Rais Karume Unadanganywa, Wananchi,Waandishi Wa Habari Si Vipofu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Karume Unadanganywa, Wananchi,Waandishi Wa Habari Si Vipofu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Sep 30, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  RAIS wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amani Abeid Karume amesema hali ni shuwari Zanzibar na kuwataka wanasiasa katika Kisiwa cha Pemba kupingana kwa hoja na wale wasioweza kujenga hoja waondoke katika ulingo wa siasa.
  Hayo ameyaeleza wakati akizungumza katika uzinduzi wa shule ya msingi ya Wingwi Mtemani katika Mkoa wa Kaskazini Pemba jana ambapo alisema kwamba kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kutumia jukwaa la kisiasa kwa kueleza mambo ya vitisho kutokana na kushindwa kujenga hoja za maana.
  “Tupingane bila kupigana kwa maana tukipingana kwa hoja ndio demokrasia kama hoja zimeisha wewe tulia tu katafute mhogo na samaki wako wa tasi ule sio kuleta vitisho” alionya Rais Karume.
  Alisema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya amani na utulivu tokea miaka ya chuma hivyo mtindo uliojitokeza katika siku za karibuni wa kuchoma moto nyumba hauna maslahi kwa wananchi na badala yake aliwataka wanasiasa waliofilisika kufunga virago na kutafuta shughuli ya kufanya.
  “Zanzibar kuna amani tena utulivu wa kutosha wau wanafanya shughuli zao za kawaida na tunawalika wengine pia waje kutembelea visiwa hivi na wachane na wale watu wanaosema kuwa Zanzibar hakukaliki” alisema Rais Karume.
  Kaika hatua nyengine Rais Karume alivitaka vyombo vya habari hasa vya nje ya Zanzibar kuacha kuandika mambo ya uchochezi dhidi ya Zanzibar na badala yake vifanye kazi kwa mujibu wa maadili na taaluma ya habari.
  Rais karume alisema kwamba katika siku za hivi karibuni habari nyingi zinazoandikwa kuhusu Zanzibar zimekuwa zikitiwa chumvi huku zikipambwa kwa vichwa cha habari mbali mbali kwa lengo la kuuza magazeti ikiwemo zile za “Zanzibar kwawaka moto, nyumba zachomwa Zanzibar na mambo mengine” na kusisitiza kuwa jukumu kubwa la vyombo vya habari ni kutoa elimu kwa kujenga jamii bora na sio kuchochea mifarakano.
  Aidha aliwaonya wanafunzi kuacha kujiingiza katika mambo ya siasa kwani kwa kufanya hivyo wanaweza wakakubwa na matatizo mbali mbali ikiwemo ya kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwa watawasikiliza wanasiasa waliofilisika ambao wamekuwa wakiwaotosha.
  Aliwataka wanafunzi hao kukataa kutumiwa na wanasiasa kwa kufanya udanganyifu kwenye vyeti vya kuzaliwa ili wajipatie vitambulisho vya mzanzibari mkaazi wanaweza wakajikuta wanaishia mahakamani na wanasiasa hawatawasaidia kitu zaidi ya kuwakimbia.
  Aliwahimiza wenye sifa za kusajiliwa kupatiwa vitambulisho vya mzanzibari wende katika afisi za idara hiyo kwani kufanya hivyo watakuwa wanatetea haki yao lakini aliwakumbusha kuwa serikali haitawavumilia wale watakaofanya udanganyifu.
  Wakati Rais Karume akitoa tahadhari hiyo tayari mwanafunzi mmoja wa kidatu cha tatu katika shule ya sekondari Kisiwani Pemba amemaliza kutumikia kifungo cha wiki mbili jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya udanganyifu wa cheti cha kuzaliwa katika wilaya ya wete mkoa wa kaskazini Pemba.
  Ziara ya Rais Karume ni ya siku moja ya kufungua shule hiyo ya wingwi iliyoanza na wanafunzi 890 ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na michango kutoka kwa wadau mbali mbali ikiwemo serikali ya mapinduzi Zanzibar.
  Awali akimkaribisha Rais Karume Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman alisema kwamba serikali itaendelea na juhudi za ujenzi wa shule karibu na makaazi ya wananchi.
  Waziri Haroun nae aliwaasa wanafunzi kuzingaia masomo na kuachana na vitendo vya kujihusisha katika mambo ya kisiasa sambamba na kutoa onyo kali kwa walimu kwamba serikali haitawavumilia watakaochanganya kazi na siasa.
  Alisema kuna taarifa kwamba wapo baadhi ya walimu wanajishirikisha na siasa na hivyo kuwataka waachane na tabia hiyo kwani kufnaya hivyo kunaweza kuwasababishai matatizo katika kazi zao.
  “Nimepata taarifa kuwa wapo baadhi ya walimu wanajiingiza katika siasa lakini mimi nawaambia waache mambo hayo maana nasikia mwalimu mmoja ameshiriki kupiga watu mawe nasema isije ikawa kama mwaka 1995 nasema msiturudhise nyuma” alisema Waziri huyo.
  Alisema mwaka 1995 walimu wengi wlaifukuzwa kazi baada ya kudhaniwa wanajiingiza katika siasa lakini katika awamu hii ya Rais Karume hakuna mwalimu haa mmoja aliyefukuzwa kazi hivyo aliwataka kuachan ana kujishirikisha katika siasa ili waendelee na kazi zao wasije wakafukuzwa.

  SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pengine au ndo ilivyo kuwa Karume anapotoka Ikulu na kuelekea Nyumbani kwake, msafara wake unakuwa wa kasi sana hivyo hawezi kuona kwa utulivu hata akitaka kuangalia nje kuona raia zake walivyochoka kwa manyanyaso ya serikali yake, natamani siku moja ange simama walau soko la Darajani akaona watu wanavyosonya na kumkunjia uso kwa kuchoshwa na uongo wake na kujidai kwake kuwa kila kitu kiko shwari zanzibar...watu wamechoka Mh. Karume na washauri wako wanakwambia hali ni shwari nawe unakariri kama unavyoambiwa matokezeo yake unasutwa na hali halisi.
   
 3. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wala hadanganywi, nadhani anaujua ukweli wote ila yeye ndio anadanganya umma kwa maslai yake ya kisiasa.....
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu sio kwamba andanganywa ANAPENDA kudanganywa!
  Suala la Pemba taratibu linaanza kumtokea puani,kama sasa hivi jamaa wanchomeana nyumba, mwakani ndo kutakuwa kisanga.
  Huyu Rasi Karume heleweki, inaelekea yeye na JK hawawivi na kuendelea kwake kukaa pale ni lazima apate ridhaa ya JK.
  JK mwenyewe hawajaonana kwa kipindi sasa katika shughuli za pamoja na sherehe, amekuwa akitoa udhuru mbali mbali.
  Imebidi Polisi Namba Moja Saidi Mwema aende Zenj kutoa somo kuwa msitegemee amani wakati mifumo yenu ya kisiasa haijakaa sawa.
  Karume kama mtoto wa Abeid Aman Karume ametuangusha na anpoelekea mwishoni mwa kipindi chake cha uongozi haeleweki kama anchofanya ni mbinu ya kubaki madarakani au la!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani wapemba wameamua kumuonyesha kwa kulipua bomu miguuni pake!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nasikia wamisema kuwa sasa kazi, kama duniani hawajui kuna kasehemu ka ardhi kanateswa hapa ulimwenguni kwa kutumia vyombo vya Dola vya Nchi ya Tanzania ,basi karibu wataelewa na kila mmoja hapa ulimwenguni ataijua Pemba ipo wapi na kama haitoshi viongozi wa nchi itawabidi wajibu kama Muwa ni tunda au si tunda au mpaka wafahamu na kuweza kuwaelewesha watu Muwa ni kitu gani ?
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mh. Kiketwe aseme alichoambiwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kii Moon kuhusu hali ya kisiasa Tanzania hususan Zanzibar katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010. Wasifikiri huu ujinga wao wa kupiga piga watu watanyamaziwa siku zote wenzao Kenya tumbo joto huko, ICC weshasema wanataka kuweka mfano na wanaanzia Kenya, ole wao akina Kikwete na Karume.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naomba ieleweke kuwa, Rais Aman Abeid Aman Karume ni kibaraka (puppet).

  Kwa jina lingine ni karagosi. Kwa wale wenye kujuwa maana ya karagosi sina haja ya kufafanua zaidi. Kwa wale wasiojuwa maana ya karagosi, ufanunuzi ni huo hapo chini:


  Puppetry > Your Puppet Play

  [SIZE=+1]Your Puppet Play[/SIZE]
  [​IMG]


  Walioelewa wameelewa, na wale ambao hawajaelwa:

  Karagosi hana akijuwacho, ni kisanamu kilichotengenezwa na kinaweza kuchezewa na alie kitengeneza atakavyo.

  Karume ni kiKaragosi cha MKAPA alipoondoka, akamrithisha Kikwete. Simpo.

  Kama ni hivyo, mwenye akili timamu atamlaumu Karagosi? nope.
   
 9. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Anasutwaje? (thibitisha!!) na hiyo hali. Enzi hizi siyo za propaganda, bali ni za ukweli na uwajibikaji. Acha porojo za wale wa zamani -Ndugu yangu.
   
 10. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu wanataka kujua TANZANIA ipo wapi na siyo Pemba. Pole yako Bwana Mwiba.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pakacha, Karume aliposema kuwa hali ya Zanzibar shwari siku ya pili usalama wake wa taifa wamekwenda kulipuwa mabomu, hiyo shwari ipo wapi hapo kama si mtu mzima kusutwa na hali halisi ya matukio?
  We huoni mawaziri wake Karume wanavyoamka na kupayukwa payukwa "...kuna mabomu wee, daraja limelipuliwa weee...watu wanafanywaje sijuwi..." halafu wenye uchungu na roho za watu wao wanawakataza wasije Zanzibar maana weshasikia kuwa hali si shwari huko, mabomu mtindo mmoja, haohao walotoa onyo hilo wanarudi kinyume wanasema "..ooooh! ajenda ya siri..." huku si kusutwa na halisi ya mambo?
  Tatizo la viongozi wa SMZ na SMT hawafikiri nje ya boksi wao wanaona kauli zao zinaishia humo humo tu vijiweni, hushangai Kikwete anakutana na Ban Kii Moon, NY Marekani anaulizwa habari za mchafu koge za Zanzibar anatoa macho akitafuna maneno tu, huku si kusutwa na hali halisi?
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Na wewe ni kikaragosi cha nani? You dont sound original
   
Loading...