Rais Kibaki amsimamisha Naibu Jaji Mkuu, Nancy Baraza Amteua Mtz Jaji A. Ramadhan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kibaki amsimamisha Naibu Jaji Mkuu, Nancy Baraza Amteua Mtz Jaji A. Ramadhan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jason Bourne, Jan 26, 2012.

 1. Jason Bourne

  Jason Bourne Senior Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  25/01/2012

  *

  Rais wa Kenya, Mwai Kibaki amemsimamisha kazi Naibu Jaji mkuu bi. Nancy*Baraza na*kuunda jopo ambalo litaufanyia uchunguzi mwenendo wake kutokana na shutuma zinazomkabili.

  Jaji*Baraza, anashutumiwa kumtishia maisha kwa bastola mlinzi wa duka moja kubwa, Bi Rebecca Kerubo wakati wa sikuya mkesha wa mwaka mpya, pale Rebecca alipomwendea na kutaka arudi ili amkague kufuatia utaratibu wa duka hilo ulilokuwa ukikagua kila mtu aliyeingia ndani ikiwa ni hatua za kujlinda dhidi ya hatari ya mashambulizi ya Al-Shaabab.

  Inasemekana Bi. Baraza alichukizwa na kitendo hicho na kukiona kama kudhalilishwa na ndipo aliposhikwa na ghadhabu na kumwambia bi Rebecca kuwa anapaswa kuwafahamu baadhi ya watu mashuhuri nchini humo, huku akimfinya pua na kumsukuma.*

  Kama vile dhihaka hiyo haitoshi, inaripotiwa kuwa Bi. Baraza alitoka nje na kuendeleza vitisho na maneno dhidi ya Rebecca kiasi cha kusema angeweza kumwua na hata kuthubutu kumwamuru mmoja wa mlinzi wake ampige risasi lakini mlinzi huyo hakufanya hivyo. Ndipo inaposimuliwa kuwa Naibu Jaji *huyo alitoa bastola na kuielekeza tumboni mwa bi. Rebecca ambapo alisema angeweza kuifyatua.*

  Alipohojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo, kwenye video Rebecca anasema kitendo alichofanyiwa kilimstua na kusababisha kuhofia uhai na maisha yake.

  Jopo la wachunguzi hao litaongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhan kama Mwenyekiti.

  Wajumbe wengine ni Profesa Judith Behemuka, Philip Ransley, Surinder Kapila, Beuttah Siganga, Grace Madoka na Prof Mugambi Kanyua.

  Katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ikulu ya Nairobi, Rais Kibaki alisema wakati wa uchunguzi, Bi*Baraza hatoendelea na majukumu yake ya idara ya mahakama.

  "Kwa wakati huu, Mheshimiwa Jaji Nancy Makokha*Baraza, Naibu Jaji Mkuu, Mahakama ya juu ya Kenya amesimamishwa kazi mara moja kwa mujibu wa kifungu 168(5) cha katiba." Alisema rais Kibaki.

  Katika muda huo atakaokuwa amesimamishwa kazi, Jaji*Baraza, atakuwa anapata nusu mshahara hadi pale uchunguzi utakapokamilika na kufahamika kupitia mapendekezo ya jopo kama atarejeshwa kazini au atimuliwe.

  Kuundwa kwa jopo kumetokana na mapendekezo yaliyowasilishwa kwa rais Kibaki na tume inayoshughulika na masuala ya idara ya mahakama iliopendekeza*Baraza*asimamishwe kazi na uchunguzi juu ya mwenendo wake ufanywe.
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Good, hapa hakuna kulindana
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,508
  Trophy Points: 280
  Ndiyo adhaa ya wamama kuwa na vyeo vikubwa,
  wanaona kama kila kitu wanakiweza wao.
   
 4. H

  House1932-1951 Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni hatua nzuri katika usawa kati ya tabaka tawala na tawaliwa,kibaki vipi kuhusu Uhuru na Ruto kwa mjibu wa ibara ya 60 ya katiba mpya ulipaswa kuwasimamisha kwa kuwa wameshusha hadhi ya ofisi zao,acha uoga Mh.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Jaji Augustino Ramadhan wa Tanzania anahusikaje na utendaji kazi wa public figure Kenya?
   
 6. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,802
  Likes Received: 2,575
  Trophy Points: 280
  Matunda ya katiba mpya baba.
   
 7. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Mkuu Kuchunguza tuhuma c lazima uwe mtu wa eneo au nchi husika, ni kama kina Ocampo, Interpol nk tena ndio poa zaidi kwa vile hakuna kulindana hapo! Wakenya wenyewe wako corrupt na ukabila mno pengine ndio mana Jaji Ramadhani kawekwa hapo kudhibiti upendeleo au uonezi.
   
 8. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,721
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  ungekuwa umesoma sheria ungekutana na somo linaitwa legal method humo ndani kuna kitu kinaitwa tenure of jugdes hapo ungejua utaratibu mzima unaotumika kumvua mtu u judge.
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280

  Kweli Wakenya hamnazo unamfinya pua mwezio kisa wewe ni mtu maarufu..khaaa!
   
Loading...