GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nina neno moja tu zuri kwa Mheshimiwa Rais wangu mpendwa leo Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli nalo ni kukushauri tu kuwa kama utaweza ifanye Taasisi ya Mwalimu Nyerere ( MNF ) kama ' Kioo ' chako cha kukuongoza vizuri na hatimaye uzidi kukubalika.
Nasema hivi Kwako nikiamini kabisa kuwa humo ndani ya MNF kuna ' vichwa ' vya maana ambavyo nisingependa kuvitaja hapa ila ' Wasaidizi ' wako hapo Ikulu wanavijua ambavyo viliweza kufanya Kazi zao kwa Kizalendo kabisa kwa nchi hii na sifa zao hadi leo hii wengine wakiwa hai na wengine wakiwa wameshatangulia mbele ya haki ni za ' Kutukuka ' kabisa.
Kuwa nao karibu sana, washirikishe pale unapoona kuna haja ili watumie katika kukusaidia kudumisha umoja na mshikamano wa nchi hii kwani awamu iliyopita iliisahau mno hii Taasisi hadi pale ilipoona inaanguka ndipo ikaifuata na wao bila hiyana na kwakuwa wana uchungu na uzalendo wa kweli kwa nchi hii tokea uhuru wakawa tayari kuipa ushirikiano ndipo kidogo ikawa nafuu kwao Kiuongozi na Kiutawala.
Yangu ni hayo tu Mheshimiwa Rais wangu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kila la kheri na majukumu mema katika kuiongoza Tanzania yetu ili ifikie kule ambako una shauku ya kutupeleka na ambako sisi pia tunaamini kuwa utafanikiwa.
Akhsante na naomba kuwakilisha.