Rais JPM hawa ndiyo baadhi ya Watendaji wako ‘ wanaokuangusha ‘ na kufanya ‘ uchukiwe ‘ pamoja na Serikali yako

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,476
108,603
Katika hali isiyo ya kawaida kabisa na ambayo si tu kwamba imenisikitisha bali pia imenikera mno Mimi An Eagle ni Kitendo cha Mamlaka ya Maji Mkoa wa Simiyu huko Maswa imekuja na maamuzi ya ‘ Kikatili ‘ kabisa kwa Kuwakataza Watu wenye Mabomba ya Maji Kugawa ( Kuwasadia ) Raia wengine ambao hawana Mabomba ya Maji na ‘ wanataabika ‘ nayo pia kwakuwa hawana Uwezo wa kuwa nayo.

Wakiongea kwa ‘ Uchungu ‘ kabisa leo asubuhi kupitia Kipindi Kizuri ( An Eagle ninachokipenda ) cha ‘ Matukio ‘ kinachorushwa na Redio bora kabisa Kanda ya Ziwa kama siyo nchini ya RFA Wakazi mbalimbali wameshikwa na butwaa hasa juu ya aina hii ya Roho Mbaya na ya Kikatili ambayo Wafanyakazi ( Maafisa ) wa Mamlaka ya Maji Mkoani humo wanayo.

Moja yapo ya Kauli ambayo imetolewa na Mmoja wa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo ni hii ninayoinukuu hapa ambayo imesemwa na Mkazi aliyehojiwa…” Tunawaombeni nyie wenye Mabomba ya Maji ni Marufuku kabisa kugawa Maji iwe bure au hata kwa Kuyauza kwa Watu wengine na wasio na Mabomba ili nao wakome na waweze Kumiliki Mabomba yao. Mkiwanyima Maji mara mbili tatu na wakitaabika akili zitawakaa na watawahi upesi kuja Kwetu Ofisini waombe tuwawekee Mabomba. Hata ukiona Mtu ana shida gani na anataka hata Kukata Roho hakuna kumgawia Maji sawa?

Ombi langu la Kwanza kwa Mkuu wa Mkoa huo wa Simiyu anza Kulifanyia ‘ Uchunguzi ‘ wa Kina ‘ Sakata ‘ hili na kama ukikuta ni kweli kabisa basi tunaomba kabla ya Kuchukua hatua utuombe na Sisi Watanzania tusiopenda ‘ Uonevu ‘ tukuchagulie aina ya Adhabu Kali ya Kuwapa ili basi iwe ni Fundisho kwa Watendaji wengine ‘ Wapumbavu ‘ wanaohudumu katika Serikali hii ya Tano ya Rais JPM.

Na pia nawaombeni wale ‘ Wasaidizi ‘ wa Mheshimiwa Rais mfikishieni haraka sana huu Ujumbe ili kuanzia leo hii aanze Kuwajua baadhi ya Watendaji wake ( kama hawa wa Mamlaka ya Maji Mkoani Simiyu ) ambao Kimsingi ndiyo ‘ wanachagiza ‘ Yeye pamoja na Serikali yake nzima ya Awamu hii ya Tano anayoiongoza ‘ Kuchukiwa ‘ vibaya mno na Wananchi wengi.

Hakuna kitu ambacho kinanikera hadi Kunipandisha ‘ Hasira ‘ kama nikiona Watu fulani ‘ wanaonewa ‘ tu au ‘ kudharaulika ‘ kwakuwa hawana Uwezo ( Mafukara ) na huku wakinyanyasika ndani ya nchi yao. Na katika moja ya Wosia ambao Marehemu Bibi yangu aliwahi Kuniambia na mpaka leo hii naukumbuka na nauishi vile vile ni pale aliponiambia kuwa hata Siku moja ikitokea Mtu ambaye ana Shida ya Maji ( Kiu ) au Chakula amekuja Kwangu Kuniomba ( hata kama ni Adui yangu ) basi kama kweli ninayo / ninacho nisimnyime na nimpe mara moja kwani kwa Mungu hakuna ‘ Dhambi ‘ mbaya kama ya ‘ Uchoyo ‘ na ‘ Roho Mbaya ‘ ambao Mamlaka ya Maji Mkoani Simiyu ( Maswa ) wameanza Kutuonyesha Watanzania.

Naomba ‘ Laana ‘ ya Mwenyezi Mungu iwapate Watendaji wote hapo mliohusika na aina hii ya ‘ Ukatili ‘ mkome.
 
Back
Top Bottom