James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Wasalaam
Ni ukweli usiopingika kuna matatizo makubwa sana tena sana kwenye mradi huu wa mabasi yaendayo haraka na hatua za haraka zisipo chukuliwa ni ukweli ulio wazi taifa litaingia kwenye maafa yanayo weza kuzuilika kabisa!
Mh Rais
Lazima tukubali kuwa matatizo ya mradi huu yamewashinda watu wengi akiwemo waziri mkuu lakini bado matatizo kwenye huu mradi yanaongezeka kila leo.
Mh Rais
Ni ukweli ulio wazi kabisa mradi huu una matatizo mengi na una hatarisha maisha ya watanzania wengi wanao tumia mradi huu na ni kwamba ni mradi hatarishi sana kwa maisha ya watu ni lazima watu wachukue hatua sio kuongea tuuu!
Mh Rais
Mradi huu mabasi yanajaza habaria kupita kiwango
Kupitia Mradi huu umekuwa sehemu ya watu kupoteza vitu vyao vya thamani kutokana na vurugu za kugombania magari
Mh Rais
Kupitia mradi huu watu wamekuwa wakiumizwa na kuvunjwa viungo wakigombea magari...
Kupitia mradi huu imethibitika kabisa waendesha mradi wanafanya makusudi kuchelewesha magari hili watu wajazane kwenye gari moja au mawili ili wasave mafuta maana ni magari machache yatatumika!
Mh Rais
Kupitia mradi huu tumethibitisha kuwa watanzania wenyewe ndio wahujumu namba moja wa miradi yao maana inawezekanaje hakuna kiongozi wa juu au wachini ambaye aoni kama kuna shida kubwa sana....
Kupitia mradi huu watumiaji wa magari haya wameshuhudia magari ya kizidiwa uzito na mengine kupata pancha na hakuna anaye jali kabisa ....kweli hatujui kitakacho fata?
Mh Rais watu wengi wamesema sana tena sana kuhusu mradi huu lakini hakuna linalofanyika kabisa hakuna kiongozi anayechukua hatua lakini ukweli ni kwamba mradii kwa mwendo wake ujiandae kuandika barua ya kutoa pole kwa watanzania kama hatua azito chukuliwa !
Mh Rais mradi huu kila miundombinu yake haifanyi kazi kuanzia kwenye tuketi, speaker na camera na hata vituo mabati yameanza kutoka na hakuna anayefanya lolote............hii ni makusudi kabisa!
Mh Rais
Huhitaji kuwa mtabari kujua kuwa mradi huu kama hatua hazichukuliwi ni lazima utaleta maafa makubwa na tutakuwa wanafiki kutuma salamu za rambi rambi wakati tunaweza tatua matatizo haya!
Ni lazima hatua za haraka zichukuliwe kuzuia maafa kwenye mradi huu
Mkuu unafanya vizuri kuchangia hoja lakini waziri wa usafiri si yupo? Ninachojaribu kusema ni kwamba kila kitu hawezi kufanya rais peke yake la sivyo mtammaliza kwa presha.
Waziri wa usafiri yupo na analipwa na pesa zenu kufanya kazi hizi.