Rais Kikwete aagiza flyovers zijengwe Dar haraka sana

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Date::6/2/2010
Mwandishi Maalumu

RAIS Jakaya Kikwete, ameagiza hatua za haraka zichukuliwe, kujenga barabara zinazopita juu katika Jiji la Dar es Salaam, ili kupunguza misongamano mikubwa ya magari.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM alitoa agizo hilo juzi, baada ya kupewa taarifa ya utendaji ya CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu ya kukagua shughuli za CCM mkoani humo.

"Hili la flyovers lipewa kipaumbele ili tupunguze msongamano wa magari katika Dar es salaam. Tusipofanya hili jiji hili litakuwa halipitiki katika muda wa miaka mitano, ama hata katika miaka miwili ama mitatu ijayo," Rais Kikwete.

Rais Kikwetepia aliwaagiza wataalam wa mipango miji katika Jiji la Dar es Salaam, kuanza kupunguza maeneo yasiyopimwa kwa kuzingatia kuwa kwa sasa ni asilimia 30 ya jiji ndiyo iliyopimwa.

Alisema Jiji la Dar es Salaam, haliwezi kuendelea kupanuka bila mpangilio na kwamba wakati sasa umefika wa kuhakikisha kuwa linajengwa kwa kuzingatia mipango miji.

"Hatuwezi kuendelea namna hii na mji unaopanuka namna hii. Hili ni jambo zito, kubwa linalohitaji umakini wa haraka kutatuliwa. Ndio maana kipindupindu hakiishi katika mji huu." alisema Rais Kikwete baada ya kupata taarifa kutoka kwa watalaam wa huduma za maji, ardhi na barabara.

Katika mkutano huo, Rais Kikwete pia alipewa taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ukosefu wa maji ya katika jiji hilo.

Rais Kikwete pia aliusifu utendaji wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam akiwataka viongozi wa chama hicho kutafuta njia za haraka za kutatua matatizo ya wananchi.

"Angalieni na chunguzeni sana matatizo ya wananchi. Haya ndiyo muhimu kwetu kuyashughulikia, tena kwa haraka. Hii ndiyo nguvu ya chama chetu," amesema Mwenyekiti huyo wa CCM


Source: MWANANCHI

My take:
Swala la mpangilio wa mji wa DAR linatia hadi hasira, sijui walikuwa wapi muda wote huo. Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa?

Unaweza kukuta wengine hata wamepanga Manzese na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? Isije ikawa kama ile ya maisha bora.
 
Hivi huyu mzee anafikiriaga kweli maagizo anayoyatoa au anapauka tu? Madawati kununua yanawashinda anawaza flyovers?
 
Rais na mwenyekiti wa ccm ameagiza barabara za juu zijengwe kwenye jiji la DAR kwa sababu ndani ya miaka 3 barabara zilizopo zitakuwa hazipitiki.Pia amewaagiza mipango miji waanze kuliweka jiji kwenye ramani :
source:
MWANANCHI.
My take:
swala la mpangilio wa mji wa DAR linatia hadi hasira, sijui walikuwa wapi mda wote huo. Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa? unaweza kukuta wengine hata wamepanga manzese,na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? isije ikawa kama ile ya maisha bora.
Hivi ni baada ya miaka mitatu ndio zitakuwa hazipitiki, au ni tangu miaka zaidi ya mitatu ya nyuma?

Au kwa vile yeye anapita kwenye njia iliyosafishwa kila atokapo!

Wataahidi sana hawa safari hii, yetu macho.
 
Uchaguzi unakuja....miaka minne yote alikua wapi kuzijenga hizo barabara za juu...wanatafuta ahadi mpya.
wakati wauchaguzi mkuu mwaka 2005 walikua na ahadi kuwa kufikia 2009 kutakua na usafiri wa mabasi yaendayo kasi DSM, SASA WAMESHINDWA WANAKUJA NA KELELE MPYA, tunataka vitendo, Kikwete tumechoka na maneno maneno yako.
 
Yaani JK kwa sasa namfananisha na goalkeeper ambaye beki zake hazikabi sasa anahangaika tu mipira inavogonga besela....hahaaaaaa
 
Kweli wazee mabasi yaendayo kasi yameyeyuka, ahadi gani inachukua karne? Then anajaribu kutoka na single nyingine tena sahivi.
 
Wameshindwa kujenga shule za matofali watoto wanasomea shule zilizoezekwa kwa nyasi sasa wanaota flyovers bado tunasafari ndefu na hiki chama za zidumu fikra za mwenyekiti wa chama.
 
kweli wazee mabasi yaendayo kasi yameyeyuka .ahadi gani inachukua karne?,then anajaribu kutoka na single nyingine tena sa ivi.
Napata sana shida kumuelewa Kikwete, naonaga uvivu kumsikiliza na waliomsikiliza mkiniambia aliyoyasema nafadhaika sana......anaanza kuleta ngonjera hizo, yeye ni mtendaji mkuu awaachie wanataarabu kina Tabwe Hiza watuburudishe na nyimbo za kipropaganda....yeye awe mtendaji....Kikwete na watu wako ya wapi mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam kabla hamjakuja na mradi hewa mwingine.
 
Mmmh, mwaka huu tutasikia mengi na mengine yasiyo na kichwa wala miguu, mwenyekiti wa taifa yake wanachama nao hoi kwa umaskini unawaambia habari ya flyovers, Makamba nae ni zaidi ya hoi!!! Hizo flyovers wamwambie Chenge na Lowassa ambao ni wajumbe wa kamati kuu wazijenge wenyewe kwa vijisenti vyao!
 
Kwanza baadhi ya barabara ambazo huo mradi ungetakiwa upite zishaanza kuharibika aka Kilwa road.
 
kwanza baadhi ya barabara ambazo huo mradi ungetakiwa upite zishaanza kuharibika aka kilwa road.
Sasa nilikoma kuringa nilipoambiwa wanataka eti kupanua barabara za Posta mpya na mnazi mmoja ili kuruhusu magari hayo kupita...nilihisi ni ulongo usio kifani, sasa kama unavyosema, tukajengewa KILWA RD kwakiwango cha chini kuliko, waziri wa miundombinu sijui Kawambwa sijui nani ni kama hayupo, aaah Kikwete bana, unaniboaga basi tu.
 
OK. WAKUU TUSHAANZA KUSIKIA NGONJERA,NA TUKIENDELEA KUBLAME HUMU HAKUNA FAIDA YOYOTE.SASA INABIDI TUJE NA SOLUTION: JF NI KUBWA NA PANA HATA IKULU WATAKUWA WANAISOMA HIO NI KWELI KABISA.SASA BASI WE COME WITH SOLUTION INSTEAD OF BLAMMING.piriodi.
 
sasa nilikoma kulinga nilipoambiwa wanataka eti kupanua barabara za posta mpya na mnazi mmoja ili kuruhusu magari hayo kupita...nilihisi ni ulongo usio kifani, sasa kama unavyosema, tukajengewa kilwa rd. Kwakiwango cha chini kuliko , waziri wa miundo mbinu sijui kawambwa sijui nani ni kama hayupo, aaah kikwete bana, unaniboaga basi tu.

Kote huko ni watu wanataka kula tu. Utakuta hata kwenye kugawa ile tenda kulikuwa na utata.
 
kote huko ni watu wanataka kula tu. Utakuta hata kwenye kugawa ile tenda kulikuwa na utata.
Utata utakosekana vipi, kama wajanja walitaka kukomba hadi mradi wa vitambulisho vya Taifa.... nchi bana, uongo mwingi, wizi mwingi, umbea umbea mwingi...na Mtawala nae anaingia kwenye mkumbo huo, mimi kwakweli simfagilii.....
 
Rais na mwenyekiti wa ccm ameagiza barabara za juu zijengwe kwenye jiji la DAR kwa sababu ndani ya miaka 3 barabara zilizopo zitakuwa hazipitiki.

Kamuagiza nani!?

Hivi anaelewa hata 'feasibility study' ya hii kazi inachukua muda gani?

Majuzi hapa wamesema wapo njiani kuleta train ziendazo kasi ya ajabu (kupitia kwenye reli ile ile ya mjerumani!!?)

Hivi uchaguzi mkuu ni mwezi wa ngapi vile!!?

Nadhani imefika muda sasa tusiwe na president mwanasiasa
 
Hivi April 1 ishafika tayari? Are you guys on some type of Klingon calendar?

Huyu Kikwete anasema hivyo kwa ushauri wa wataalam au yeye kashakuwa Engineer in Chief siku hizi?
 
Rais na mwenyekiti wa ccm ameagiza barabara za juu zijengwe kwenye jiji la DAR kwa sababu ndani ya miaka 3 barabara zilizopo zitakuwa hazipitiki.Pia amewaagiza mipango miji waanze kuliweka jiji kwenye ramani :
source:
MWANANCHI.
My take:
swala la mpangilio wa mji wa DAR linatia hadi hasira, sijui walikuwa wapi mda wote huo. Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa? unaweza kukuta wengine hata wamepanga manzese,na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? isije ikawa kama ile ya maisha bora.

Hamna kitu kaka...mbio za Oktoba 2010 zimeshaanza..
 
Mimi mwenyewe nimeshtuka sana nilivyosikia hivyo lakini sikushangaa kwani huyu kiongozi wetu ni mtu wa kutamka mambo sana bila kuyafikiria. Manake vitu vingine hauhitaji kuambiwa kuwa ni bla blaa, juzi juzi tu wamezungumzia train ziendazo kasi leo hii fly-overs tena mh? Hiri rinchi sasa!!
 
Kamuagiza nani!?

Hivi anaelewa hata 'feasibility study' ya hii kazi inachukua muda gani?

Majuzi hapa wamesema wapo njiani kuleta train ziendazo kasi ya ajabu (kupitia kwenye reli ile ile ya mjerumani!!?)

Hivi uchaguzi mkuu ni mwezi wa ngapi vile!!?

Nadhani imefika muda sasa tusiwe na president mwanasiasa

Nani atakubali kumpika? Uchaguzi ndio huo na mkulu hadi sasa anaongoza tatu bila winga na mfungaji akiwa mnajimu wetu. Makamba beki la kupanda na kushuka. Mrema D:D:D:???
 
Back
Top Bottom