Rais Karume Amechemka? Adaiwa Kuvunja Katiba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Karume Amechemka? Adaiwa Kuvunja Katiba.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 4, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Amani Karume amefanya uteuzi wa Jaji Mkuu bila ya kushauriana na Tume ya Utumishi ya Mahakama imebainika.
  Taarifa za uhakika kutoka ndani ya serikali na mahakama, zinasema Rais Karume amemteua Hamid Mahmoud kushika tena wadhifa huo baada ya kuwa amestaafu kwa hiari na kulipwa mafao yake.
  Ofisa Mwandamizi katika Ofisi ya Waziri Kiongozi amethibitisha kwamba Rais Karume tayari amemteuwa Hamid.
  Alisema, "Unachokisema ni kweli. Tayari Mzee (Rais) ameteua Jaji Mkuu baada ya kuwa amestaafu na hapana shaka katiba imevunjwa maana utaratibu unaobainishwa na katiba haukufuatwa."
  "Hivi wewe unafikiri mambo yanaendeshwa kikatiba hapa. Mwenyewe akishasema hakuna wa kuuliza," alisisitiza.
  Taarifa za kuaminika kutoka serikalini zinasema, Hamid alistaafu kwa hiari Aprili mwaka huu akiwa na umri wa miaka 60.
  Hata hivyo, anaendelea na wadhifa huo, baada ya kuteuliwa tena bila rais kushirikisha Tume ya Utumishi ya Mahakama.
  Mrajis (Msajili) wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Yesaya Kayange alithibitisha Karume kumteua Hamid kuwa Jaji Mkuu mpya baada ya kustaafu.
  Kayange ndiye Katibu wa Tume ya Utumishi ya Mahakama na mratibu wa vikao vya tume hiyo.
  Alisema jukumu la tume ni kutoa maoni kwa rais ambaye kikatiba ndiye anayeteua majaji; baada ya rais kufanya uteuzi wake, inachofanya tume ni kutekeleza hatua za kufanikisha lengo la rais.
  Jaji Hamid amestaafu akiwa hajafikia umri wa miaka 65, ambao unatajwa na Katiba ya Zanzibar kuwa wa kikomo kwa mtu anayeshika wadhifa huo. Kifungu 95(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinaelekeza kuwa akifikia hapo, anastaafu kwa lazima.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Katiba na Utawala Bora), Mahadhi Juma Maalim amethibitishia gazeti hili juzi Jumatatu kwamba "Rais amefanya uteuzi wa Jaji Mkuu" na kwamba mezani kwake alikuwa anakamilisha taratibu za mkataba wake wa miaka miwili.
  "Ni kweli na mimi nimeletewa jalada ili kupitia masuala ya mkataba wake wa miaka miwili. Mambo ya taratibu nyingine yana wahusika wa kuyafanyia kazi," alisema.
  Alisema, "Hayo mengine ungewapata watu wa Tume ya Utumishi ya Mahakama. Hao ndi wahusika wakuu." Alikiri kwamba anaamini jaji angeweza kumaliza muda wake wa awali baada ya kufikia miaka 65.
  Kwa mujibu wa sheria, Jaji akishastaafu, iwe kwa hiari au kwa lazima, anakuwa amekoma kuwa jaji na kwa hivyo, hata kile kiapo alichokula wakati wa uteuzi kinakuwa kimefutika.
  Aidha, kwa mujibu wa sheria ajira ya Jaji anayepewa mkataba inaweza kufutwa wakati wowote na mamlaka iliyomteuwa (Rais) kwa kuwa halindwi na katiba.


  Ifuatayo ni version kwa mtizamo wetu MwanaHALISI: Suala la kupindisha katiba limekuwa moja ya matatizo makubwa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  Jaji Steven Bwana, katika kitabu chake, "Haki, Amani na Maendeleo: Nafasi na wajibu wa mahakama Tanzania," anasema, "Majaji wanaostaafu na kupewa mikataba si majaji kwa mujibu wa katiba."
  Jaji Bwana anasema suala kubwa ambalo linaweza kuibuka ni: "Je, ajira hizi za mikataba kwa majaji ni sahihi?" Anasema kwa kuwa jaji amestaafu, kiapo chake nacho kimeondoka… Ni hoja yangu kwamba majaji waliostaafu si majaji kwa mujibu wa Katiba."
  Hamid alipoulizwa kuhusu kustaafu kwake, kulipwa mafao yake na kurudishwa kazini kwa mkataba kinyume cha taratibu, haraka alisema, "Mimi najua nimeongezewa muda. Basi!"
  Alisema "Nimepewa mkataba wa miaka miwili. Hilo suala la kucheleweshewa mafao yangu, mbona halipo."
  Alipong'ang'anizwa kama ameshalipwa mafao yake ya awali, Hamid alijibu, "Ninachojua nimeongezewa mkataba. Hicho ndicho ninachokijua."
  Gazeti lilithibitishiwa na ofisa mmoja wa hazina ambaye hakutaka kutajwa kuwa tayari Hamid amelipwa mafao yake ya kustaafu yanayofikia zaidi ya Sh. 180 milioni.
  "Suala la mafao yake ya kustaafu halina utata. Tayari ameshalipwa na hatuna mgogoro naye… ukweli tuko mbele katika kulipa mafao ya watu, na yeye angetakiwa kusubiri waliomtangulia kudai mafao yao lakini hatukumchelewesha kwa sababu ya hadhi yake," alisema.
  Alisema, "Nilipo siwezi kujua kwa hakika kiasi cha fedha cha mafao yake lakini nina hakika tumemlipa tayari," alisema kwa mkazo.
  Kuna taarifa kwamba Hamid ametaka serikali kumlipa mafao yake ya mkataba mpya, kwa mkupuo kabla ya mkataba wake kumalizika, jambo ambalo limezua zogo ndani ya serikali kwa madai ni kinyume cha taratibu.
  Jitihada za kumpata Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Khamis Mussa hazikuzaa matunda. Kila alipopigiwa simu ofisini kwake mjini Zanzibar, majibu ya makatibu muhtasi wake yalikuwa "bado hajarudi kwenye kikao."
  Ijumaa iliyopita, mwandishi wa habari hizi alipomtafuta Mussa alijibiwa kuwa yupo masomoni Uingereza. Waliopo badala yake, ni manaibu wake, Amina Khamis Shaaban na Abdi Khamis Faki.
  Hata hivyo, wote wawili walipotafutwa hawakupatikana kwa madai kwmaba walikuwa nje ya ofisi kikazi. Juzi Jumatatu waliendelea kutafutwa tena, lakini jibu lilikuwa ni hilohilo.
  Kifungu 94(1) cha Katiba ya Zanzibar kinaelekeza kuwa jaji mkuu atateuliwa na rais kutokana na majaji wa mahakama kuu na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi ya Mahakama.
  Kijifungu (2) cha kifungu hicho, kinasema majaji wa mahakama kuu watateuliwa na rais kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi ya Mahakama.
  Tume ya Utumishi ya Mahakama inayotajwa katika kifungu 102 cha Katiba ya Zanzibar, imeundwa rasmi kwa Sheria Na. 2 ya mwaka 2002 na wajumbe wake kwa mujibu wa kijifungu (1), ni Jaji Mkuu, Jaji mmoja wa Mahakama Kuu, jaji mmoja mstaafu wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Wote wanateuliwa na rais.
  Wengine ni wakili mmoja aliyeteuliwa na rais kutokana na mapendekezo ya Chama cha Wanasheria Zanzibar; Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikalini; Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Kadhi Mkuu; na Mtu mwingine yeyote ambaye rais ataona anafaa.
  Kifungu 102A kinasema tume itakuwa na uwezo wa (a) Kumshauri Rais juu ya uteuzi wa Jaji Mkuu; na (b) Kupendekeza kwa Rais uteuzi wa jaji wa mahakama kuu.
  Tume hiyo pia ndiyo yenye mamlaka ya kupendekeza mishahara, marupurupu na mafao ya uzeeni ya majaji na mahakimu.
  Wajumbe watatu wa Tume hiyo waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina wamesema, taarifa za Hamid kuteuliwa baada ya kustaafu wanazisikia pembeni.
  Mmoja alisema, "Hizi ni taarifa mpya kwangu. Kwa hakika ndio unanifahamisha kuwepo kwa jambo hili na hakuna kikao cha tume nilichoalikwa kuhudhuria nikakosa kushiriki."
  Alisema, "Labda wenzangu wanalijua jambo hili waulize. Hili suala ni zito sana, nami sifahamu ni kwa vipi limetendeka. Hivi umefika kuwauliza wenyewe, maana labda haiwezekani."
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Iddi Pandu Hassan ambaye ni mjumbe kwa wadhifa wake, amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sasa na mwandishi hakufanikiwa kumpata hata alipomfuatilia nyumbani kwake mjini Zanzibar. Pandu hana simu ya mkononi.
  Lakini taarifa za ndani ya ofisi yake, zimeithibitishia MwanaHALISI kuwa suala hilo hadi anaondoka kwa ajili ya kwenda kupata matibabu nje ya nchi, hawakulisikia kutoka kwake.
  Mawakili watatu wa serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, walisema wanasikia tu mitaani lakini hawajaona kama uteuzi huo umepita katika utaratibu unaotakiwa.
  "Nimesikia mafao yake yameandaliwa tayari. Lakini kwa kweli nadhani utaratibu haukufuatwa wa kumteua tena," alisema mmoja wao kwa msisitizo.

  SOURCE:ZANZIBAR YETU BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Karume nasema hakuna wa kumuuliza fanyeni tu kama nilivyoagiza,kwa hiyo hizo tirigivyogo za uchaguzi na kuiba kura pamoja na kutumia mtutu wa bunduki kulinda wizi huo ataendelea kufanya tu na hakuna wa kumuuliza. Jamani CCM imechoka nyie na watu wameichoka, hila hazishi, viongozi kila kukicha mikasa tu. Lo!
   
 3. C

  Chakarota Member

  #3
  Aug 4, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eee Bwana,
  Kwa hili mimi naona kafanya cha maana, kwani jamaa ameshaona mbali kua kuna mpango wa kuletewa jaji mkuu kutoka bara (Dodoma's choice). Kwani hukumbuki kuletwa majaji kibao kutoka bara mpaka wilaya ndogo ndogo za Pemba, cha ajabu wote walioletwa majaji ni wakiristo.
  Mind you sina ugomvi na wakiristo lakini kesi ya mke Fatuma kagombana na mumewe Khamis abeid niambie jaji huyo ataiamua vipi/ WAKATI UGOMVI UMO KWENYE SHERIA YA KI-ISLAM. Kwa hakika ni vichekesho tu mahakamani.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hapana Karume kachemka kweli, Karume kaona Tume ya Uajiri ya Mahakama ingempendekeza Naibu Jaji Mkuu Mshibe Ali Bakari, ambaye ni kutoka Pemba.kwa muda wote Mshibe amekaimu nafasi ya Jaji Mkuu na ana uzoefu Mkubwa wa nafasi hiyo, lakini katika kile ambacho SMZ wameapa hawatokifanya ni kumpa Mpemba nafasi yoyote ya juu katika mihimili mitatu ya dola, na kwa kuhofia hilo ndo maana nafasi hiyo imezibwa kimagube kabla ya tume ya uajiri ya mahakama haijampendekeza Mshibe ambaye alionekana dhahiri ndo mtu pekee anaeimudu na mwenye uzoefu wa nafasi hiyo. Ni siasa tu.
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Jamani nchi hii nzuri ya tz udini tuatupeleka pabaya!

  Sote tu Watz!
   
 6. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zanzibar kuna makadhi sasa lini majaji wa serekali ya muungano wakaingilia mambo ya ndoa? Acheni udini tufikirie tanzania mpya yenye neema hivi mmerogwa?
   
Loading...