Rais John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.

Dkt. Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.

3-7.jpg
2-9.jpg
 
Huyu mama ni sawa na mchezaji wa kulipwa anayerudi kucheza league ndogo kumalizia soka lake,msimlaumu sana mwacheni tu akale bata ukikaribia kustafu mambo ya utumishi
 
Mama angeenda kufundisha tu.ulishawahi kuwa boss kwann huoni fedheha
 
Huyu mama ni sawa na mchezaji wa kulipwa anayerudi kucheza league ndogo kumalizia soka lake,msimlaumu sana mwacheni tu akale bata ukikaribia kustafu mambo ya utumishi

Uzalendo ndo alionesha mama na sio maslai binafsi
 
Hizi teuzi zinazomfuata mtu huyo huyo miaka nenda miaka rudi!!! zikikutana na mwanaume mkorofi anaenda kupima dna watoto wake wote!!!!
Manake inatishia usalama wa fikra.
 
Raisi wa nchi, Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu wetu pamoja na Mawaziri wa Wizara zote wote wapo Mji mkuu wetu Dodoma wakifanya kazi, kweli kuna dhamira ya dhati kabisa ya kuhamia Dodoma!


MIG4.jpg


MIG6.jpg


MIG7.jpg
 
Back
Top Bottom