Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
KAGAME ASHINDA TUZO YA KIONGOZI BORA AFRIKA.
Mtandao "African Leadership" wa nchini Uingereza uliokuwa unaendesha mashindano ya kuwapata viongozi bora wa Afrika ktk nyanja za kisiasa, na kiuchumi, umemtangaza Rais Paul Kagame wa Rwanda kuwa mshindi wa jumla wa tuzo hizo.
Kagame ametangazwa kuwa Rais bora zaidi Afrika na kuwapiga mweleka washindani wake ambao ni Rais John Magufuli wa Tanzania, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mohamed Buhari wa Nigeria. Kagame ameshinda tuzo hiyo kubwa na ya heshima barani Afrika licha ya Magufuli kuongoza kwa kura, kwa sababu kura haikuwa kigezo pekee cha kumpata mshindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa jarida la African Leadership Magazine ambao ndio waandaaji wa Tuzo hizo Dr.Ken Giammi amesema licha ya Magufuli kuongoza kwa kura lakini alishindwa katika vipengele vingine ikiwemo masuala ya ukuzaji wa uchumi, demokrasia na haki za binadamu.
Muda mfupi kabla ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura, kijana Yericko Nyerere aliongoza kampeni ya kupinga Rais Magufuli kupewa tuzo hiyo kwa kutaja masuala ya kuzorota kwa demokrasia nchini. Bado haijafahamika kama kampeni aliyoiongoz Yericko imechangia kumnyima ushindi Rais Magufuli.
Tuzo hiyo ya heshima zaidi barani Afrika hadi sasa imetolewa kwa viongozi 8 tangu kuanzishwa kwake, ambao ni Dr.Mohamed Ibrahim, muasisi wa tuzo za MoIbrahim (2010), Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia (2011), Atiku Abubakar, Makamu wa Rais mstaafu Nigeria (2012); Xavier Duval, Naibu Waziri mkuu wa Mauritius (2013), Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Tanzania, (2014), Goodluck Jonathan, Rais Mstaafu Nigeria, (2015), na Bw.Mohamed Dewji, Mkurugenzi mkuu wa MeTL, (2016). Na sasa Kagame anakuwa mtu wa 8 kupata tuzo hizo.
Rais Kagame pamoja na washindi wa categories nyingine za tuzo hizo, watakabidhiwa tuzo zao katika sherehe zitakayofanyika tatehe 24 mwezi Febryary mwaka huu mjini Johannesburg, Afrika ya kusini.!
AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE PERSONS OF THE YEAR 2017 WINNERS - African Leadership Magazine