Rais Kagame wa Rwanda Kusaini Mikataba ya Utendaji na Mawaziri Wake Wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kagame wa Rwanda Kusaini Mikataba ya Utendaji na Mawaziri Wake Wote

Discussion in 'International Forum' started by Gosbertgoodluck, Dec 17, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wandugu,

  Hii nimeipata kupitia habari za Afrika ya Mashariki zilizorushwa na Kituo cha ITV leo kwenye taarifa ya saa mbili usiku kwamba Rais Paul Kagame wa Rwanda atasainiana na mawaziri wake wote mkataba unaoitwa kwa kimombo "Peferfomance Contract". Lengo la mpango huo, ni kuongeza uwajibikaji kwa mawaziri na matokeo yake ndiyo yatakayomhakikishia waziri husika kuendelea au kuachia ngazi baada ya mwaka mmoja tu. Kwa maneno mengine, survival ya waziri itatokana na "perfomance" yake na si vinginevyo.

  Kana kwamba hiyo haitoshi, Rais Kagame hajaishia hapo. Ameenda mbele zaidi. Ameagiza kwamba waziri wa mambo ya nchi za nje naye asainiane mikataba ya "performance" na mabalozi wanaoiwakilisha Rwanda nje ya nchi.

  My take:
  Nchi yetu ingeendeshwa kwa staili hii, sidhani kama kuna waziri yeyote ambaye angesalia kwenye baraza baada ya mwaka mmoja. Labda mmoja au wawili.
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wenzetu wanajaribu, kwa hiyo hata wakishindwa hatutawalaumu. Watanzania tumeshindwa hata kujaribu.
   
 3. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hakika ni Habari njema kwake, lakini je nini kimebebwa kwenye mkataba husika?
  Ni nini kipimo cha uwajibikaji kwa waziri/balozi?
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Bado sijajua kwa undani ni mambo gani yapo kwenye Performance Contract lakini naweza kuhisi kwamba inawezekana mkataba ni wa kiutendaji zaidi kwa maana kwamba una orodha ya kazi anazopaswa kufanya waziri katika kipindi fulani say mwaka mmoja na vigezo vya kupima mafanikio. Kwa wale watumishi wa umma nadhani wanafahamu kitwa kinachoitwa OPEN PERFORMANCE REVIEW APPRAISAL SYSTEM (OPRAS). This is an output-based kind of assessment which has proved success in many countries. Hapa kwetu Tanzania imeshindikana kutekeleza.
   
 5. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hapa kwetu inashindika kwa kuwa "Shughuli"i nyingi kuliko KAZI. Maana leo mtumishi kafiwa na mwanae, tunafunga ofisi, kesho kuna kilele cha siku ya ukimwi duniani, halafu siku inayofuata kuna kikao cha kamati ya ulinzi na usalama baada ya mvua kubwa na upepo mkali kuezua nyumba za wananchi na siku inayofuata tena mwenge unapokelewa na kukimbizwa siku mbili hapa wilayani, siku inayofuata tunamtambulisha mkuu wetu mpya wa mkoa siku nyingine ni ka uchaguzi kadogo kujaza nafasi iliyoachwa wazi ya diwani. " Yuko nje ya Ofisi-njoo kesho".
   
 6. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ndio gharama za kua Dikteta kwa kipindi flani,nampenda Kagame naipenda Rwanda na pia nauchukia Ufisadi ufanywao na viongozi wa serikali ya sisiemu
   
 7. m

  mbweta JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Rwanda wakati wanafyekana tulikuwa tunawaona saiz wameanza kutupita katika maendeleo twawaangalia 2 after few years tutaanza pokea misaada kutoka Rwanda.
   
 8. P

  PreZ 2B EL Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wao wamejari sisi tumethubutu,tumeza na sasa tunasonga mbele
   
 9. k

  kicha JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  hongera kagame, naamini utakua mfano wa afrika na dunia kwa ujumla, hio ni ishara njema ya kua una nia.
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Vema sana Kagame.....keep it up.......
   
 11. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Je yeye Kagame atasaini mktaba wa utendaji wake badala ya kutumia mituriga na rongorongo za kunyamazisha wapinzani wake au ni mkuki kwa nguruwe?
   
 12. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Kagame yupo serious bwana. Siyo huyu Dr. Dr. Dr. Dr. (heshima - UDOM) ambaye kutwa nzima yupo busy anatembeza bakuli la kuomba misaada kwa wenzie. Itafika wakati atafika atapeleka bakuli lake Rwanda.
   
 13. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni mwezi huu waziri wa nyumba na makazi wa Rwanda anapimwa na Kagame kufuatia mkataba alifunga na Rais wa kuhakikisha Hakuna nyumba ya majani Rwanda mpaka december hii.
   
 14. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Na sisi Dr. Dr. Dr. Dr. (heshima-UDOM) atampima Magufuli ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kama amekamilisha ujenzi wa fly-overs jijini Dar.
   
Loading...