manywangari jean malonkwa
Senior Member
- Mar 17, 2016
- 193
- 188
Upinzani wa Tanzania umeendelea kuwa ule ule. Wanaishi kwa hoja za matukio, hawana mipango na Sera za kueleweka za mda mrefu.
Kibaya zaidi wamekuwa wakiongea mambo ambayo sasa tumepata uhakika wanayasikia mtaani na bila kuyafanyia utafiti wanayadandia ili mradi wanajua yatawapa nafasi kwenye media na kwakuwa Watanzania wengi hatuna tabia ya kuhoji basi tutakurupuka kama walivokurupuka.
Nitatoa mifano michache hapa kuonesha msingi wa hoja yangu;
1. Mbowe alishawahi kunukuliwa akisema Lowassa ni dhaifu, lkn ni Lowassa huyu ambaye ameleta msisimko mkubwa sana uchaguzi uliopita, na Mbowe alimshangilia sana.
2. Lema alishawahi kusema Lowassa ni fisadi na ni heshima kwa mungu kumzomes lkn kwenye hotuba yake inayosambaa kwenye mitandao anamtaja Lowassa kama shujaa na mtu mhimu kwa CDM.
3.Msigwa alishawahi kusema wanaomshangilia Lowassa wakapimwe akili, lkn baadaye yeye akawa mshangiliaji maarufu wa Lowassa na hadi leo hajatoka hadharani kueleza kama amepima akili yake.
4.Kubenea na Mnyika na Lissu waliwahi kutuhakikishia kuwa Lowassa ni fisadi na wanaushahidi na kuwa hasafishiki lkn Lowassa amesafishika na wao ndo walishika madodoki.
5. Walimbeza sana presided wa awamu ya 4 Leo wameibuka na stori kuwa wamemmisi.
Ninachotaka kusema, hawa ni watu wanaoheshimika na wanatoka ndani ya chama cha upinzani kinachoonekana kuaminika zaidi.Wanayoongea yanachukuliwa na kuaminiwa na watu pengine hata kuyaishi.
Wengi tunaamini baada ya kilichotokea mwaka Jana wangebadili aina ya Siasa na kujikita ktk mikakati badala ya matukio. Madhara ya kilichotokea uchaguzi uliopita na wanachoendelea kukifanya ni kuwa hata kama wanayoyaongea sasa ni ya kweli lkn watu wanaojielewa hawawez kuwaamini tena, bali wanawaona kama watu wanaojitafutia umaarufu kama walivyofanya miaka 8 iliyopita na kuja kuyakana yote waliyokuwa wameyasema nyuma.
Kwa msingi huu kuna kundi kubwa la watu ambao wanayapuza haya wanayoyaibua sasa kwakuwa wanawaona kama hawa watu ni watu wasio jua wanachokifanya.
Kwa msingi huu Raisi Magufuli awapuze hawa watu kwa kuwa watampotezea mda wake kama walivyofanya kwa watanzania miaka nane iliyopita. Hawa wanajitafutia umarufu tu wa kisiasa hivyo wataokota kila takataka wanayodhani itawasaidia kujijenga kisiasa. Magufuli anatakiwa aendelee kusimamia yale anayoyaamini na aendelee kuwaamini wale wote anaodhani watamsaidia kutekeleza mipango yake.
Hawa achane nao maana hayo wanayoyapinga yanaweza kuwa hoja zao za msingi miaka michache ijayo na hao wanaowaita majina kibao wanaweza kuja kuwa wacheza ngoma wao maarufu huku mbeleni.
Hakuna kisichowezekana kwao, kwa sasa wamekosa sifa kuu ya wanasiasa na chama makini ambayo ni kuaminika na kusimama ktk Yale wayasminiayo yaani kutokuwa vigeu geu.