Rais Kenyatta atoa onyo kwa Somalia, ataka nchi hiyo kuacha kuichokoza Kenya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1583391168960.png

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameionya serikali ya Somalia kuacha uchokozi wa mara kwa mara dhidi ya Kenya.

Onyo lake linajiri siku moja baada ya wakazi wa Mandera kulazimishwa kutoroka makazi yao baada ya ghasia zilizozuka kati ya wanajeshi wa Somalia dhidi ya wanajeshi wa eneo la Jubaland katika eneo la Bulla Hawa

Ufyatulianaji mkali wa risasi na milipuko ilionekana kutoka katika eneo hilo la Bulla hawa nchini Somali linalopakana na mji wa Mandera.

''Wanajeshi wa kigeni waliokiuka sheria na kupuuza kabisa sheria za kimataifa na maazimio yalioafikiwa walitekeleza vitendo vya uchokozi na ukatili kwa kuwanyanyasa na kuharibu mali za raia wa Kenya wanaoishi katika mji wa mpakani wa Mandera'' , alisema Uhuru Kenyatta.

''Wacheni uchokozi wa mara kwa mara na badala yake angazieni mambo yenu ya ndani''.

Uhuru amesema kwamba taifa la Somalia linapaswa kuangazia maswala ya raia wake kwa kukabiliana na kuushinda ugaidi ili kuweka amani, usalama na udhibiti katika eneo zima la Afrika mashariki.

"Tuhuma za kila mara zisizo na msingi zinazotolewa na Somalia kwamba Kenya inaingilia mambo yake ya ndani ni mbinu ya Somalia kutaka kuitumia Kenya kama kisingizio '', alisema.

Akiongezea kwamba : Kenya haitakubali kutumika kama sababu ya changamoto zinazoikumba Somalia kisiasa.

Kiongozi huyo ametoa wito kwa Somalia kuacha kampeni hiyo chafu dhidi ya Kenya na badala yake kupeleka nguvu yake katika kutoa uongozi bora kwa watu wake.

Alisema kwamba Kenya imelazimika kuathirika pakubwa kutokana na hatua yake ya kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuweka amani na usalama katika nchi jirani ya Somalia.

Kiongozi huyo pia amesema kwamba Kenya sasa inaunga mkono wito unaotolewa na Umoja wa Mataifa na washirika wengine wa kieneo na kimataifa wanaoitaka Somalia kutafuta makubaliano mapana ya kisiasa.

Joto la wasiwasi kati ya Nairobi na Mogadishu limeongezeka katika siku za hivi karibuni huku pande zote mbili zikitoa matamko makali ya kulaumiana kwa kuingia katika himaya ya taifa jingine.

Uhusiano kati ya Mogadishu na Jubaland ni tete

Mapigano hayo ya Somalia ni kisa cha hivi karibuni cha wasiwasi kati ya Mogadishu na serikali zake za kijimbo.

Mamlaka ya Jubaland mnamo mwezi Agosti iliishutumu Mogadishu kwa kuingilia uchaguzi wake na kutaka kumpindua madarakani rais wake Ahmed Madobe ili kuweza kujipatia uwezo wa kulidhibiti jimbo hilo.

Madobe ambaye alichaguliwa kwa muhula mwengine ni mshirika mkubwa wa Kenya ambayo inaiona serikali ya Jubaland kama kizuizi kikuu dhidi ya wapiganaji wa Alshabab ambao wametekeleza mashambulizi chungu nzima nchini Kenya.

Waziri wa ulinzi wa eneo la Jubaland Abdirashid Janan alikamatwa mjini Mogadishu mwezi Agosti mwaka jana akiwa njiani kuelekea Addis Ababa kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamu. Alikuwa amehudumu miezi mitano jela kabla ya kutoroka katika mazingira ya kutatanisha mapema mwaka huu.

Tangu Bw Janan alipowasili Kenya, hali ya taharuki mjini Mandera imekuwa ikitanda na kuwalazimu baadhi ya wakazi kuyakimbia makazi yao wakihofia mapigano kuzuka.

Habari za kuwepo kwa Bwana Janan nchini Kenya zimezidisha uhasama wa kidiplomasia kati ya Mogadishu na Nairobi.

Waziri huyo amekuwa akijificha katika hoteli moja mjini Mandera tangu Januari 30 baada ya kukwepa kutoka jela alikokuwa akizuiliwa na serikali ya Somalia tangu Agosti 31, 2019.

Hofu kati ya mataifa hayo mawili pia iko juu kutokana na madai ya umiliki wa eneo moja lililo katika mpaka wake wa bahari hindi linalodaiwa kuwa na gesi pamoja na mafuta mengi.

Mwezi uliopita serikali ya Kenya ilipuuzilia mbali taarifa ya waziri wa maswala ya kigeni wa Somalia kwamba Kenya ilikuwa inaingilia maswala ya ya ndani ya Somalia.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba huenda hatua ya Kenya ya kumlinda waziri wa ulinzi wa eneo la Jubaland Abdirashid Janan huenda ikachochea uhasama zaidi wa kidiplomasia kati ya mataifa haya mawili na kulemaza vita dhidi ya wanamgambo wa Al-shabaab.

Mchambuzi wa maswala ya kiusalama George Musamali anasema huenda utawala wa rais Farmajo ukasitisha ushirikiano wake na Kenya katika mikakati ya kupambana na wapiganaji wa Al-shabaab.

Inaaminika pia kwamba viongozi wengi wa Kaskazini mwa Kenya, wakiwemo wale wabunge waliokutana na Rais Farmajo, hawaungi mkono hatua ya serikali ya Kenya ya kumhifadhi na kumlinda Bwana Janan.
 
Kenya hamuwawezi Somalia just shut up Ur mouth before they shut it up for you
:D:D:D Hebu kuwa serious na uweke hisia zako za kijihadi kando kwa dakika moja. Yaani serikali ambayo ililemewa na vikundi haramu hadi ikasambaratika ndio itakuwa tishio kwa Kenya? Mwaka wa 2011 rais wao aliungana na wananchi kujivinjari na kujirusha rusha kwenye fukwe za mji wa Mogadishu kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka mitatu!
Baada ya vikosi vya kijeshi vya UG, Kenya na ET kuwafurusha magaidi ambao walikuwa wameitesa serikali na wananchi kwa muda mrefu. Hata sasa hivi rais wa sasa Farmajo hawezi akatia mguu wake nje ya ikulu ya Villa Somaaliya bila ulinzi wa vikosi vya AMISOM, la sivyo magaidi wa alshabaab lazima watapita na shingo lake. Somalis hit the beach in Mogadishu for first time in three years - The Mail & Guardian[/
 
Nadhani diplomasia ya kenyatta ndio inafanya huu mgogoro kuwa simple hawa somalia wangepata jirani kama PK sijui ingekuwaje
Diplomasia na strategy zinazoeleka ndio huwa za maana zaidi ya ubabe. Alafu kuna dynamics za kiukoo(qabil kwa kisomali) na historia kati ya wasomalia kutoka Somalia na wazawa wa Kenya. Ndio maana inambidi rais UK awe makini, ukizingatia kwa mara ya kwanza tangia uhuru serikali ya Kenya imewajumuisha wasomali wa Kenya kwenye uongozi wa nchi. Somalia tulipigana nao kwa miaka 6, kwenye vita ambavyo vilikuwa vinaitwa Shifta Wars(1963-1969). Kabla ya Kenya kufanikiwa kuzima ndoto yao ya kutupokonya NFD. Serikali kuu ya Somalia na PM wao enzi hizo kwa usaidizi na Russia waliwapa mafunzo ya kijeshi maelfu ya wasomali(mashifta) ambao walivuka boda kupigana na GOK kule NFD. Vita ambavyo viliwaangamiza wasomali zaidi ya 10,000. Kenya’s first secessionist war : The Standard
 
Acha Kenyatta awe mpole tu maana anajua vita sio mchezo
Hongera sana maana Ksh itakuwa kama ya Zim

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
All in all hakuna namna zaidi ya KDF kuondoka somalia alafu naona kama AU imewachekea saana kwa mlichokifanya cha kuigawa somalia
Diplomasia na strategy zinazoeleka ndio huwa za maana zaidi ya ubabe. Alafu kuna dynamics za kiukoo(qabil kwa kisomali) na historia kati ya wasomalia kutoka Somalia na wazawa wa Kenya. Ndio maana inambidi rais UK awe makini, ukizingatia kwa mara ya kwanza tangia uhuru serikali ya Kenya imewajumuisha wasomali wa Kenya kwenye uongozi wa nchi. Somalia tulipigana nao kwa miaka 6, kwenye vita ambavyo vilikuwa vinaitwa Shifta Wars(1963-1969). Kabla ya Kenya kufanikiwa kuzima ndoto yao ya kutupokonya NFD. Serikali kuu ya Somalia na PM wao enzi hizo kwa usaidizi na Russia waliwapa mafunzo ya kijeshi maelfu ya wasomali(mashifta) ambao walivuka boda kupigana na GOK kule NFD. Vita ambavyo viliwaangamiza wasomali zaidi ya 10,000. Kenya’s first secessionist war : The Standard

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ni ukweli msiotaka kuukubali, Farmajo anajivunia uungwaji mkono na Ethiopia, anajua kabisa kwamba Kenya haina uwezo wa kupigana na Ethiopia ndio sababu anaichokoza Kenya bila woga wowote ule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inakuaje Rais was Somalia amempigia Rais wa Kenya kuomba msamaha?

Google Translation
Mr. President JFS@M_Family and Kenyan President Uhuru Kenyatta over the telephone line discussed the importance of working jointly between the two countries in maintaining border security and overall regional stability.
 
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameionya serikali ya Somalia kuacha uchokozi wa mara kwa mara dhidi ya Kenya.

Onyo lake linajiri siku moja baada ya wakazi wa Mandera kulazimishwa kutoroka makazi yao baada ya ghasia zilizozuka kati ya wanajeshi wa Somalia dhidi ya wanajeshi wa eneo la Jubaland katika eneo la Bulla Hawa

Ufyatulianaji mkali wa risasi na milipuko ilionekana kutoka katika eneo hilo la Bulla hawa nchini Somali linalopakana na mji wa Mandera.

''Wanajeshi wa kigeni waliokiuka sheria na kupuuza kabisa sheria za kimataifa na maazimio yalioafikiwa walitekeleza vitendo vya uchokozi na ukatili kwa kuwanyanyasa na kuharibu mali za raia wa Kenya wanaoishi katika mji wa mpakani wa Mandera'' , alisema Uhuru Kenyatta.

''Wacheni uchokozi wa mara kwa mara na badala yake angazieni mambo yenu ya ndani''.

Uhuru amesema kwamba taifa la Somalia linapaswa kuangazia maswala ya raia wake kwa kukabiliana na kuushinda ugaidi ili kuweka amani, usalama na udhibiti katika eneo zima la Afrika mashariki.

"Tuhuma za kila mara zisizo na msingi zinazotolewa na Somalia kwamba Kenya inaingilia mambo yake ya ndani ni mbinu ya Somalia kutaka kuitumia Kenya kama kisingizio '', alisema.

Akiongezea kwamba : Kenya haitakubali kutumika kama sababu ya changamoto zinazoikumba Somalia kisiasa.

Kiongozi huyo ametoa wito kwa Somalia kuacha kampeni hiyo chafu dhidi ya Kenya na badala yake kupeleka nguvu yake katika kutoa uongozi bora kwa watu wake.

Alisema kwamba Kenya imelazimika kuathirika pakubwa kutokana na hatua yake ya kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuweka amani na usalama katika nchi jirani ya Somalia.

Kiongozi huyo pia amesema kwamba Kenya sasa inaunga mkono wito unaotolewa na Umoja wa Mataifa na washirika wengine wa kieneo na kimataifa wanaoitaka Somalia kutafuta makubaliano mapana ya kisiasa.

Joto la wasiwasi kati ya Nairobi na Mogadishu limeongezeka katika siku za hivi karibuni huku pande zote mbili zikitoa matamko makali ya kulaumiana kwa kuingia katika himaya ya taifa jingine.

Uhusiano kati ya Mogadishu na Jubaland ni tete

Mapigano hayo ya Somalia ni kisa cha hivi karibuni cha wasiwasi kati ya Mogadishu na serikali zake za kijimbo.

Mamlaka ya Jubaland mnamo mwezi Agosti iliishutumu Mogadishu kwa kuingilia uchaguzi wake na kutaka kumpindua madarakani rais wake Ahmed Madobe ili kuweza kujipatia uwezo wa kulidhibiti jimbo hilo.

Madobe ambaye alichaguliwa kwa muhula mwengine ni mshirika mkubwa wa Kenya ambayo inaiona serikali ya Jubaland kama kizuizi kikuu dhidi ya wapiganaji wa Alshabab ambao wametekeleza mashambulizi chungu nzima nchini Kenya.

Waziri wa ulinzi wa eneo la Jubaland Abdirashid Janan alikamatwa mjini Mogadishu mwezi Agosti mwaka jana akiwa njiani kuelekea Addis Ababa kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamu. Alikuwa amehudumu miezi mitano jela kabla ya kutoroka katika mazingira ya kutatanisha mapema mwaka huu.

Tangu Bw Janan alipowasili Kenya, hali ya taharuki mjini Mandera imekuwa ikitanda na kuwalazimu baadhi ya wakazi kuyakimbia makazi yao wakihofia mapigano kuzuka.

Habari za kuwepo kwa Bwana Janan nchini Kenya zimezidisha uhasama wa kidiplomasia kati ya Mogadishu na Nairobi.

Waziri huyo amekuwa akijificha katika hoteli moja mjini Mandera tangu Januari 30 baada ya kukwepa kutoka jela alikokuwa akizuiliwa na serikali ya Somalia tangu Agosti 31, 2019.

Hofu kati ya mataifa hayo mawili pia iko juu kutokana na madai ya umiliki wa eneo moja lililo katika mpaka wake wa bahari hindi linalodaiwa kuwa na gesi pamoja na mafuta mengi.

Mwezi uliopita serikali ya Kenya ilipuuzilia mbali taarifa ya waziri wa maswala ya kigeni wa Somalia kwamba Kenya ilikuwa inaingilia maswala ya ya ndani ya Somalia.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba huenda hatua ya Kenya ya kumlinda waziri wa ulinzi wa eneo la Jubaland Abdirashid Janan huenda ikachochea uhasama zaidi wa kidiplomasia kati ya mataifa haya mawili na kulemaza vita dhidi ya wanamgambo wa Al-shabaab.

Mchambuzi wa maswala ya kiusalama George Musamali anasema huenda utawala wa rais Farmajo ukasitisha ushirikiano wake na Kenya katika mikakati ya kupambana na wapiganaji wa Al-shabaab.

Inaaminika pia kwamba viongozi wengi wa Kaskazini mwa Kenya, wakiwemo wale wabunge waliokutana na Rais Farmajo, hawaungi mkono hatua ya serikali ya Kenya ya kumhifadhi na kumlinda Bwana Janan.
Aache unafiki kuingilia mumbo ya ndani ya nchi ya Somalia ndo kunasababisha haya kuanzia ku-support Jubaland na pia kuiba Territory ya Somalia Indian Ocean. Mkianza vita na Somalia ndo mwisho wenu maana Wabunge wote wa North eastern wanaiunga mkono Somalia including Duale! Don't be surprised the whole Arab world throw a support behind Somalia! Uliza kilichoitokea Ethiopia walipokuwa wakipigana na Eritrea!

CC: Zigi Rizla Kafrican Depay Teargass Tony254 pingli-nywee komora096
 
Back
Top Bottom