RAIS John Magufuli amewataka wananchi kuchagua vizuri viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika mwaka huu

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1066513


RAIS John Magufuli amewataka wananchi kuchagua vizuri viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika mwaka huu. Aidha, ameagiza vyombo vya usalama, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na viongozi wote wa serikali kufuatilia na kuhakikisha waliolisi Benki ya Wananchi Mbinga wanawajibishwa.

Rais ambaye ameeleza siri ya kubadilisha mara kwa mara mawaziri wa Kilimo, alisema hayo akiwa ziarani wilaya ya Mbinga ambako alihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Makita Mjini baada ya kuweka jiwe la msingi ya ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay.

“Mwaka huu ni uchaguzi serikali za mitaa, hakikisheni mnachagua viongozi vizuri,” amesema jana katika eneo la Kigonsera akiwa njiani kwenda kwenye uzinduzi wa barabara ya Mbinga- Mbamba Bay kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Makita mjini Mbinga.

Alitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuchapa kazi kwa kubadilisha mfumo kuhakikisha inajengwa Tanzania yenye maendeleo. Rais Magufuli ambaye pia alizungumzia shule kongwe ya sekondari ya Kigonsera na azma ya uboreshaji elimu nchini, alisisitiza ifanyiwe ukarabati ipasavyo, akisema ina historia kubwa kwani ndipo alisomea Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi kadhaa wa juu serikalini.

Kwa mujibu wa Waziri, Osi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, Sh bilioni nane zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ukarabati. Akizungumzia huduma mbalimbali za jamii na miradi inayotekelezwa, Rais alisema serikali haiwezi kumaliza utekelezaji wa mambo yote kwa wakati mmoja. “Tunajua hatuwezi kumaliza siku moja, lakini kupanga ni kuchagua… sisi ni binadamu…haya tunayotekeleza ni kwa niaba yenu, mlituchagua bure, tutawatumikia bure,” alisema.

Alihimiza ulipaji kodi akiwahakikishia wananchi kuwa itatumika vizuri. Waliolisi benki “Waliolisi benki wako wapi? Je, vyombo vya usalama viko wapi? …Naachia vyombo vya usalama. Fuatilia Benki ya Mbinga Community imelisika na leo haipo na wananchi wanahangaika nani aliyeilisi? “Lazima tutafute mzizi wa tna na si kufunika.

Wako watu ambao utajiri wao ni kutokana na mali za masikini waliowadhulumu,” alisema na kutaka Mkuu wa Wilaya, Takukuru, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) na Mkuu wa Mkoa kuanza kushughulikia suala hilo. Akijibu malalamiko ya Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda kuhusu wanunuzi wa kahawa kuwapunja wakulima, alisema, “Wataje hawa waliokuwa wanawadhulumu watu wako.

Ungenikabidhi mimi majina ungeona…lakini unayafumba haya mambo maana yake hutaki kutafuta dawa. “Nataka majibu yapatikane. Viongozi mko hapa waliokuwa wananunua kahawa, wapo hapa, mkuu wa wilaya uko hapa, mkuu wa mkoa uko hapa hata waziri wa kilimo yuko hapa.

Shirikianeni na wizara na vyombo vya ulinzi na usalama tunataka haya tuyakomeshe,” alisema. Kubadilisha mawaziri Rais Magufuli amesema mateso wanayopata watu wanyonge yapo kila mahali. Alisema yako kwenye korosho, kahawa, pamba, chai hivyo anachotaka ni kuona mambo hayo yanabadilika. “Na ndiyo maana nimekuwa nabadilisha Waziri wa Kilimo.

Bado sijachoka kubadilisha, nimebadilisha mara tatu, mara nne. Namshukuru Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ameanza kujitahidi,” amesema na kutaja na kutoa mfano wa kazi nzuri ni pamoja na kuanzisha mnada wa kahawa mjini Mbinga.

Magufuli ambaye aliendelea kusisitiza kuwa kupata uwaziri katika kipindi chake ni mateso, alisema pia wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi hawana budi kuombewa kwani kazi yao ni ngumu na hawajui kesho itatokea nini.

Akitaja pia wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya na makatibu tawala, amesema, “Nataka niseme kwa dhati wote ninaowateua, hawajaniangusha wanajitahidi sana. Mnaowaona wote ambao bado wako, ujue wanafanya kazi.” Akikemea rushwa na vitendo vya kughushi (u-hewa), Magufuli alihoji sababu za viongozi wanaopewa madaraka kuwa wabinafsi.

Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekuwa mbinafsi Uhuru usingepatikana. Alisema watu waliozoea vya bure hawatavipata kwani serikali iko imara. “Ndiyo maana mkisikia kelele ni wale waliozoea vya bure; hawatavipata ng’o.” Akizungumza barabara aliyoweka jiwe la msingi, Rais Magufuli alisema Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya China Company Group ilikuwa imalize ujenzi mwaka 2021, amemwambia aikamilishe mwakani. Alisema kwa vile Sh bilioni 134.72 zipo na mfadhili Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ameshaleta fedha, hakuna sababu ya kutumia kipindi kama walichokuwa wametaja badala yake wafanye kazi usiku na mchana ikamilike mwakani.

Alizungumza na wananchi katika eneo la Makita Mjini Mbinga baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay itakayogharimu Sh bilioni 134.72.
 
Back
Top Bottom