Rais Kenyatta afanya mabadiliko katika baraza la mawaziri

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
BALOZI Amina Mohamed ndiye Waziri mpya wa michezo wa Kenya baada ya Rashid Echesa kupigwa kalamu Machi 1, 2019.

Echesa ameangukiwa na shoka katika teuzi za serikali zilizofanywa na Ikulu ya Rais, Ijumaa. Amina, 57, alihudumu katika Wizara ya Masuala ya Kigeni kutoka Aprili 23, 2013 hadi Januari 26, 2018, alipohamishiwa Wizara ya Elimu kabla ya kuteuliwa Ijumaa kuongoza Wizara ya Michezo.

Echesa aliteuliwa kuongoza Wizara ya Michezo mnamo Januari 26, 2018 akisubiri kuhojiwa kabla ya uteuzi huo kuidhinishwa Februari 12 mwaka 2018. Ripoti wakati huo zilienea kwamba Echesa atetemwa.

Hata hivyo, alifaulu kujaza nafasi ya Dkt Hassan Wario. Naibu Rais William Ruto alilazimika kutetea uteuzi wa Echesa alipokuwa na sherehe ya kurejea nyumbani katika eneo bunge la Mumias mnamo Machi 13, 2018.

Echesa alihudumu kama waziri kwa mwaka mmoja kabla ya kutemwa Machi 1, 2019.

Sababu kuu ya Echesa kutaka kutemwa Februari 2018 ilikuwa kutokana na kiwango chake cha chini cha masomo.

“Echesa aliacha kusoma katika darasa la saba,” vyombo vya habari viliripoti Februari 12.

Taifaleo
 
Hii Amina naona ni Chakula ya Mkubwa fulani.😁😁😁😁😁
 
Vita vidi ya ufisadi. Mabadiliko zaidi baada watuhumiwa kuchunguzwa. Hadi mawaziri /CS watano wanatuhumiwa kesi zaidi ufisadi.
 
“If you read the report on the maize crisis in the Senate, keenly analyse the dam scandal, and if you look at other scandals that relate to waste of public resources and embezzlement, all the roads seem to lead towards one headquarters,” Siaya senator J.Orengo.:oops:
 
Dah Umetisha mkuu ila
Nahisi tu Kama ana mume na watoto sijui wanajisikiaje huko walipo
Skiiza Mbunye ni yako pale tu uko ndani yake lakini ikitoka glass Mbili za Finest French wine sio yako tena..ingia kwa siasa utaona mengi.
 
Hii Amina naona ni Chakula ya Mkubwa fulani.
Huu udhalilishaji wa dada zetu huwa nauona sanasana na wanigeria. Kwa akili zao huwa wanajua kwamba hakuna mwanamke yeyote ambaye anaweza akifanikiwa kwenye nyanja yeyote ile bila ya kupanua mapaja. Umeona C.V. ya ambassador Amina Mohammed wewe?
 
Back
Top Bottom