Rais Karume Abariki "Vurumai" Pemba.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amesema Serikali haitafuta matumizi ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kama kigezo moja wapo cha kuandikishwa kuwa mpiga kura kama ilivyopendkezwa na wapinzani visiwnai hapa.

Kauli hiyo ya Rais Karume imekuja siku chache baada ya wapinzani kulamikia zoezi la utoaji wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kwa madai ya kutolewa kwa misingi ya kisiasa jambo ambalo baadhi ya wananchi hukoseshwa kupewa na kusababisha kukataliwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura lililoanza jana Kisiwani Pemba baada ya kuakhirishwa mwezi uliopita.

Rais Karume ameyasema hayo katika mikutano yake na wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Matawi na Maskani za Chama hicho katika Mkoa wa Kusini Pemba jana kabla ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili kisiwani hapa.

Alisema watu wasiokuwa na sifa wasahau kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwani hatua ya Serikali ni kuondosha malalamiko katika Uchaguzi kwa kuwepo mamluki.

"Taarifa zilizonazo ni kwamba wananchi wengi wanavyo vitambulisho hivyo wanastahiki kuandikishwa kama wapigakura isipokuwa wapo wengine wametupa vitambulisho vyao kwa sababu ya dharau, jeuri, kiburi, na ujinga, ila nasema hawajachelewa waende wakajiandikishe ili waingie kwenye daftari" amesema Rais Karume katika mkutano wake.

Amesema kuna Mbunge wa Kaskazini Pemba ambaye hakutaka kumtaja jina lake alimlalamiki kuwa wapigakura katika Jimbo lake 2000 hawana vitambulisho lakini alichomwambia ni kuwa aandike majina ya watu wake na baadae ampelekee mkuu wa mkoa wa mkoa huo.

Rais Karume alisema lengo la kuwepo kwa daftari ni kutaka kudhibiti mambo mbalimbali ikiwemo udanganyifu katika Uchaguzi kwa kuwashirikisha watu wasiokuwa wakazi katika Majimbo kuwachaguliwa Viongozi wa jimbo fulani hivyo suala la vitambulisho litakuwepo na haliwezi kusitishwa.

"Haipendezi mtu kutoka Tanga au Mombasa aje kupigakura hapa Mkanyageni…nyie hilo mtakuwa hamkubali na ni suala ambalo ni kinyume na sheria maana tumekubaliana mtu akae katika Jimbo miezi 36 mfululizo sasa wewe hujakaa unataka kuandikishwa" aliuliza rais Karume

Hta hivyo Rais aliwabeza wapinzani kuwa hawawezi kushind akatika uchaguzi mkuu wa 2010 na kuwataka wanachi wa pemba kuachana na wapinznaia na waendelee kikiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwa kimepleta maendeleo makubwa katika visiwa vya Unguja na Pemba.

"Kwa hiyo anayekataa daftari ni mchezo wa siasa tu unaotumika kukataa daftari hili niwatobolee siri moja wapinzani wanaona haya kwani kila jambo tuliloahidi tumefanya sasa hawana cha kusema kazi yao wao ni kupinga sasa wakiunga mkono hawapaswi kuwepo hapo wanahofia tunaweza kuchukua nafasi" Alisema Rais Karume.

Alisema mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa hapa nchini wanasiasa waliounda vyama vya Upinzani walidhani kuwa ni ugomvi, uhasama na chuki kwa kuwa hawakuwa weledi katika ushindani wa siasa za vyama vingi na ndio mambo ya ugomvi hutokea kutokana na kutokujua maana halisi ya vyama vya siasa.

Rais Karume alitumia ziara hiyo kuelezea mafanikio mbalimbali ya Serikali yake ikiwa pamoja na ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami, vituo vya afya na huduma nyengine za kijamii.

Pia aliwahakikishia wananchi wa Pemba kuwa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika litakuwa historia kwao kwani Serikali ipo k`tika hatua za mwisho za kukamilisha mradi mkubwa wa umeme chini ya bahari wa gridi ya Taifa kutoka Pangani Mkoani Tanga hadi Kisiwani Pemba ambapo umeme huo utaanza kutumika Desemba mwaka huu.

siku ya mwisho ya ziara yake iliyoanza juzi, Rais Karume ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, alitembelea Maskani mbalimbali na kubadilisha mawazo na wazee wa Chama hicho ambapo alisema chama chake kimejipanga vyema katika kuhakikisha kinachinda katika uchaguzi wa 2010 na kuwatak wana CCM kutokuvunjika moyo na ushindi huo.

Akizungumza na wazee wa chama cha mapinduzi katika matawi mbali mbali ya wilaya ya mkoani kisiwani pemba Rais Karume alisema kwamba sheria za uchaguzi zitaendelea kutumika ikiwa pamoja na matumizi ya vitambulisho ili kudhibiti wapiga kura mamluki.

"Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wapinzani wetu wanasema kura zinaibiwa katika hali hiyo tulisema atuweke utaratibu wa kuondosha malalamiko hayo kwa kuwa na vitambulisho…sasa leo watu wanataka vitambulisho visitumike hilo haliwezekani" alisema rais karume.

Wakati Rais Karume akiwa kisiwani Pemba akijivunia mafanikio ya serikali yake ya kuimarisha miondo mbinu ya barabara, maji na umeme wananchi wa kisiwa hicho kwa wiki nzima sasa wanalala giza kutokana na khitilafu zilizotokea katika shirika la umeme Pemba na kusababisha magenereta yenye kutoa huduma hiyo kusafirishwa dar es salaam kwa matengenezo.
 
Kama nilivyawahi kusema siku zile karume alipokutana na wawakilishi wa EU, ikulu Zanzibar kuwa atajikosha na kuwaondoa njiani huku akiendelea na mipango yake ya kuhujumu wananchi na kuvurugua uchaguzi. Karume kawaahidi wajumbe wa EU uwongo kwa kuwa kauli na matendo yake hayatangamani hata kidogo.
 
Mwaka huu, haki ya Mungu cha moto watakiona pemba!ngoja wachague ama karafuu au nyuki na mabomu wanayoyaona deal!
 
waziri mkuu wa Denmark alipofika hapa Zenj baada ya uchaguzi uliopita, na kukutana na karuma iliripotiwa katika magazeti ya kidenish akisema kuwa huyu Rais wa zanzibar (karume )si mkweli hata ukimuangalia usoni kwake utaliona hilo )namnukuu waziri wa mkuu wa denmark
 
Swala la vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi zinaumiza kichwa ni mbinu chafu za CCM.
 
Swala la vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi zinaumiza kichwa ni mbinu chafu za CCM.
Mh!! Siyo mbinu chafu za CCM Bwana, ni mbinu za kuwadhibiti wapiga kura mamluki. sasa hawa mamluki kwa kule Pemba wanaweza kuwa ni watumishi wa vikosi vya ulinzi na wa Serikali wanaopelekwa uhamisho kwa kazi kule. Lakini pia wanaweza kuwa ni wapambe wanaoishi Dar, Tanga, Mombasa au hata daraja Bovu na kwahani kule Zanzibar na wakataka kwenda kupiga kura Mgogoni wakiwa si wakaazi wa Shehia ya Mgogoni. Upo hapo!!!
 
Mambo ya huko ni magumu sana. lazima SMZ ifikiri tene na tena kwani wanatakiwa wajue kuwa Pemba hawana chao. wao muhimu wakazane na Unguja.

Najiuliza hivyo kweli kabisa hawa Viongozi wa SMZ wamefunga kweli?
 
Wadugu wa zenj matatizo yenu mnamwita mzungu aje asuluhishe!!! Muzungu huyo huyo akisema Bashir atiwe ndani mnasema Mzungu anaingilia mambo yenu.

Nashauri mtumie waarabu zaidi watawasaidia kuondoka tatizoni.
 
Mh!! Siyo mbinu chafu za CCM Bwana, ni mbinu za kuwadhibiti wapiga kura mamluki. sasa hawa mamluki kwa kule Pemba wanaweza kuwa ni watumishi wa vikosi vya ulinzi na wa Serikali wanaopelekwa uhamisho kwa kazi kule. Lakini pia wanaweza kuwa ni wapambe wanaoishi Dar, Tanga, Mombasa au hata daraja Bovu na kwahani kule Zanzibar na wakataka kwenda kupiga kura Mgogoni wakiwa si wakaazi wa Shehia ya Mgogoni. Upo hapo!!!

Pakacha wacha ishitizai zako hizo nakuapia kwa Mmungu ipo siku atakushushia mitihani itakayo kuletea majuto hadi siku yako utakayowekwa katika mwanandani, ukweli siku zote unayafanya batil.
 
Last edited:
Pakacha wacha ishitizai zako hizo nakuapia kwa Mmungu ipo siku atakushushia mitihani itakayo kuletea majuto hadi siku yako utakayowekwa katika mwanandani, ukweli siku zote unayafanya batil.
Usiwe hivyo Ndugu yangu mtu humuombea mwenziwe mema. Mimi ni m-tan-ZAN-ia mwenzio, Bwana!!!!
 
Pakacha wacha ishitizai zako hizo nakuapia kwa Mmungu ipo siku atakushushia mitihani itakayo kuletea majuto hadi siku yako utakayowekwa katika mwanandani, ukweli siku zote unayafanya batil.
Mkuu kweli inauma...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom