Rais John Magufuli na wito wa uhuru wa kiuchumi uliotolewa na Marcus Garvey 1916

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
RAIS JOHN MAGUFULI NA WITO WA UHURU WA KIUCHUMI ULIOTOLEWA NA MARCUS GARVEY 1916.

Leo 22:30pm 08/06/2020

Kwa wengi, hasa wale waliozaliwa katika miongo mitatu iliyopita, jina la Marcus Garvey litakuwa geni masikioni mwao. Wachache wanaweza kuwa wamelisoma katika vitabu vya historia,

Nchini Jamaica,Marcus Garvey ni sawa na kiongozi wa kidini mwenye hadhi kama ile ya Yohana Mbatizaji katika ukristo,kama ambavyo Yohana Mbatizaji alivyotabiri ujio wa Yesu Kristo na kumwandalia mazingira kwa ajili ya kazi yake,

Ndivyo pia Marcus Garvey alivyofanya kwa kutabiri ujio wa Rastafari Haile Selassie aliyekuja kuwa mtawala wa Ethiopia kati ya mwaka 1930 na 1974,

Tukumbuke kuwa Haile Selassie,Kwame Nkrumah, Julius Nyerere ndio walioanzisha Jumuiya ya nchi huru za Afrika 1963 na kudumu hadi 2002 ilipomzaa Umoja wa Afrika (AU),ndoto yao kubwa ilikuwa Afrika ipate Uhuru na ijiendeshe kiuchumi.

Marcus Garvey mwanaharakati wa Uhuru wa kiuchumi na Mfanyabiashara aliyeweza kuwaajiri watu weusi 1000 katika jiji la New York City kati ya mwaka 1916-1926.

Mpinga unyonyaji na kiongozi katika harakati za watu weusi(black nationalist movement) kwa kutumia mawazo ya kiuchumi ya Pan-Africanists ambayo ilikuwa ni nguzo kubwa ya watu weusi katika maeneo ya mijini enzi hizo,

Marcus Garvey aliamua kuunganisha watu weusi kila mahali duniani lakini mafanikio yake yalikumbwa na athari kubwa chanya na hasi nchini Marekani, ambapo yeye alipigania kuimarishwa na kuongezeka matarajio ya watu Weusi kwa ajili ya haki,Kumiliki mali, na hisia ya jamii.

Baada ya kuwasili mjini New York mwaka 1916, alianzisha gazeti lililoitwa Negro World newspaper, kampuni ya kimataifa ya meli inayoitwa Black Star Line na viwanda Negro Corporation.

Wakati wa miaka ya 1920, Shirika lake la Universal Negro Improvement Association (UNIA) lilikuwa shirika kubwa kidunia katika historia ya watu wa asili ya Afrika na Marekani.

-Ujio wa Rais John Magufuli na Ujasiri wa kuitikia Wito alioutoa Marcus Garvey wa Uhuru wa Kiuchumi.

Kwa miongo kadhaa Afrika imeshuhudia uwepo wa viongozi wenye busara na hekima na hata uzalendo juu ya bara la Afrika, lakini kilichokuwa kinakosekana mara nyingi kutoka kwa viongozi hao ni ujasiri na kusema waziwazi kile ambacho kiongozi anakusudia kwa kumaanisha!

Ujasiri ni siri na tumaini pekee lililokosekana Afrika na lililosubiriwa kwa udi na uvumba,Nani aje kuziba mwanya mdogo wenye madhara katika uwajibikaji kwa muda mrefu!?

Rais John Pombe Magufuli amekuja kama “Tunu” iliyotumwa na Mwenyezi Mungu kuhitimisha shughuli nzito ya kuziba ufa mdogo lakini uliopata kuwa wenye madhara makubwa katika maongozi ya bara la Afrika,

Katika Zama hizi baada ya kupita kwa zama za Haile Selassie,Julius Nyerere na Kwame Nkrumah,Kwa hakika Rais John Magufuli ama ameweza au anakaribia kuuziba ufa ulidumu kwa muda mrefu katika bara la Afrika kwa vigezo vifuatavyo.

-"Hapa kazi Tu" kwa vitendo sio porojo.

Wiki ya tatu toka kuapishwa kwa Rais John Magufuli,Mtandao wa Twitter "ulitikiswa na Trend" ama hashtag #WhatWouldMagufuliDo,

Kwa hakika watumiaji wa Mtandao wa Twitter toka sehemu mbalimbali duniani walionyesha kuridhishwa na hatua za mwanzoni alizochukua Rais John Magufuli kuelekea kuifanya Tanzania kuwa taifa linalojitegemea kiuchumi,

Katika hali inayoweza kuonekana kama miujiza,ikifika hatua kundi la wananchi nchini Kenya liliandamana wakidai "Magufuli awe rais wao"wakionyesha kuchoshwa na tuhuma mbalimbali zinazoandama utawala wa Rais Uhuru Kenyatta,

Kadhalika watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii kutoka kila kona ya dunia walimtumia Daktari John Pombe Magufuli kama "reference" kudai uwajibikaji wa viongozi katika nchi zao,

-Falsafa ya Uhuru wa kiuchumi katika Baraza la Mawaziri la Rais John Magufuli.

Kiungo sahihi katiks kutekeleza falsafa ya Uhuru wa kiuchumi alikuwa ni Daktari Philip Mpango,mchumi wa zamani katika Benki ya dunia na mchapakazi na baada ya uteuzi wake alifanya muujiza wa kuikusanyia Mamlaka ya mapato zaidi ya shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi mmoja tu,

Hii ilileta matumaini makubwa kwa Watanzania kuwa baraza la Mawaziri la Rais Magufuli lipo tayari kuendana na falsafa ya Uhuru wa kiuchumi itayotengeneza taifa la Tanzania lenye kujitegemea kiuchumi,

Daktari Philip Mpango Kama mchumi na Waziri wa fedha wa Serikali ya Rais Magufuli,ni Jiwe lililoua ndege wawili katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda itayokuja kujitegemea kiuchumi,

-Kwa nini Daktari Philip Mpango ni Jiwe la kuua ndege wawili kwa wakati mmoja!?

I)Amekusanya na atakusanya kodi kwa Mafanikio.

ii)Kuondoa matumizi yasiyoendana na kodi iliyokusanywa.

Tatizo la Tanzania halikuwa kwenye kukusanya kodi pekee bali pia matumizi yasiyoendana na kodi iliyokusanywa, Daktari Philip Mpango ameondoa urasimu na daima hajawafumbia macho watu waliobainika kuitumia TRA kama pango la kujinufaisha kiuchumi,

Kwa hakika falsafa ya Rais John Magufuli ya Uhuru wa kiuchumi ilipata watendaji kazi wazuri katika falsafa hiyo,

-Vita dhidi ya Makampuni ya Kibepari,

Kwa muda mrefu taifa letu lilikuwa chini ya mfumo wa kinyonyaji wa makampuni ya kimataifa ya kibepari,Kwa wenye kumbukumbu vizuri kama Kampuni ya Williamson Diamond ya Mwadui tokea miaka ya kabla ya uhuru hadi utawala wa awamu ya nne,

Hakuna mwenye hakika ni kiasi gani cha madini ya almasi kilipatikana tangu wakati huo na hivyo kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kama pato la Taifa kuinua Uchumi wa Tanzania.

Buzwagi,GGM,Mgodi wa North Mara hii ni migodi ambayo ilisifika kwa dhahabu hata Viwanja vya ndege kujengwa katika migodi hiyo,

Upatikanaji wa raslimali hii ya dhahabu ukatafsiriwa kuwa laana badala ya neema na wananchi wengi hasa wa mikoa ya Shinyanga, Mara, Kagera, Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Singida na Arusha.

Kwa wasiofahamu, laana hii inatokana na wananchi kutimuliwa kwenye maeneo yao kwa kisingizio cha uwekezaji baada ya kupatikana kwa madini aina tofauti tofauti.

Rais John Magufuli baada ya kuiona hali hiyo, akaamua kuzuia na kukamata makontena yote ya mchanga wa dhahabu na madini mengine uliokuwa katika hatua za mwisho za kusafirishwa nje ya nchi,

Kwa kisingizio cha kwenda kuchenjuliwa katika viwanda na mitambo ambayo haiko hapa nchini kwa madai kuwa ilihitaji nishati kubwa ya umeme ambayo hatujaweza kuizalisha wala hatutaizalisha kwa siku za karibuni.

Baada ya Rais Magufuli kuunda tume za mabingwa na wanasheria waliobobea katika mambo ya madini, ilibainika baada ya uchunguzi kuwa makinikia hayo yaligundulika kuwa na kiasi kikubwa cha dhahabu, shaba, zinki, cobalt, manganizi, fedha,

Kwenye makontena 77 yaliyozuiliwa katika bandari ya Dar es Salaam yakiwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu zenye thamani ya shilingi bilioni 676 sawa na Dola za kimarekani 307, 292, 720 na kubainika kuwa na kiasi cha dhahabu chenye kilogramu 13,157.5 zenye thamani ya Sh 1, 146, 860,330,000 sawa na Dola za kimarekani 521, 300,150.

Kudhihirisha kuwa wizi huo ni wa muda mrefu, pengine zaidi ya miaka 18, Rais aliamuru Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kulipa fidia ya hasara hiyo pamoja na kodi na mazungumzo kati ya serikali na Barick yamezaa matunda.

Rais John Magufuli akashinikiza marekebisho mapya ya Sheria ya kodi ya madini na kuiamuru Barrick kuafiki marekebisho hayo ama iondoke nchini Tanzania jambo ambalo Kampuni walikubali mabadiliko,wakalipa fidia na ikasainiwa Sheria mpya yenye kutoa umiliki wa ubia katika migodi hiyo kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick.

Ikaundwa Kampuni mpya inayofahamika kwa jina la Twiga Minerals Corporation Limited,

Kampuni hiyo ina makao yake makuu Mwanza, kaskazini magharibi mwa tanzania ambapo Serikali ya Tanzania ina umiliki wa hisa asilimia 16 ilihali barrick ina umiliki ya asilimia 84.

-Rais John Magufuli autafuna mfupa wa Rushwa.

Rais Magufuli ameutafuna mfupa wa rushwa uliomlazimisha Mwasisi wa Taifa hili, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuutungia Kitabu kilichojulikana kama Uongozi na Hatima ya Tanzania,

Kinachozungumzia kwa ukali madhara ya rushwa na uongozi wa taifa letu akionyesha kwa uchungu jinsi rushwa ilivyokuwa inautafuna uongozi na uchumi wetu.

-Nimalizie kwa ujumuifu wa mambo mbalimbali ya Rais John Magufuli aliyoyatenda kwa ufanisi wa hali ya juu na ukamilifu wake.

Shirika la ndege ambalo lilikuwa limekufa kwa miaka mingi, ameweza kulirejeshea uhai kwa kasi.

Sasa Tanzania ina ndege za aina mbalimbali kumi bomberdier,Airbus,Boeing huku alipoingia kulikua na ndege moja mbayo pia ilikua mbovu.

Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa na ndege moja tu tena ilikuwa inafanyiwa matengenezo mara kwa mara, soko la ATCL lilishuka sana hadi kufikia asilimia 2.5.

Lakini sasa tumenunua ndege 7, na nyingine kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner zitakuja mwishoni mwa mwaka 2020" kufanya jumla ya ndege kumi,na nyingine mbili za mizigo tayari zimetolewa order kwa ajili ya kutengenezwa,

Upanuzi wa uwanja wa ndege wa kisasa, hadhi ya kimataifa uliweza kujengwa na umeanza kutumika sasa.

Mradi mwingine mkubwa ambao unaendelea ni wa gari moshi ,Reli ya kisasa inaendelea na ujenzi huku maendeleo ya ujenzi yakionekana kuwa chanya.

Mradi mwingine ambao umekua ukipingwa sana na wahifadhi wa mazingira na mashirika ya kimataifa, ni mradi mkubwa zaidi wa uzalishaji umeme wa Stigler's Gorge,

Uliopewa jina la Bwawa la Umeme la Julius Nyerere,tayari Bwawa hilo litalozalisha megawati 2,200 limeanza kujengwa na linatarajiwa kukamilika mwakani,

Wahujumu uchumi au wale walioitwa mafisadi wameweza kufikishwa na kufungwa gerezani. Majina ya watu maarufu matajiri yaliwashangaza wengi walipoishia gerezani kwa Ufisadi,

Nimalizie kwa kusema Wito wa Marcus Garvey wa Uhuru wa kiuchumi,umeitikiwa vyema na Rais John Pombe Magufuli,

Chini ya Rais John Pombe Magufuli tunajenga Bwawa la Umeme la Rufiji litakalo zalisha Megawati 2,200 ikiwa sasa Taifa letu linatumia Megawati 1,100 tu,

Kwa hiyo Bwawa la Umeme la Julius Nyerere kule Rufiji litazalisha Umeme tunaotumia Sasa mara mbili,hii ni faida kubwa kwa Taifa na shukrani za dhati ziende kwa Rais wetu,Ndugu John Pombe Magufuli.

Baada ya Kujenga Bwawa la Umeme,chini ya Rais John Pombe Magufuli tunakwenda kujenga Viwanda vitakavyotumia Umeme huo kuviendesha,Viwanda vitatengeneza Taifa linalojitegemea ambalo nguzo kuu ya uchumi wake ni sekta ya viwanda.

Tunataka tufike mahali ambapo Taifa letu litakuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi na kutekeleza mipango yake ya maendeleo bila kutegemea misaada.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

Research;Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom