Rais John Pombe Magufuli naomba usikilize ombi langu.

Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Dec 17, 2015
795
479
Mh. Rais wangu mpendwa Pombe Joseph Magufuli. Kwanza kabisa nakusalimu, pia napenda kukupa pole kwa Kazi ngumu uliyonayo ya kuliongoza taifa letu. Mh. Ni muda mrefu nimeleta ombi kwako kupitia mahali hapa la kutaka kuongea nawe kama baba yangu nikueleze Shida niliyonayo.

Nimeamua kupitia hapa nikiwa na uhakika kuwa wewe au wasaidizi wako huwa mnapata nafasi ya kuingia humu na kusoma maoni ya watanzania.

Hata hivyo mpaka leo siamini kwamba imeshindikana kuongea nawe bali naendelea kujipa moyo ipo siku nitaongea nawe.

Mh Rais wangu JPM najua una majukumu mengi sana ya kututumikia watanzania na yawezekana ukakosa hata muda wa kumsikiliza mtanzania mmojammoja, tafadhali kama utashindwa naomba hata kupitia wasaidizi wako unipe nafasi nifikishe ujumbe wangu.

Ni matumaini yangu utanisikia. MUNGU AKUBARIKI.
 
Wenye nchi wakiona mwananchi analalamika watasema mwananchi huyu njaa inamsumbua! Kwa hiyo jiangalie usije ukaambiwa unasumbuliwa na njaa.
 
Back
Top Bottom