasi cha kupunguza zisizokuwa za lazima ili apate kwenda hii.

mie kwa upande sioni umuhimu wa JK kufungua mkutano wa Sulivan, angeenda kuunga instead na huko nje angepata kukutana na wananchi wake na kuwasikiliza maoni yao
 
Heee mara kisha tia tim..
Sii alikuwa Japan hivi Majuzi ama naota ndoto za mchana!...
 
hii sawa angeenda yeye, lakini safari hii aliijua mwaka mmoja nyuma, kwa hiyo angepanga kiasi cha kupunguza zisizokuwa za lazima ili apate kwenda hii.

Hakuna kitu; tunajadili mambo kiimla sana... zitaje hizo safari... Wengi mnazo lalamikia safari za Rais hamna zozote za maana mnazozungumzia...
 
Heee mara kisha tia tim..
Sii alikuwa Japan hivi Majuzi ama naota ndoto za mchana!...

Ndio mkuu alienda kwa mission nyingine... na Alienda kama Rais wa Jamhuri tena kabla hata ya kuwa Mwenyekiti wa AU.

Sasa ameenda kama Mwenyekiti wa AU; Yeye sio malaika kwamba angejua angechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Africa hivyo angekuwa na Kikao wakati huu...

Jadilini hoja za maana kama hakuna tuache kutoa vioja!
 
Hakuna kitu; tunajadili mambo kiimla sana... zitaje hizo safari... Wengi mnazo lalamikia safari za Rais hamna zozote za maana mnazozungumzia...

...Carbon footprint!

anachangia kwa namna fulani global warming kwenye hizo carbon emissions za ndege anazosafiria kila mara,

does it make sense sasa?
 
viongozi Wa Afrika Wametuweza Kweli Kumpa Huyu Kilaza Wetu Uenyekiti Wa Au...wamejua Anazipenda Safari Na Karibu Alikuwa Anakosa Sababu Za Kusafiri Sasa Kwa Hii Kofia Ya Mwenyekiti Wa Au...basi Hakosi Sababu!!!
 
1.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 08) kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

2.
Je kwa safari hii on hand alitakiwa asafiri nani zaidi ya Rais mwenyewe?

Mkuu Kasheshe,

Heshima mbele, ukinisikia ninasema something ujue nina sababu mkuu, hizi safari huwa wanazipanga kwa sababu walizonazo kisiasa, na sio zote huwa ni muhimu sana, mkuu alipoenda India ilikuwa ni kuikimbia ishu ya Chenge, kupekuliwa, alipokwepa kwenda London na kukimbilia NY ilikuwa kukwepa waandishi wa habari kule London on ishu ya Chenge, hii safari ya Japan ina nia moja tu, nayo ni kukwepa ishu hii ya Balali,

Ninaomba nikuulize, iwapo rais angekuwa anaumwa ingekuwaje? Hiyo mikutano ingeaahisrishwakwa sababu yeye hayupo?
 
..na Alipotoka London Tarehe 1 May..akawa Uganda Hadi Jioni Kukwepa Kuwahutubia Wafanyakazi Meimosi..maana Alishaaga Hatakuwapo....sasa Na Hii Sijui Nakimbia Hili Wimbi La Mauwaji Ya Balali...akirudi Moja Kwa Moja Anaenda Kutua Kia - Arusha Anaosha Jina Na Mkutano Wa Sullivan...maisha Yanaendelea...

..sijafahamu Ukubwa Wa Ujumbe Wake Huko...na Sijui Kamtosa Tena Mama Ziara Hii Kama Ile Ya Mara Ya Mwisho.....maana Siku Hizi First Lady Naye Ana Ziara Tofauti Na Za Rais ...badala Ya Ilivyozoeleka Kufanya Ziara Bega Kwa Bega Na Rais[jukumu Lake La Kwanza Ni Kumtunza Rais]....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom