Rais Karume ChupuChupu Na Mabomu Pemba: Ni Siku Moja Baada Ya Kudai Hali Ni Shwari. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Karume ChupuChupu Na Mabomu Pemba: Ni Siku Moja Baada Ya Kudai Hali Ni Shwari.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Sep 30, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SIKU moja baada ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwahakikishia wananachi na wageni kuwa Zanzibar ni shuwari na atakayetaka kutembelea anakaribishwa mripuko mkubwa umetokea katika nyumba moja Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Mripuko huo umetokea majira ya saa 4 usiku katika nyumba ya Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhan Issa Kipaya Mtaa wa Mtemani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kusababisha nyumba hiyo kuharibika eneo la kuta zake lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
  Juzi katika ziara yake ya ziku mbili Kisiwani Pemba Rais Amani Karume amewahakikishia wananchi na wageni wanaotaka kutembelea katika visiwa vya Zanzibar kuwa Zanzibar ni shuwari na hakuna matatizo yoyote kama inavyokuzwa na waandishi wa habari kwamba hakukaliki.
  Alisema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya amani na utulivu tokea miaka ya chuma hivyo mtindo uliojitokeza katika siku za karibuni wa kuchoma moto nyumba hauna maslahi kwa wananchi na badala yake aliwataka wanasiasa waliofilisika kufunga virago na kutafuta shughuli ya kufanya.
  “Zanzibar kuna amani tena utulivu wa kutosha watu wanafanya shughuli zao za kawaida na tunawalika wengine pia waje kutembelea visiwa hivi na wachane na wale watu wanaosema kuwa Zanzibar hakukaliki, nyumba zaripuliwa hayo ni maneno ya waandishi tu” alisema Rais Karume.
  Kada huyo anadaiwa kuwa ndio mhamasishaji mkubwa wa wana CCM wenye kuogopa kujitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kisiwani Pemba.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi alithibitisha kutoka kwa mripuko huo ambao umeshitua kutokana na mlio mkubwa uliotokea katika mtaa huyo ambapo sehemu kubwa ya wananchi wa eneo hilo wlaikuwa majumbani mwao.
  “Ni kweli mshindo ulikuwa mkubwa sana na watu nyakati hizo walikuwa wamelala na mimi nilikuwa nipo nyumbani naangalia televisheni lakini niliposikia nikatoka na kwenda katika eneo la tukio tukiwa na mkuu wa mkoa wa kaskazini” amesema Kamanda Bugi.
  Amesema mripuko huo unatokana na bomu linalotengenezwa kwa baruti ambalo hutumika kwa kupasulia miamba baharini na nchi kavu ambapo baadhi ya watengenezaji wa barabara huwa wanatumia kwa kupasulia barabara kubomoa na kuitawanya miamba hiyo.
  “Haya mabomu hutengenezwa kwa baruti lakini huwa inapasuliwa miamba ya baharini na na nchi kavu pia hutumika hasa kwa wale watengenezaji wa barabara na mlio wake unakuwa mkubwa kama mabomu ya kawaida” Alisema Kamanda.
  Kamanda Bugi amesema mabomu hayo yaliotokea Mtemani ni sawa na yale yalioripuliwa hivi karibuni katika madaraja ya Piki wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi amesema uripuaji wa mabomu huo anauhusisha na wanachama wa CUF kutokana na kuwa hawataki kuona wananchi wanajitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaoendelea Kisiwani Pemba.
  Dadi amesema pamoja na kuwa wana uhakika wa wanaoendesha vitendo vya uharamia ni wafuasi wa CUF lakini hawatawachukulia hatua za kuwakamata kwa kuhofia kwenda kuwalisha chakula cha bure ambacho kitaigarimu serikali ya mapinduzi Zanzibar.
  “Sisi tunawajua wenye kuendesha miripuko na vituko hivi ni hawa CUF lakini hatuwakamati maana hatutaki kuwalisha bure tunataka tukimkamata mtu tumepeleke mahakamani afungwe na sio kumlisha bure” amesema Mkuu wa Mkoa Dadi Faki.
  Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura unaoendelea katika Mikoa mwili Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba umekuwa na matukio ya kila aina huku baadhi yao yakiwa na ya uvunjifu wa amani ambapo jeshi la polisi yatari limeshatoa tahadhari kwa wananchi kutoancha kuwachukulia hatua kali dhidi yao watakaokwenda kinyume na agizo la kudumisha amani katika visiwa hivyo.

  SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hizi kauli za Dadi na kada mwenzake kamanda Bugi zinaonyesha wazi kuwa mlipuko huo ni wa kuzuga tu, lakini wanachokifanya hawakijuwi ni kuitia doa nchi katika sura ya kimataifa, leo rais anasema hali shwari kesho usalama wa taifa wanatafuta milipuko hewa wanalipua nani atakubali kuwa hali ni shwari?
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Junius Staghrafillu Ndugu yangu. Usiombee mabaya kuhusu watu wako wala usiwadanganye watu wako.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pakacha alodanganya Karume...kageuka kawa kama yule alyekuwa waziri wa habari wa Saddam Hussein M. Saed al Sahaf, akisema kuwa wameyadhibiti majeshi ya wavamizi huku mabomu yakilipuka nyuma yake.
   
 5. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu junius utajiumisha kichwa bure na sikuhizi hata zile vinaki hakuna tena kwa kuyasikilia maneno ya watu ambao wamesoma hawakujuwa lakini wanasema wamejifunzawamejuwa kwa mana hiyo walipokuwa wakisoma elimu ilikuwa inaingia sikio la kulia na kutokea la kushoto ,na kuna wengine hadi leo wanatumia mapakacha kutekea (kuchotea maji) kazi ipo hapo,asie na mwana aeleke jiwe.Tariq azizi alikuwa na maneno kuliko mwanamume anaevalishwa kanga na wanaumwe wenziwe

  Tariq Aziz  [​IMG] Aziz was 43rd in the US "most wanted"  Former Deputy Prime Minister Tariq Aziz was the face of Saddam Hussein's regime on the world stage for many years.
   
Loading...