Rais John Pombe Magufuli anahujumiwa na kuibiwa vibaya na watumishi wa BRELA

mimi hati ya kiwanja changu mwanza wilaya ya ilemela hawajaipeleka kwa mkurugenzi wa ardhi ili nipate hati wamekaanayo tu ardhi halmashauri ya ilemela tangu mwezi wa 5 nimemaliza process zote nasikia mpaka uwape chochote
Mkuu kwa hili nakuunga mkono, kichwa, miguu, na ........... mimi kila siku niko pale ni usumbufu usiokuwa na maana, vile vibanda vya pale Ardhi wamenikalili utadhani ni mfanyakazi wao
 
Rais John Pombe Magufuli anahujumiwa na kuibiwa vibaya na watumishi wa BRELA[ MSAJILI WA MAKAMPUNI].
Watumishi hao wao baada kuingia mfumo wa kusajili makampuni kupitia mtandao, wamekuwa kwa maksudi kuchelewa kazi[ Ufunguaji wa kampuni na jina za biashara pamoja na Haki miliki] huku mtu ambaye anawatafuta nje ya mfumo rasmi kufanyiwa kazi hiyo ndani ya saa zisizozidi mbili.

kwa sasa ukitaka kusajili kampuni, kufungua jina la Biashara na kazi kama hizo, kwa mfumo rasmi UTATUMIA ZAIDI YA WIKI TATU , ila kama ukiwatumia internals [watumishi wa ndani wa BRELA] Kazi hiyo utawalipa laki moja tu na ndani ya saa moja inatoka huku yule aliyefuata mfumo rasmi akisubiri wiki tatu .

Watumishi wa BRELA wakifuatiliwa simu zao za mkononi, kwa siku hawa vijana wanaingiza miamala isiyopungua shilingi laki tano huku fedha hizo bora tu wangeongeza watendaji kazi zitoke mapema.

Rais wetu wa wanyonge, tunakuomba kupitia tasisi za kiuchunguzi na ukitaka majina na namba za waghusika tutakupatia uone hujuma unayofanyiwa na hawa BRELA[baadhi ya watu wa IT na kitengo cha usajili.]

kuna makampuni mengi yameshindwa fungua ofis Tanzania kwa kukwamishwa na watu ambao wanalipwa mwisho wa mwezi, wanakula hela za pembeni na wanaofuata sheria hakuna kabisa.

Watumishi hawa hawashughulikii kazi yeyote iliyopo kwenye list[online]kama hujawapa chochote, kwahiyo kunakuwa na kazi nyingi pending na serikali inakosa mapato makubwa , makampuni mengi yanashundwa kufanya annual return kutokana na urasimu huu.

Mh Rais "unibiwa": na hawa watoto, naomba simu zao zichukuliwe, wakaguliwe nyumbani na mali zao utaona ukwasi wa ajabu ambao hauendani na muda na kipato chao tangu waaanza kazi.

Mh Raisi Bila kodi nchi haiendi, tunahitaji reli, madaraja, steiglers gorge na pia ulinzi wa nchi, naomba sana mh Rais kama watendaji wako wataacha hili basi utazidi kuibiwa kitu ambacho hatuta kubali.

andiko lingine nitakuletea wizi wa UHAMIAJI MAKAO MAKUU[watumishi wasio waaminifu wakishirikiana na walinzi getini]

tumsaidie JPM , Tuijenge Tanzania yetu
Swala la kuhujumiwa na watendaji au watumishi sio kwa brela pekee, hili lipo kwa kada zote hata wakurungezi anaowaamini
 
b8b7d751-64a7-4f60-aba9-e26ef1a41fd4.jpg
 
Back
Top Bottom