RAIS JOHN MAGUFULI AMETANGAZA NEEMA KWA WASANII

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
TIMES FM RADIO on Fri, 02/19/2016

iku4-559x520.jpg




Rais John Magufuli ametangaza neema kwa wasanii ikiwemo kuamuru Mamlaka ya Mapato (TRA) kufanya operesheni maalumu dhidi ya kazi za wasanii za nje ya nchi zikiwemo CD zinazouzwa mitaani bila stika, hatua stahiki zichukuliwe.

Magufuli ambaye ameahidi kukutana na wasanii angalau kila mwaka, pia amekubaliana na maombi ya kutaka haki ya ubunifu isisimamiwe na Chama cha Hatimiliki cha Tanzania (Cosota), kilicho chini Wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji badala yake iwe chini ya wizara yenye dhamana ya wasanii.

Alisema hayo jana kwenye hafla iliyokutanisha wadau mbalimbali walioshiriki kwenye kampeni zake za urais mwaka jana; Wengi wao wakiwa wasanii aliowahakikishia kuwa ameanza nao, atamaliza nao na hatawaacha.

Akizungumzia wizi wa kazi za wasanii ikiwemo kusambaa kwa CD zisizo na stika, Rais Magufuli alisema kama ambavyo TRA imefanya kazi kubaini kontena zisizolipa kodi, alitaka ifanye hivyo pia kwa upande wa kazi hizo za wasanii. Utaratibu huo wa kubandika stika kwenye kila nakala ya kazi itakayosambazwa, ulifikiwa na serikali ikiwa ni hatua ya kupambana na wizi wa kazi za wasanii .

Kuhusu Cosota, Magufuli aliwataka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri mwenye dhamana ya sanaa, Nape Nnauye, kuhakikisha mambo yanayohusu wasanii yanakuwa chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo .

Alisema masuala ambayo hayahitaji kwenda kwenye Baraza la Mawaziri au bungeni, yafanyiwe kazi mara moja. Alimtaka Waziri Nape amwandikie Waziri Mkuu, ili mambo yaliyo kwenye mamlaka yake (Rais) ayafanyie kazi mara moja wasanii wanufaike na kazi zao.

Cosota ilianzishwa kwa mujibu wa Sehemu ya 46 ya sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Namba 7 ya mwaka 1999.

“Nataka wasanii wafaidike na haki na ubunifu wao. Wamepewa vipaji na Mungu, haiwezekani mtu mwingine ndiye afaidi kazi yake,” alisema Magufuli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom