Rais Kagame Yeye Nchi Yake U.S.A Na EU Hawajawahi Kumjadili Na Wala Kumwekea Vikwazo.

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,963
28,450
Baada Ya kuangalia Dunia ilivo napata maswali mengi sana juu ya nchi yangu Tanzania, Mama Tanzania.
Hivi Rais Magufuli kwa miaka mitatu amefanya mabaya sana kuliko Rais Kagame wa Rwanda?
Naona kuna kitu kisicho cha kawaida kitatujia Watanzania.
Mbona Rwanda haijawahi kujadiliwa kama sisi na wala hata kuwekewa vikwazo vyovyote na EU au U.S.A
images.jpg
 
Kwanza tofautisha akili ya Jiwe na akili ya Kagame.

Mwenzako akiharibu anaenda kuwafuata kabisa huko huko kwao kuyamaliza ndio maana unaona hawasemi kitu.

Sasa jiwe linaharibu halafu linajifungia ndani huku likiporomosha "matusi" unategemea nini? wakati huendi kuongea nao
 
Ameharibu kipi?
 
Unamjua kagame kweli wewe never seen someone so rude like him! Aliwaambiaga kama vp watume drone likaipige Rwanda waondoe udhia!
 
Watazungukaaa, nukta itarudi pale pale, rasilimali. Wazungu ukiwabania rasilimali zako, lazima wakutoe madarakani tena kwa vita.

Wakati nyie mpo busy kupigana, wao wanawaletea silaha na kuondoka na rasilimali.

Endeleeni kuwa chekelea tu.
 
kwaiyo tuwabanie tusiwabanie?

Hilo ndo swali la msingi. Jibu lolote kati ya hayo ni lazima sisi kama nchi twende pamoja.

Ingawa tunajua hatuwezi wote kuwa na mawazo sawa lakini angalau tuweze kutofautisha ukweli na propaganda. Tujue kuwa nchi ni yetu, siyo ya mchina na wala siyo ya mzungu.

Yoyote anayekuja kukusaida, tumwangalie mara mbili na tujue kuwa kuna kitu anataka kutoka kwetu.

Pia tuelewe kuwa, chochote tunachofanya cha maendeleo Tanzania, kuna watu taifa lingine wana athirika.

Mfano, kufanya processing ya Tanzanite Tanzania, kuna watu India wamekosa kazi. Hawawezi kufurahi.

Tukiweza changanua hizo mbichi na mbivu, tutaweza kwenda pamoja.
 
Japo mkuu wetu kuna mambo ameyaharibu katika kijiji chetu hiki amepeleka mambo mengi sana ya kijiji ndivyo sivyo. Kubwa litakalosababisha tukumbwe na radi kali ni Umeme (hivi ule mradi alikuja kuuzindua nani vilee), kingine ni zile pesa zinazochimbwa kwenye mashimo. Huyo bwana mwiingine kijiji chake hakina lolote lakusababisha kiangaliwe mara mbili mbili labda milk teh teh. Hivi jirani yake Mr slim alishawahi tolewa matamko pia?

Kijiji changu kinatia hasira sana sometimes ila nakihurumia sana ngoma inayopigwa sijui kama tutaweza kuicheza.
 
Hilo ndo swali la msingi. Jibu lolote kati ya hayo ni lazima sisi kama nchi twende pamoja.

Ingawa tunajua hatuwezi wote kuwa na mawazo sawa lakini angalau tuweze kutofautisha ukweli na propaganda. Tujue kuwa nchi ni yetu, siyo ya mchina na wala siyo ya mzungu.

Yoyote anayekuja kukusaida, tumwangalie mara mbili na tujue kuwa kuna kitu anataka kutoka kwetu.

Pia tuelewe kuwa, chochote tunachofanya cha maendeleo Tanzania, kuna watu taifa lingine wana athirika.

Mfano, kufanya processing ya Tanzanite Tanzania, kuna watu India wamekosa kazi. Hawawezi kufurahi.

Tukiweza changanua hizo mbichi na mbivu, tutaweza kwenda pamoja.
Baada ya kutoa point zako konki nimegundua kuwa kuna jitu moja tu la kulaumiwa kwa haya yote. Lipo bize kuua umoja na mshikamano wetu kiasi kwamba hatuwezi kusimama pamoja tena hata kwa maslahi ya taifa. Adui Wa taifa ni hili jitu moja tu
 
Back
Top Bottom