Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Date::6/2/2010
Mwandishi Maalumu
RAIS Jakaya Kikwete, ameagiza hatua za haraka zichukuliwe, kujenga barabara zinazopita juu katika Jiji la Dar es Salaam, ili kupunguza misongamano mikubwa ya magari.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM alitoa agizo hilo juzi, baada ya kupewa taarifa ya utendaji ya CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu ya kukagua shughuli za CCM mkoani humo.
"Hili la flyovers lipewa kipaumbele ili tupunguze msongamano wa magari katika Dar es salaam. Tusipofanya hili jiji hili litakuwa halipitiki katika muda wa miaka mitano, ama hata katika miaka miwili ama mitatu ijayo," Rais Kikwete.
Rais Kikwetepia aliwaagiza wataalam wa mipango miji katika Jiji la Dar es Salaam, kuanza kupunguza maeneo yasiyopimwa kwa kuzingatia kuwa kwa sasa ni asilimia 30 ya jiji ndiyo iliyopimwa.
Alisema Jiji la Dar es Salaam, haliwezi kuendelea kupanuka bila mpangilio na kwamba wakati sasa umefika wa kuhakikisha kuwa linajengwa kwa kuzingatia mipango miji.
"Hatuwezi kuendelea namna hii na mji unaopanuka namna hii. Hili ni jambo zito, kubwa linalohitaji umakini wa haraka kutatuliwa. Ndio maana kipindupindu hakiishi katika mji huu." alisema Rais Kikwete baada ya kupata taarifa kutoka kwa watalaam wa huduma za maji, ardhi na barabara.
Katika mkutano huo, Rais Kikwete pia alipewa taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ukosefu wa maji ya katika jiji hilo.
Rais Kikwete pia aliusifu utendaji wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam akiwataka viongozi wa chama hicho kutafuta njia za haraka za kutatua matatizo ya wananchi.
"Angalieni na chunguzeni sana matatizo ya wananchi. Haya ndiyo muhimu kwetu kuyashughulikia, tena kwa haraka. Hii ndiyo nguvu ya chama chetu," amesema Mwenyekiti huyo wa CCM
Source: MWANANCHI
My take:
Swala la mpangilio wa mji wa DAR linatia hadi hasira, sijui walikuwa wapi muda wote huo. Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa?
Unaweza kukuta wengine hata wamepanga Manzese na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? Isije ikawa kama ile ya maisha bora.