Rais John Magufuli anapaswa kuliomba radhi taifa hili

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,485
18,048
Rais John Pombe Magufuli anapaswa aliombe radhi taifa hili kwa niaba yake na chama chake cha CCM pamoja na marais wenzake waliomtangulia William Mkapa na Jakaya Kikwete kwa kulisababishia hasara kubwa taifa hili kutokana na mikataba na sheria za madini za kinyonyaji walizozipitisha ndani ya bunge kwa kura zote za ndiooo na mbwembwe nyingi kwa kudhani wanakomoa upinzani kumbe wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe.

CCM ndicho kilichotufikisha hapa tulipo leo, mchawi na adui mkubwa wa nchi hii ni CCM, hawa hawana nia njema na taifa hili na wala hawajawahi kuwa nayo hiyo nia njema mara baada ya kufariki baba wa taifa Hayati Julius K Nyerere, wameiba vya kutosha sana katika nchi hii, na wale waliojaribu kuwaonesha kuwa mnaiba ama mmetuingiza chaka kama taifa walikiona cha mtema kuni wakiwemo akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Dr Slaa, John Mnyika n.k na wakaonekana ni maadui wa taifa hili, lakini muda huongea tumeona uchafu wao mchana kweupe waliokuwa wanaufunika funika kwa maslahi ya matumbo yao pamoja na makuwadi wao.

Mzungu hakuja na Vifaru vya kivita kuichukua migodi, bali ccm na Serikali yake waliwaita na wakakaa pamoja na kukubaliana na kupeleka mikataba na Sheria zake ndani ya bunge na kuipitisha kwa vifijo na nderemo kwa kujua wameliibia taifa kwa maslahi ya matumbo yao na ccm yao.

Leo hii eti ccm na rais wao wanatuambia hii ni vita!! Ni vita ya nani na nani?! Hii siyo vita bali ni uozo uliofanywa kwa mkono wa CCM na Serikali yake kwa manufaa yao wenyewe na chama chao, hii siyo vita ni makubaliano kati mwizi na mwizi.
 
Hata mie nimeona jicho lako
 
Mtoa mada una mawazo saafi sana ila, hukujua namna ya kuyaleta mawazo yako. Tafuta tu lugha ya staha utasikilizwa. Sijawahi kumsikia rais aliyejishusha kiasi hicho katika kizazi hiki. Labda kizazi kijacho wakati makosa yatakapo hesabiwa kuwa ndio kazi nzuri. Hivyo, usitarajie neno "samahani"
 
Kwa nchi ilivyofanywa na hawa wapitisha mikataba mibovu alafu wanaanza kulalamika haina haja ya staha
 
Back
Top Bottom