Rais John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi Mei mosi

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,908
2,889
Imeripotiwa kuwa Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei mosi mwaka huu najaribu kufikiria atakachozungumza katika hotuba hiyo.

===============================
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu Mei Mosi ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya alisema Tucta waliwasilisha maombi rasmi ya kumuomba Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo na tayari wamepata taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Rais amekubali kuwa mgeni rasmi.

Mgaya alisema hayo jana mjini hapa wakati wa mkutano baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na timu ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi Kitaifa, ambao mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili na kuendelea kuweka mipango na maandalizi ya kufanikisha sherehe za mwaka huu kwa mafanikio makubwa.

Alisema ili kufanikisha sherehe za Mei Mosi, Tucta Makao makuu watachangia nusu ya gharama zote za sherehe nzima na nusu inayobaki itachangiwa na wadau mbalimbali wakiwemo waajiri ambapo kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi Bajeti nzima ya sherehe ya mwaka huu ni Sh milioni 29.6.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Rugimbana aliishukuru Tucta na Serikali kwa ujumla kwa kuupa Mkoa wa Dodoma ambao ni Makao Makuu ya Nchi heshima ya kipekee ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya sherehe ya Sikukuu ya Mei Mosi Kitaifa mwaka huu.

Naye Katibu wa Tucta Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa alisema tayari wameunda kamati ya maandalizi ya sherehe na jukumu kubwa lililoko mbele ni kutafuta fedha na michango kutoka kwa wadau, wengi wao wakiwa ni waajiri serikalini


Chanzo: HabariLeo
 
Nidhamu ya kazi, uadilifu, uzalendo, kuwajibika.....wafanyakazi hewa, bajeti ya mwaka huu,misaada, ufisadi, nchi imeoza kil sehemu, mishahara mikubwa,mwaka huu tujibane tujipange hakuna nyongeza ya mshahara....tufanye kazi tuzalishe zaidi na kurudisha heshima ya kazi!..ataongea kuvunja mikataba ya kununua umeme....sukari kidogo atagusa....na mengineyo!
 
Pia atatuomba tumuombee kama kawaida ili awe na ujasiri katika tumbuatumbua maana kwakweli sio kila mtu anaweza kutumbua jipu
 
Nidhamu ya kazi, uadilifu, uzalendo, kuwajibika.....wafanyakazi hewa, bajeti ya mwaka huu,misaada, ufisadi, nchi imeoza kil sehemu, mishahara mikubwa,mwaka huu tujibane tujipange hakuna nyongeza ya mshahara....tufanye kazi tuzalishe zaidi na kurudisha heshima ya kazi!..ataongea kuvunja mikataba ya kununua umeme....sukari kidogo atagusa....na mengineyo!
Umesahau 'kupunguza PAYE kuanzia July
 
Umesahau 'kupunguza PAYE kuanzia July
Itabidi pia atangaze kima kipya cha chini cha mishahara kwa sekta ya Umma na sekta binafsi, kwa kuwa siyo ubinadamu hata chembe, kwa nchi hii hii moja, wawepo watumishi wanaoishi kama wako peponi kwa kulipwa mishahara ya shilingi milioni 40 na wengine waishi kwa mateso makubwa kwa kulipwa shilingi laki 1 kwa mwezi.

Iwapo mahitaji matatu makuu ya msingi ya binadamu ni chakula, mavazi na malazi, inakuwa hao wanaojilipa milioni 40 kama vile wanamkufuru Mungu, kwa kuwa haiwezekani ndani ya jamii kuwepo na kikundi kidogo cha watu wanaoishi katika utajiri wa kupindukia wakati mamilioni ya wananchi wengine wakiishi katika ufukara wa kutisha ambapo wanaishi kwa kula mlo mmoja kwa siku.
 
Back
Top Bottom